Nadhani unge rephrase kichwa cha mada na kuwa "Kwa nini Afrika ni bara maskini?"
Ila mwisho wa siku, baada ya kufanya kila aina ya diagnosis na kudhani mmejua au tumejua sababu ya nini sisi kuwa maskini, ukweli unabaki palepale kuwa sisi Miafrika ni Ndivyo Tulivyo na hiyo ndiyo sababu kuu (underlying reason) ya umaskini wetu na yote yaliyowahi kutokea Afrika pamoja na utumwa na ukoloni.
Hapana mkuu wangu sio Afrika yote maskini, maskini sisi na walalahoi wengine ambao hawafahamu pia ni maradhi gani yamewapata. Nasema hivi kwa sababu hata Ulaya kuna mataifa masikini tena maskini zaidi yetu na wao ni wazungu kuliko wazungu wa Uingereza maana Uingereza leo hii imejaa Machina, Wahindi, Wayahudi na mataifa mengi ambayo naweza kabisa kudai kwamba Mataifa tajiri duniani ni yale yenye mchanganyiko mkubwa wa wageni.
Hili neno Utumwa na Ukoloni ndilo nataka sana kuliewa vizuri sana maanake ikiwa kweli umaskini wetu umetokana na Utumwa na ukoloni hivi dawa yake nini haswa?..kuondoa viongozi wenye fikra za Ukoloni au sisi sote tujenge fikrazipi maanake kweli hadi leo hii nchi zote za Kiafrika zinategemea akili ya mzungu ktk kila strategy inayotumika.
Nitarudi ktk mfano wa WATU na MAZINGIRA, unajua toka mkoloni tulizoea ukienda Hospital unapewa dawa, sasa tabia hiyo imeendelea hadi leo kiasi kwamba daktari anayepokea mgonjwa akataka kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kutoa dawa kuitwa sii daktari mzuri. Tunataka ukisha fika hospital dakati awe tayari na dawa mkononi iwe sindano au dawa ya kumeza..Na wakati mwingi dawa ya kumeza haiaminiki zaidi ya sindano, meaning sisi wenyewe tayari tumekwisha jenga fikra za kupona kwa sindano zaidi ya vidonge..Je, ni fikra hizi zinazotokana na utumwa kiasi kwamba tunaendeleza fikra hizo hata ktk dunia hii ya uchunguzi kabla ya kutibu?.
Mkuu, mimi bado nipo palepale, NDIVYO TULIVYO ni somo kubwa sana ambalo linaweza kujaza vitabu volume 10 kwa urahisi kabisa, lakini pamoja na hayo yote ni lazima kuna tofauti ya maradhi ya Umaskini kama vile Zimbabwe wanakwisha kwa sababu ya gonjwa la Ukimwi na Tanzania inaongoza kwa vifo kutokana na Maleria.. yote ni maradhi lakini imani yangu inanituma kwamba dawa ya Zimbabwe kuondokana na Umaskini (ukimwi) haiwezi kuwa sawa na dawa itakayotumika Tanzania kuondokana na Umaskini wetu (Maleria)..Pia maradhi ya Tanzania yanatibika tofauti na Ukimwi wa Zimbabwe ambao hata wataalam wanapendekeza kinga.
Halafu kwa kuongezea tu, ni jinsi gani maradhi hutibiwa?... Je, inapotokea pendamic ni muhimu kuzuia maradhi kusambaa au kinachotangulia ni kuweka karantini waathirika ili maradhi hayo yasisambae.. mfano huu unahusu scandal kama za mafisadi. je, kinachotakiwa ni kuweka sheria kinga ya Ufisadi (chanjo) kwa wananchi wote au kuwasweka mafisadi wote ndani lupango (karantini) hao mafisadi waathirika.
Mkuu najaribu kutafuta jibu aloshindwa kulijibu JK.. nikiwa na maana kuwa hapa JF wapo wasomi wanaoweza kunifunulia..kwa sababu ikiwa sote hapa tuliweza kumbeza JK kwa majibu yale ina maana wapo watu hapa wanaelewa vizuri kwa nini Tanzania ni nchi maskini.. Na kama jibu la Watanzania wengi wasomi hapa JF ni sawa na lako, sasa kweli unaweza kumlaumu JK kwa kushindwa kujibu hoja ile? yaani tulitegemea JK aseme Sio Tanzania tu, Afrika nzima ni maskini kwa sababu NDIVYO TULIVYO!
Ingeleta maana kweli kwa kiongozi wa nchi kutoa majibu kwamba kushindwa kwetu kunatokana na laana a Curse, kama alivyohitimisha mkuu Son of Alaska!