Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Asee!,unauatafuta mkopo kwa jasho na damu na rushwa juu alafu bado unakutana na mlima wa riba.
 
Maisha ya kutumia ^kata fupi^ (short cut), ndivyo yalivyo hasa. Hii kitaalam inaitwa ^Kutumia nguvu nyingi bila maarifa^ Anyways, bourgeoisies kazi yao ni kuhodhi rasilimali na fedha, kwa hila na mabavu, ili maskini na walalahoi wawapigie magoti na kuwaabudu.

^Of all passions of the human race, the appetite for dominion is the most intoxicating^ ~ St. Augustine
 
Bora useme ukweli kuliko kukaa kimya !

Uwezi kusafiri kwa wenzako ukaona wanakitu kimoja tu mfano mafuta,kilimo,utalii na n.k lakini kinawanufaisha mpaka unabaki kusema kwa nini hawa wapo hivi!

Kwa nchi yangu ina madini,kilimo,bandari,utalii,usafirishaji nchi za mipakani kwenye maitaji na n.k lakini hivi vyote bado ni kichwa pasua kwa serekali yetu!

Tuje kwenye makusanyo ya mapato TRA,manispaa,tarura ,polisi na faini,utaifishaji na kila kona unapokwenda utakutana na rungu la serekali pesa inapatikana.

Tuje kwenye misaada ambayo kila siku unasikia serekali inapokea pesa sijui bilioni,tilioni hivi vyote vina kwenda wapi!


Kusema ukweli kuna tatizo ya kuangalia hili.!
 
Hakika sasa ni miaka 60 toka tuwe huru kama taifa. Tanzania tumebarikia sana kuwa na raslimali kila mkoa raslimali ambazo nchi nyingi hawana.

Kuna nchi zina bandari tu lakini uchumi wa nnchi na wa wananchi wake ni mzuri. Kuna nchi hazina kabisa raslimali zinategemea misaada na mikopo lakini wananchi wake wanaishi vizuri.

Tanzania tuna watu mil. 60 hiyo ni nguvu kazi ya kutosha kama watapangwa vizuri kila mwananchi afanye kazi

Tuna ardhi nzuri kwa kilimo na ufugaji lakini ni sehemu ndogo tu ya ardhi inayotumika tena kwa kilimo kusicho na tija zaidi ya ugali tu.

Kilimo cha jembe la mkono kilimo cha kutegemea mpaka mvua zinyeshe.

Tanzania tuna bandari, mbuga za wanyama gesi makaa ya mawe madini ya kila aina mlima kilimanjaro misitu mikubwa lakini vyote hivyo vimeshindwa kututoa kwenye dimbwi la umasikini.

Tanzania imekuwa nchi ya kukopa ili kujenga madarasa na zahanati kweli? Tunakwama wapi?

Ushauri

Binafsi naamini kikwazo cha kupata maendeleo na uchumi wa Tanzania upo kwenye uongozi na siasa hapa ndio pana shida. Haiwezekani nchi tajiri kwa kuwa ba raslimali hizi iwe masikini na wananchi wake na ili ijenge madarasa.

Itegemee kodi za hao wananchi wake masikini na mikopo na misaada ya mabeberu.
 
Mtu kama unapenda kusaidiwa kila jambo hauwezi kutoboa.Misaada mingi ni laana
 
Nikiangalia Nchi kama Oman huwa najiuliza yaani mafuta tu ndio yamewapa utajiri huu
 
Kama baba anakula hadi msosi wa watoto unategemea nini? na aina ya wabunge wetu ndio hao kina babu tale umasikini lazima uendelee tu hakuna namna
 
Kuna wakati najiuliza tumemkosea nini Mungu wetu mpaka huu umasikini wa watanzania upo kwa miaka 60 sasa licha ya Mungu kuibariki nchi hii kwa kuipa raslimali karibu kila mkoa lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa?

Raslimali zilizopo Tanzania hakuna nchi ya kufanana nayo Afrika Mashariki na kati.

Viongozi wetu kwa miaka 60 ni wale wale chama ni kile kile lakini wameshindwa kuzitumia raslimali tulizopewa na mungu kuwaondolea umaskini wananchi wake, badala yake wameamua kuwatoza kodi za maumivu na kukopa nje mpaka deni la taifa limefika tril 71 lakini umaskini upo pale pale.

Binafsi naanza kuamini Tanzania tuna tatizo na Mungu ni wakati kama taifa kufanya maombi na kuombana msamaha kwa maovu tuliyofanyiana ili Mungu arudishe upendo wake kwa nchi tupate maendeleo na wananchi wanufaike na kuondokana na umaskini kwa kutumia raslimali alizotupa Mungu.

Kuna watu wapo magerezani kwa miaka kwa kesi za kuonewa, kuna watu wamepigwa risasi, wamepotea, wameuawa kwa uonevu tu.
Yote hayo Mungu hapendi na hasira ya Mungu huwa ni mateso kwa watu.
 
Maelezo yako ni mazuri ila Mimi naamini Mungu anaipenda sana Tanzania licha ya mabaya yote tunayoyatenda. Kuhusu umaskini wetu sababu zake ni nyingi lakini kubwa ninaloliona ni mgawanyo mbaya wa raslilimali ambazo zinawanufaisha wachache.

Urasimu mkubwa sana ambao unafanya shughuli za kiuchumi za sekta binafsi kukwama, kilimo chetu kutopewa umuhimu unaostahili na miundo mbinu ya maji,umeme, barabara nk kutotolewa kwa uwiano unaoridhisha kati ya mijini na vijijini na mengine mengi.

Kiongozi thabiti, mkali atakayesimamia maneno yake na kufuatilia utekelezaji wa watendaji wa ngazi zote za uongozi na kuwarudishia Wananchi spirit na hamasa ya kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii na awe tayari kuchukua maamuzi magumu bila kuangalia sura ataipeleka mbele Tanzania bila kujali anatoka chama gani. Ni maoni yangu tu
 
Back
Top Bottom