Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?



Nyerere anaondoka ni 3 percent tu walikuwa wanakwedna sekondari. Vilevile Mzee Mwinyi ku-ruhusu private schools kuliongeza sana wanafunzi. Labda wewe ujarudi Tanzania ndio maana unafikiri kwenda form I bado ni sherehe ya kijiji ya kuchinja mbuzi.
 
Zakumi,
Hatuongei maneno matupu...nipe Takwimu zako..
 
Nyerere anaondoka ni 3 percent tu walikuwa wanakwedna sekondari. Vilevile Mzee Mwinyi ku-ruhusu private schools kuliongeza sana wanafunzi. Labda wewe ujarudi Tanzania ndio maana unafikiri kwenda form I bado ni sherehe ya kijiji ya kuchinja mbuzi.

3% kutoka vyanzo gani. Tupatie source nasi tujiridhishe
 
Mkandara,

I know, with complete certainty, that only 1,800 youngsters completed Form 6 in 1974. It so happens that I was one of them! I thank the Good Lord who arranged matters in such a way that I did my Forms 5 and 6 at Mkwawa. That way, I did get to do some actual studying, rather than hand hoe farming, for my A-levels.

I have lately realized that Mwalimu preferred to see pupils in the fields rather than in classrooms. No wonder he didn’t bother to supply schools with desks!

I see that you conveniently refuse to acknowledge the fact that Mwalimu under funded education. From independence up to 2007, Kenya spent 20 – 27 % of its budget on education, year in and year out. In the meantime, while trying to get us to “run while they walk”, Mwalimu proceeded to reduce our educational funding from 20% of the budget to a measly 4.9%!

Mwalimu used to say that “Tusipolima tutakufa!” I’ll paraphrase him and say that “Tusiposoma tutakufa!” Didn’t Mwalimu realize that education was the conditio sine qua non for development? Thanks to his neglect of it, we have become the economic backwater of East Africa! You want to toast him for the condition we find ourselves in. I refuse to join you!
 
Are you cooking the data or quoted somewhere. Please try to indicate the source of your data so that others can make reference otherwise we will not understand you!
 
Mambo aliyofanya Mzee Mwinyi:
1.UHURU WA KISIASA.
Kuruhusu mfumo wa vyama vingi.Hata kama kulikuwa na shinikizo, Regime nyingine zipo tayari kuingiza nchi kwenye vita,ili kulilinda tabaka tawala.

2.UHURU WA KIUCHUMI
Watanzania waliruhusiwa kujihusisha moja kwa moja na shughuli za kiuchumi.Mnakumbuka enzi zile hutakiwi kuwa na hisa kwenye kampuni ya kibepari.

2.UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Alijenga msingi imara wa vyombo binafsi vya habari.Uhuru wa vyombo vya habari mnaoinjoi leo ni matunda ya utawala wake.Magazeti mengi binafsi yalianzishwa kipindi cha mzee Mwinyi.kama siyo uvumilivu wake kwa vyombo vya habari leo Kubenea asingethubutu kuandika anayoandika.

4.SERA YA UBINAFSISHAJI
Ubinafsishaji ulikuwa mgeni kwetu,lakini ulifanyika kwa hadhari kubwa.
Kumbuka Taasisi zote nyeti zimekuja uzwa baada ya yeye kumaliza muda wake.

5.UHURU WA KUTOA MAONI
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,watu walidiriki kumchambua rais hadharani.Ni jambo kubwa sana hilo alijenga culture ya uvumilivu kwa upande wa watawala.Kama kuna kiongozi aliyezungumzwa vibaya na vyombo vya habari wakati wa utawala wake basi ni huyu mzee.

5.UJENZI WA SEKTA BINAFSI
Ujasiriamali ulianzia hapa.


Yalifanyika haya ingawa mapungufu yalikuwepo , yeye ni binadamu lakini naye alifanya sehemu yake.Lakini ya EPA na mengine yafananayo na hayo hayakutokea kipindi chake.

Kwangu mimi amefanya sehemu yake.
 

Nakubalina na wewe.

Kuna mtu anajua Budget ya kusaidia Ukombozi kusini mwa Bara la Afrika ilikuwa Tshs ngapi at the same period of time??

You guys can not cnvinced me with your arguments,Mwalimu got eyes off the Ball.
 
Last edited:
Tunamlaumu Nyerere mioyoni mwetu lakini midomoni na katika maandishi yetu tunamuona shujaa.

KWa sababu akili zetu ziloshwa na nyimbo nyingi za kipuuzi tulizo imba kila asubuki machan na jioni.

Mchaka mchak chinja.
Akija Banda chinja tupa.
Akija Amini chinja tupa
Akija kaburu chinja tupa

Aliselema adija! aliselema.
Selema selema.

Alikwenda mpaka UNO
Na siasa akaimwaga
Alifanya makubwa sana kwa Watanzaniaaaa!

Nyerere ni komando lelelelele ni komando.
Nyerere ni komando lelle lelele ni kmandoo eeh!
ya kweli hayo?

Nyerere yupo Nyrerere yupo
Ukiona kundi la siasa Nyerere yupo
By definition it is true.

Menyekiti mwalimu Nyrerere mwenye hekima na wingi wa sifa Tanzania!

Unafiki mtu.
Ni kujikomba.
Ni ku Brainwash watu.
Even his best friend Kambona would have done it better
 

Attachments

Mwalimu Nyerere aling'atuka mwaka 1984 - hivi sasa ni miaka 25 au nusu karne toka aachie ngazi. Tukichukulia kuwa umri wa kuanza shule ni miaka 7, walioanza shule kipindi hicho hivi sasa wana umri wa wastani wa miaka 32 - ni wazazi ambao wanakaribia kupata wajukuu. Mtoto aliyezaliwa wakati huo kama amebahatika kusoma bila matatizo sasa anamaliza chuo kikuu - ni mtu mzima.

Nina wasiwasi kuwa wengi wa wachangiaji hapa wapo kwenye kundi hilo na kwa sababu hiyo wamesimuliwa tu kuhusu Mwalimu Nyerere na jitihada zake za kuiendeleza Tanzania. Wasimulizi wamegawanyika katika makundi mawili - wale wanaoelewa kuwa alifanya aliyofanya kwa nia njema na wale ambao katika kufanya aliyoyafanya aliwakwaza kimaslahi - kidini au kijamii na wana kisasi.

Ambaye alishindwa kusoma wakati huo ni kwamba alikuwa mtupu na hana uwezo maanake ilibidi ushinde mitihani na hiyo mitihani haikuwa ikisahihishwa na ndugu, wajomba ama washikaji. Kilichokufikisha chuo kikuu ni uwezo wako wa kumudu masomo na si fedha kama ilivyo sasa. Hata mpangilio wa kukaa madarasani kulizingatia uwezo wako - vipanga nyuma na vihiyo mbele karibu na mwalimu.

Je yawezekana kuwa hizi lawama anazotupiwa Mwalimu Nyerere ni mbinu za kufunika kombe mwanaharamu apite. Miaka 25 bado tunamlaumu kiongozi ambaye alithubutu kung'atuka alipong'amua kuwa kama binadamu mwenye mapungufu hawezi kuendelea kupambana na dunia ya kwanza. Hivi karibuni tumeshuhudia Mugabe naye akijaribu na watu Zimbabwe wameumia kwa kuwa vita havina macho !!
 

- Kukosa elimu wakati wa Mwalimu, ni lazima lilikuwa ni tatizo lako na kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake Mwalimu, mimi nimefundisha Ngumbaru as part ya kuwa darasa la sita in primary school, I mean what else Mwalimu angefanya na kukuza elimu?

- Mwalimu alikuwa na mapungufu mengine lakini la elimu mnamuonea, ninakumbuka safari ya mwisho ya Mwalimu UN, tumekutana naye pale nyumbani kwa Balozi, Mwinyi akiwa rais, Mwalimu akijibu swali la Dada Anna Muganda, kuhusu elimu, akisema kwa madaha sana kwamba katika machache aliyofanikiwa elimu ni namba moja, na kwamba toka atoke urais Tanzania imeshuka kabisaa kielimu as opposed na yeye alipokuwa rais, alisema Tanzania ilikuwa inashika namba one kwa Africa, akauliza sasa what happened baada ya yeye kutoka?

- Sikutegema siku moja kusikia haya, kwamba Mwalimu ni chanzo cha bongo kutokuwa na elimu? Hapana wakuu muogopeni Mungu japo kidogo, mimi nimesoma under Mwalimu, na sina lalamiko hata moja na Mwalimu, kuhusu elimu.

FMES!
 
Nakubaliana nawe ingawa data zinatofautiana maana itategemea mtu anayeandaa report anamarengo gani. Mfano Report ya Tanu ya mwa 1974 inaongelea kuwa mwaka 1975 8% ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza. za Unesco zinatuambia 3% during 1970. Nani aliwapatia hizo data ni selikari ya Nyerere, Mwinyi au Mkapa?Pamoja na hayo kwa kutumia data za Unesco, utakuta kuwa toka wakati wa Mwalimu, Mwinyi, mpaka Mkapa tumeendelea kucheza makida makida kwenye elimu ya sekondary maana kama Mwalimu aliacha 3%, Mwinyi na Mkapa waliongezea 4% tu kufikisha jumla ya 7% kwa mwaka 2000
 

Shukrani kwa data.

Nikiangalia kwa haraka haraka, sioni tofauti sana kati ya 1970-1985 na 1985-2005, sijui ulikuwa unataka kututhibitishia nini.....can you elaborate please.........ningekuwa na muda ningechora graphs ili kuonyesha hali halisi.........don't forget though hizo data zinatakiwa ziwe backed na malengo tuliyokuwa nayo kulingana na mazingira both political and economical.........then you will be able to measure kwamba je tulifanikiwa au lah.......na kama tulifanikiwa kwa kiasi gani na kama tulifeli kwa kiasi gani...............then compare na tulivyo sasa ambapo suala la elimu ni vurugu mechi tupu......
 

Wakuu FMES na Mag3
shukrani sana kwa maelezo yenu.......watu ambao hawaelewi nafikiri inabidi wasaidiwe.......waache mitizamo ya kibinafsi ,kidini na kibaguzi.........

TUMLAUMU MWL JKN kwa mengine sio ELIMU
 
Those who want to understand what went wrong with our education system try to read the book by John B. Knight and R.H. Sabot (world Bank Publication, 1990) titled "Education,productivity and inequality. This book can be viewed by typing the title of the book in google search engine and you will get the pages to preview which I think are enough to make you grasp what was going on in Tanzania and Kenya on education matters

Enjoy
 
Wakuu FMES na Mag3
shukrani sana kwa maelezo yenu.......watu ambao hawaelewi nafikiri inabidi wasaidiwe.......waache mitizamo ya kibinafsi ,kidini na kibaguzi.........

TUMLAUMU MWL JKN kwa mengine sio ELIMU

- Unless humu ndani kuna wanaosimuliwa kuhusu Mwalimu, mimi sihitaji dataz wala maelezo ya UN au anybody on Mwalimu na elimu, nimemuona mwenyewe na nimeona juhudi zake on elimu, nimeshiriki kwenye project mbali mbali za kuboresha elimu, under Mwalimu, hivi hizo dataz zimeandikwa na wazungu gani hao waliokuwa wakimpenda sana Mwalimu?

- Ifike mahali tumuache Mzee wa watu apumzike salama huko mbele ya haki, tumemsema vya kutosha sasa, kwa mazuri na mabaya, kwa wale msiomfahamu Mwalimu, labda mumtafute kwa mengine lakini la elimu, hapana maana tupo wengi tuliofaidika na kazi nzuri na nzito ya Mwalimu on elimu.

- Mwalimu alituletea mpaka waalimu "Wanyamwezi" yaani Wamarekani Weusi, hivi leo hata waalimu wa-China tu hakuna, muacheni mzee wa watu.

Respect.

FMES
 

Hata mimi ningejifagilia, ningeulizwa swali kama hilo.

Kushindwa kusoma ilikuwa ni tatizo la msomaji?

Sidhani?

Watu walikua wakipasua pepa lakini kwa vile shule zao ziko vijijini hakuna aliyekuwa akienda secondari miaka nenda rudi.

Tatizo la watu kama hao ni nini?

Uzuri ni kwamba hata kule kwao Butiama Lwamkoma na Kyabakari nako hakujenga shule, watu bado wanatiana ngeu hata kuuana kwa kugombea Wasimbe( Wasichana walo zaa na hawaishi na wanaume).

Butiama imepata shule ya kwanza ya sekondari wakati mmoja na sehemu yeyote ile ilokuwa nyuma Tanzania.

Kitu alichofanikiwa mwalimu Nyerere kuliko jambo lolote lile alolifanya maisha mwake ni kutumia uwezo (akili na nguvu za waTanzania)na ushawishi wake wote kuzikomboa Nchi za kusini mwa Afrika.

Elimu alijenga jitihada kisha akazitelekeza na kuingia kwenye mitunduru na AK47.
 
Mwalimu kafanya mengi sana na makubwa kuhusu Elimu ya Watanzania kuliko Mwinyi, Mkapa na Kikwete combined. Watanzania wengi ambao ni wasomi nchi za nje wakifanya vitu vyao ni matunda ya sera za Mwalimu katika Elimu na wengi hawaoni aibu kusema hivyo. Wengi wasingeweza kutia mguu shuleni kwa sababu wazazi wao wasingeweza kumudu gharama hizo au chuo kikuu na vyuo vyetu vingine.

Nyerere alijenga mashule na vyuo na kwa kutilia maanani kwamba Watanzania wengi walikuwa na vipato vidogo na hivyo kutoweza kumudu gharama za shule akaamua kuifanya elimu Tanzania kuwa bure kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu na vyuo vyetu vingine.

Hao uliokutana nao labda walikuwa wanakimbia umande au wazazi wao hawakutilia mkazo elimu, lakini hapa kutka kumlaumu Mwalimu ni kumsingizia tu. Mwalimu hakuwa perfect lakini vision yake ilikuwa ni kubwa sana na ingawa aling'atuka miaka 24 iliyopita lakini matunda ya sera yake hadi hii leo yanaifaidisha siyo tu Tanzania bali nchi nyingi za Ulimwengu. Hebu mwacheni Mzee wa watu alale kwa amani badala ya kutaka kumlaumu kwa yale ambayo hastahili kabisa kulaumiwa.
 

- Rumba lilikuwa kali, kupasi darasa la saba haikuwa mchezo mkuu, sio vijijini tu hata mijini, kama ni kujenga shule tu ndio dawa basi Mkoa wa Kilimanjaro si ndio ungekuwa namba moja kwa elimu Tanzania, Mwalimu alijitahidi ila sisi ndio tumejiua kabisaaa, mara yangu ya mwisho kwenda Mlimani ilikuwa ikiongozwa na Marehemu Chagula na Msekwa, hivi kweli unaweza linganisha Mlimani ile na ya sasa? what a joke!

Mpeni Mwalimu sifa zake on elimu, sasa hivi tungekuwa juu kielmu ningekubali.

FMES!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…