Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Wakulaumiwa ni Sumaye na Lowasa walikuwa viongozi wakubwa lakini wakafilisi nchi.

Tunakuwa masikini kwa kuwa na watu kama hawa wanaojibu maswali muhimu ya kujitafakari kirahisi kwa ushabiki wa vyama
 
Pascal, why are we "ignorants"? Why did we allow ourselves to be that way? And why "us"? Is there any causal effect behind this awful phenomenon? Or is it just an arbitrary object of perception? Lastly, are we in control of this "ignorance"? Or is someone else pulling the strings to make us "ignorant", and thereby, poor?
We are ignorants kwa sababu we have chosen ignorance!'
Umechoshwa na Ujinga, Umasikini, Maradhi, Rushwa na Ufisadi?!, 25/10 "Give It, "Just One More Try!"

P.
 
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 Tulikua sawa kiuchumi na Nchi nyingi sana mojawapo ni Singapore Nchi nyingine ni Malaysia
Leo hii wenzetu wako mbali sana wametuacha haswa
Nini hasa kinatufanya tushindwe kuendelea ukizingatia hii Nchi Imejaliwa kua na Rasmali nyingi sana
Nataka tujadili kilichotukwamisha pia Ni mhimu kila Mmoja baada yakueleza kilichotukwamisha nivizuri kuhitimisha kwa kutoa Na Suluhisho
Je miaka 50 ya uhuru tunasitahili kuwa Hapa tulipo?
Karibuni Tujadili
 
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 Tulikua sawa kiuchumi na Nchi nyingi sana mojawapo ni Singapore Nchi nyingine ni Malaysia Leo hii wenzetu wako mbali sana wametuacha haswa
Nini hasa kinatufanya tushindwe kuendelea ukizingatia hii Nchi Imejaliwa kua na Rasmali nyingi sana Nataka tujadili kilichotukwamisha pia Ni mhimu kila Mmoja baada yakueleza kilichotukwamisha nivizuri kuhitimisha kwa kutoa Na Suluhisho
Je miaka 50 ya uhuru tunasitahili kuwa Hapa tulipo? Karibuni Tujadili

Hili swali watu wanauliza sana. Maendeleo ni
  1. Uongozi bora - uzalendo, umakini na uwajibikaji katika kulitumikia taifa na kutumia rasilimali zetu kwa ajili ya maendeleo yetu
  2. Siasa safi - demokrasia na sera nzuri zenye kulenga kuleta maendeleo
  3. Watu - walioelimishwa na ili kuwa nguvu kazi ya nchi
  4. Ardhi - kama rasilimali/mtaji , mazao, madini, maji nk
Sasa pima mwenyewe, tatizo liko wapi, na Malaysia na Singapore walitumiaje hivyo vitu vinne hadi wakaendelea na kutuacha nyuma
 
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 Tulikua sawa kiuchumi na Nchi nyingi sana mojawapo ni Singapore Nchi nyingine ni Malaysia
Leo hii wenzetu wako mbali sana wametuacha haswa
Nini hasa kinatufanya tushindwe kuendelea ukizingatia hii Nchi Imejaliwa kua na Rasmali nyingi sana
Nataka tujadili kilichotukwamisha pia Ni mhimu kila Mmoja baada yakueleza kilichotukwamisha nivizuri kuhitimisha kwa kutoa Na Suluhisho
Je miaka 50 ya uhuru tunasitahili kuwa Hapa tulipo?
Karibuni Tujadili
Halafu inawezekana kuwa ndiyo nchi ambayo serikali yake imejaa masomi matupu yenye Phd na uprofesa hapo unapata marais wote wawili na pia ujue ndiyo nchi pekee duniani anayoongozwa na marais wawili wote ni madokta. Ukitazama baraza la mawaziri utakuta ni madokta na maprofesa wamejaa kibao. Pamoja na usomi wote huo lakini ndio hivyo ni wa theory tu sio wa vitendo. Biashara kubwa pamoja na usomi wote huo ni siasa tu na kubinya uhuru na demokrasia na mauaji. Hayo ndiyo maendeleo tunayojivunia
 
Nani kakwambia nchi yetu haisongi mbele? Hivi unajuwa mwaka 1961 ilikuwa wapi na mwaka huu ipo wapi?
 
Hili la uzalendo kwa kweli linatuumiza sana,yaani sisi Watanzania ni wavivu sana.Hatujitumi kwenye kazi.Of course na Serikali zinatoa huduma kwa wananchi ni two ways.Ndiyo maana nikiwa jijini Perth (Australia) siku moja na ushamba wangu nikachukua taxi inipeleke kwenye mkutano Fulani dereva wa Taxi akabaki kunishangaa nikamuuliza kulikoni,akaniambia kuna "daladala" za bure hapa katikati ya jiji kwa nini unachukua tax?

Kwa sababu nilishapanda taxi nikamwambia yule mzungu twende bwana.,Tulipofika nikamlipa.Akaanza kuzitenga hela nilizompa nikamuuliza kwanini unazitenganisha akaniambia hizi ni za "TRA " ya huko na zingine ndizo za kwake,nikaendelea kumdadisi ndipo akanieleza kwamba anasikia furaha sana kulipa kodi kwani watoto wake Serikali inawajengea shule nzuri,hospitali na huduma zingine bure nk.Nikashuka na kuondoka zangu.Itaendelea.............
 
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 Tulikua sawa kiuchumi na Nchi nyingi sana mojawapo ni Singapore Nchi nyingine ni Malaysia
Leo hii wenzetu wako mbali sana wametuacha haswa
Nini hasa kinatufanya tushindwe kuendelea ukizingatia hii Nchi Imejaliwa kua na Rasmali nyingi sana
Nataka tujadili kilichotukwamisha pia Ni mhimu kila Mmoja baada yakueleza kilichotukwamisha nivizuri kuhitimisha kwa kutoa Na Suluhisho
Je miaka 50 ya uhuru tunasitahili kuwa Hapa tulipo?
Karibuni Tujadili
sio Malaysia na Singapore pia na jilani yetu Kenya Botswana nk tulikua tunawazidi lakini kwa sasa.....huwezi kuamini kwamba budget ya kenya airways ni zaidi robo ya budget yote ya Tz kwamwaka duh nani Mchawi wetu
 
Wambandwa,

Jibu ni rahisi sana! Ni ccm+ujinga wa Watz. CCM ni janga kama ilivyo majanga mengine, na sasa ivi wamejigeuza kikundi cha ugaidi! What do you expect
 
Haya ni maoni ya mdau fulani humu JF, niliyapenda mno, nyie mnasemaje?!

KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI

1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.

2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.

3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.

TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?
 
KWA NINI WATANZANIA WENGI NI MASKINI?

Sijawahi kumwona Mtanzania kwa wakati wowote ule ameondokana na umaskini, umaskini ambao sasa ni mkubwa mno na unakaribia kutudidimiza.

Binafsi nauchukulia umaskini kama kukosekana kwa mahitaji ya lazima ya kila siku kwa mwanadamu: malazi mazuri, chakula bora (ambavyo hivyo vyote vinapatikana kama binadamu huyo huyo anakuwa na njia ya kujipatia kipato) na uongozi bora wa haki unaofuata sheria (ili huduma mhimu za jamii: shule, hospitali, barabara, maji salama nk vipatikane).

Watanzania wengi tu maskini wa kutupa kwa sababu tunagharimia mno uendeshaji wa kila siku wa serikali yetu (isivyokuwa lazima).

Wanasiasa ndio watoa maamuzi hata ya kitaalauma hata kama si wana taaluma husika.

Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana. Kihio kutoka A. Kusini analipwa mamilioni ya pesa hata kama utendaji wake ni mbovu. Mfano NET GROUP SOLUTION, wanaishi maisha ambayo hata kwao hawana. Na wazawa waliokuwa nao wanajilipa pesa ambayo haina mfano.

Wanasiasa wanajilipa pesa nyingi ukilinganisha na wataalamu waliosomea taaluma mbali mbali.

Tatizo la wanataaluma kutothaminiwa limewasukuma baadhi yao kujiingiza ktk siasa. Hapa ndo kichekesho kinatokea. Mwana taaluma huyo huyo akiwa nje ya siasa anakuwa critic wa governing system! Kuna prof. mmoja ambaye ni waziri kwa sasa wakati akiwa chuoni alikuwa ni mtu ambaye aliponda jinsi nchi yetu inavyoongozwa shaghala baghala, alivyoukwaa ubunge huko kwao akateuliwa ktk baraza la mawaziri.. nasikia alikwenda kuwashukuru waliompigia kura kwa dege la jeshi kwa gharama ya serikali. Wako wengi wa aina hiyo.

Elimu ya mafunzo ya darasani na hali halisi iliyoko nje katika jamii inapaswa kuwa lila na fila. Unaelimishwa ili uweze kutumia elimu katika maisha yako ya kila siku.

Ktk hali hiyo, mwanafunzi anaye hitimu darasa la 12 au 14 ni vizuri aongeze na taaluma kama uhandisi (VETA), uhasibu nk. Wa chuo kikuu huyo tayari ni wakutumika ama kwa kujiajiri au kuajiriwa. Kujiajiri hapa ni kimbembe tatizo linakuwa mtaji.,..

Viongozi: Kama nilivyoeleza hapo juu, waviongozi wetu mara wachaguliwapo kuingia madarakani ni moja kwa moja wanona matatizo yao yamekwisha, hivyo swala la kumshirikisha mwanachi wa kawaida, labda ingekuwa kupiga kura kunakaribia.

Mila na desturi zetu: kuna jitihada za makusdi kuzifilisisha.... (ni mjadala mrefu).

KWA KIFUPI UMASKINI WETU UNATOKANA NA KUTOKUWA NA VIONGOZI WAADILIFU, WAONGOFU, WACHA MUNGU. TULIOKUWA NAO NI WANAFIKI NA WAFISADI.

===================

Return Of Undertaker anasema,

KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI

1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 54 tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza Afrika Mashariki.

2.Tz Kwa miaka 38 imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao la TANU na ASP.

3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa
ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.
Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa
Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwa
na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),
Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na
Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na
kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na
Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika
kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana
hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya
kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.

TATIZO NI NINI? NANI ANAFAIDI HUU UTAJIRI? NANI WA KUMLAUMU? NANI NI SABABU?
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?

===================================
Mtaalam aeleza kwanini Tanzania ni maskini
Hii discussion inaweza kutupa mwanga wowote wa kuleta maendeleo ya kweli Kwimba?
 
Inaweza, swala tubadilike, kama mwendo ni viwanda basi iwe hivyo, viwanda iwe kama wenzetu 24hrs, makazini tuwe wapiga kazi, wateja waheshimiwe na services ziwe bora, tuache kufikiria wizi tu kila wakati, au kufanya kazi machache tukiwa kazini, tufuate sheria na taritibu za nchi, kuendeleza ubunifu wetu kwa kila tufanyacho, tuamke, mbona tunafika tu..
 
Back
Top Bottom