Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Mwl. Augustine Moshi,
Ninarudia swali lako la pili unapotaka kuona mwalimu kajenga shule 25 za secondary.. Mkuu wangu mimi nafanya biashara, mtaji wa kwanza ni mgumu sana kuzalisha unaweza kabisa chukua mwaka kabla kuhaona faida.. na siku biashara ikianza kunoga ndipo unapoweza kununua mali zaidi na kulijaza duka.. Hata siku moja huwezi kudandia mali iliyokwisha kuwa na msingi ukasema umezalisha zaidi na kusahau kazi nzito ya mtu aliyeweka msingi huo..
Kuchukulia takwimu za Andindile:-

By 1961, 490,000 students were attending primary education and most of them ending up in STD IV but by 1967, 825,000 children were attending such schools up to STD VII.
-In 1961, there were 11,832 children in secondary schools, only 176 of whom were in Form IV. By 1967 there were 25,000 and 880 were in form IV..
-in 1973 about 106,000 pupils completed primary education,whereby 18,5OO or 8% were selected for entry to secondary schools (TANU, 1974)..

Mkuu binafsi nishafanya uchunguzi na nadhani unakumbuka miaka ya nyuma tumewahi kuzungumzia hili.. Hadi wakati wa Mkapa asilimia ya wanafunzi waliojiunga na shule za sekondary ilikuwa 7 kama ile ya Nyerere hakuna tofauti zaidi ya hesabu ya wanafunzi kuonekana kubwa.
Nikiwa na maana kama Nyerere alipeleka wanafunzi 7 sekondary kwa kila 100, Mkapa alipeleka wanafunzi 70 kwa kila 1,000...Hapo hujajenga kitu mkuu wangu kama tutataka kuitazama elimu kwa kiwango kinachotakiwa...tunashindwa kutazama wali fail kwenda mbele kama kigezo cha uzembe wa mfumo wa elimu..Ndilo tatizo kubwa la takwimu zetu siku zote.

Mwaka 1973 wanafunzi waliomaliza darasa la saba walikuwa 106,000 na akasifiwa ktk kufuta ujinga leo hii tunazungumzia millioni 1 na upupu, mara kumi ya hesabu ya mwalimu sasa hapa unahitaji shule ngapi!.. mkuu wangu tulichobadilika ni ukubwa wa umbo tu hivyo unachoona sasa hivi ni ukubwa wa nguo.. wakati wa mwalimu tukiwa wachanga tulivaa nepi ktk elimu leo hii tunavaa suruali ukubwa wa nguo hiyo usikutishe ni feki - made in China..

Nyerere anaondoka ni 3 percent tu walikuwa wanakwedna sekondari. Vilevile Mzee Mwinyi ku-ruhusu private schools kuliongeza sana wanafunzi. Labda wewe ujarudi Tanzania ndio maana unafikiri kwenda form I bado ni sherehe ya kijiji ya kuchinja mbuzi.
 
3% kutoka vyanzo gani. Tupatie source nasi tujiridhishe
 
Mkandara,

I know, with complete certainty, that only 1,800 youngsters completed Form 6 in 1974. It so happens that I was one of them! I thank the Good Lord who arranged matters in such a way that I did my Forms 5 and 6 at Mkwawa. That way, I did get to do some actual studying, rather than hand hoe farming, for my A-levels.

I have lately realized that Mwalimu preferred to see pupils in the fields rather than in classrooms. No wonder he didn’t bother to supply schools with desks!

I see that you conveniently refuse to acknowledge the fact that Mwalimu under funded education. From independence up to 2007, Kenya spent 20 – 27 % of its budget on education, year in and year out. In the meantime, while trying to get us to “run while they walk”, Mwalimu proceeded to reduce our educational funding from 20% of the budget to a measly 4.9%!

Mwalimu used to say that “Tusipolima tutakufa!” I’ll paraphrase him and say that “Tusiposoma tutakufa!” Didn’t Mwalimu realize that education was the conditio sine qua non for development? Thanks to his neglect of it, we have become the economic backwater of East Africa! You want to toast him for the condition we find ourselves in. I refuse to join you!
 
Mkandara,

I see that you conveniently refuse to acknowledge the fact that Mwalimu under funded education. From independence up to 2007, Kenya spent 20 – 27 % of its budget on education, year in and year out. In the meantime, while trying to get us to “run while they walk”, Mwalimu proceeded to reduce our educational funding from 20% of the budget to a measly 4.9%!
Are you cooking the data or quoted somewhere. Please try to indicate the source of your data so that others can make reference otherwise we will not understand you!
 
Bwana Mkandara,
Umesema Waislam walilazimishwa kubadili dini; are you sure? Mie kuna ndugu zangu zaidi ya watatu ambao ni Waislam na wanamajina ya ki-islam walisoma vizuri sana na kumaliza shule hizo hizo.
Infact suala la elimu kwa nyerere on nationalization lilikuwa political (control); centralisation and governance. Kama alivyosema mwalimu hapo juu, kichwani kwa mwalimu pamoja na kuwa na charisma; vile vile ule ujamaa wa ki-China uimwingia mno. He just wanted everything in a central government for him to exercise control. Je kama angetoa amri kwa hizo Shule zisomeshe watoto wote waislam na wakristo nani angekataa? It was more political.

Hebu mwenzetu tuambie, kulikuwa na sababu gani, niliona baadhi ya mikoa shule za msingi hadi zile shati za kuvaa shule ziliondolewa "collar" wanafunzi wakawa wanavaa kama wachina. Eti shati inaitwa choen-lai.

Achilie mbali hayo yote, you 're right in one issue; wengi wetu tumshukuru huyu mzee kwa elimu hii, wazazi wengi hawakujua nini maana ya elimu.

Lakini tena uneni-acha hapa "matunda ya wanafunzi wa mfumo wa Mwalimu hadi Mwinyi". Hivi kuna zuri alilofanya Mwinyi? To me all what he did (Mwinyi) was detrimental to our unity, and good governance; the national was in total paralysis; economically, socially and politically!! All the time I pray not to have a president like that (like Mwinyi)!
Mambo aliyofanya Mzee Mwinyi:
1.UHURU WA KISIASA.
Kuruhusu mfumo wa vyama vingi.Hata kama kulikuwa na shinikizo, Regime nyingine zipo tayari kuingiza nchi kwenye vita,ili kulilinda tabaka tawala.

2.UHURU WA KIUCHUMI
Watanzania waliruhusiwa kujihusisha moja kwa moja na shughuli za kiuchumi.Mnakumbuka enzi zile hutakiwi kuwa na hisa kwenye kampuni ya kibepari.

2.UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Alijenga msingi imara wa vyombo binafsi vya habari.Uhuru wa vyombo vya habari mnaoinjoi leo ni matunda ya utawala wake.Magazeti mengi binafsi yalianzishwa kipindi cha mzee Mwinyi.kama siyo uvumilivu wake kwa vyombo vya habari leo Kubenea asingethubutu kuandika anayoandika.

4.SERA YA UBINAFSISHAJI
Ubinafsishaji ulikuwa mgeni kwetu,lakini ulifanyika kwa hadhari kubwa.
Kumbuka Taasisi zote nyeti zimekuja uzwa baada ya yeye kumaliza muda wake.

5.UHURU WA KUTOA MAONI
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,watu walidiriki kumchambua rais hadharani.Ni jambo kubwa sana hilo alijenga culture ya uvumilivu kwa upande wa watawala.Kama kuna kiongozi aliyezungumzwa vibaya na vyombo vya habari wakati wa utawala wake basi ni huyu mzee.

5.UJENZI WA SEKTA BINAFSI
Ujasiriamali ulianzia hapa.

Yalifanyika haya ingawa mapungufu yalikuwepo , yeye ni binadamu lakini naye alifanya sehemu yake.Lakini ya EPA na mengine yafananayo na hayo hayakutokea kipindi chake.

Kwangu mimi amefanya sehemu yake.
 
Ogah na Mkandara,

Si sahihi kusema Mwalimu hakudumaza elimu ya juu eti kwa vile haikuwa na vurugu. Kitu kikiwa kidogo sana hakiwezi kuwa na vurugu.

Nimechukua mfano wa 1974 as a base line. Thirteen years after independence Tanzania was producing only 1,800 form six leavers per year. Mwalimu aliona hao ni wengi. Mwaka uliofuatia, 1975, akatangaza Azimio la Musoma ili kuwazuia wasiende chuo kikuu moja kwa moja.

Kama unatawala nchi changa, na idadi ya wanafunzi vyuo vikuu haiongezeki kiasi cha kuridhisha basi wewe unadumaza elimu ya juu. That applies squarely to Mwalimu.

Mimi nilikuwa mwaka wa pili UDSM wakati Mwalimu alipotangazia taifa kwamba wanafunzi wa chuo kikuu wamegoma kwenda vijijini. That was a shocking lie! As an idealistic youth niligundua, kwa mara ya kwanza, kwamba Mwalimu anasema uongo! With maturity, niligundua kwamba hata aliposema hakuna sabuni, hakuna dawa kwa sababu ya maendeleo ilikuwa ni uongo, na alijua anasema uongo.

Mwalimu paid lip service to education. He did not put his money where his mouth was. At independence Tangangika was spending 20% of its budget on education. Mwalimu proceeded to cut this down to a mere 4.9% at his departure. Kama angeendelea sijui ingekuwaje.

Nakubalina na wewe.

Kuna mtu anajua Budget ya kusaidia Ukombozi kusini mwa Bara la Afrika ilikuwa Tshs ngapi at the same period of time??

You guys can not cnvinced me with your arguments,Mwalimu got eyes off the Ball.
 
Last edited:
Tunamlaumu Nyerere mioyoni mwetu lakini midomoni na katika maandishi yetu tunamuona shujaa.

KWa sababu akili zetu ziloshwa na nyimbo nyingi za kipuuzi tulizo imba kila asubuki machan na jioni.

Mchaka mchak chinja.
Akija Banda chinja tupa.
Akija Amini chinja tupa
Akija kaburu chinja tupa

Aliselema adija! aliselema.
Selema selema.

Alikwenda mpaka UNO
Na siasa akaimwaga
Alifanya makubwa sana kwa Watanzaniaaaa!

Nyerere ni komando lelelelele ni komando.
Nyerere ni komando lelle lelele ni kmandoo eeh!
ya kweli hayo?

Nyerere yupo Nyrerere yupo
Ukiona kundi la siasa Nyerere yupo
By definition it is true.

Menyekiti mwalimu Nyrerere mwenye hekima na wingi wa sifa Tanzania!

Unafiki mtu.
Ni kujikomba.
Ni ku Brainwash watu.
Even his best friend Kambona would have done it better
 
Attachments

Mwalimu Nyerere aling'atuka mwaka 1984 - hivi sasa ni miaka 25 au nusu karne toka aachie ngazi. Tukichukulia kuwa umri wa kuanza shule ni miaka 7, walioanza shule kipindi hicho hivi sasa wana umri wa wastani wa miaka 32 - ni wazazi ambao wanakaribia kupata wajukuu. Mtoto aliyezaliwa wakati huo kama amebahatika kusoma bila matatizo sasa anamaliza chuo kikuu - ni mtu mzima.

Nina wasiwasi kuwa wengi wa wachangiaji hapa wapo kwenye kundi hilo na kwa sababu hiyo wamesimuliwa tu kuhusu Mwalimu Nyerere na jitihada zake za kuiendeleza Tanzania. Wasimulizi wamegawanyika katika makundi mawili - wale wanaoelewa kuwa alifanya aliyofanya kwa nia njema na wale ambao katika kufanya aliyoyafanya aliwakwaza kimaslahi - kidini au kijamii na wana kisasi.

Ambaye alishindwa kusoma wakati huo ni kwamba alikuwa mtupu na hana uwezo maanake ilibidi ushinde mitihani na hiyo mitihani haikuwa ikisahihishwa na ndugu, wajomba ama washikaji. Kilichokufikisha chuo kikuu ni uwezo wako wa kumudu masomo na si fedha kama ilivyo sasa. Hata mpangilio wa kukaa madarasani kulizingatia uwezo wako - vipanga nyuma na vihiyo mbele karibu na mwalimu.

Je yawezekana kuwa hizi lawama anazotupiwa Mwalimu Nyerere ni mbinu za kufunika kombe mwanaharamu apite. Miaka 25 bado tunamlaumu kiongozi ambaye alithubutu kung'atuka alipong'amua kuwa kama binadamu mwenye mapungufu hawezi kuendelea kupambana na dunia ya kwanza. Hivi karibuni tumeshuhudia Mugabe naye akijaribu na watu Zimbabwe wameumia kwa kuwa vita havina macho !!
 
- Kukosa elimu wakati wa Mwalimu, ni lazima lilikuwa ni tatizo lako na kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake Mwalimu, mimi nimefundisha Ngumbaru as part ya kuwa darasa la sita in primary school, I mean what else Mwalimu angefanya na kukuza elimu?

- Mwalimu alikuwa na mapungufu mengine lakini la elimu mnamuonea, ninakumbuka safari ya mwisho ya Mwalimu UN, tumekutana naye pale nyumbani kwa Balozi, Mwinyi akiwa rais, Mwalimu akijibu swali la Dada Anna Muganda, kuhusu elimu, akisema kwa madaha sana kwamba katika machache aliyofanikiwa elimu ni namba moja, na kwamba toka atoke urais Tanzania imeshuka kabisaa kielimu as opposed na yeye alipokuwa rais, alisema Tanzania ilikuwa inashika namba one kwa Africa, akauliza sasa what happened baada ya yeye kutoka?

- Sikutegema siku moja kusikia haya, kwamba Mwalimu ni chanzo cha bongo kutokuwa na elimu? Hapana wakuu muogopeni Mungu japo kidogo, mimi nimesoma under Mwalimu, na sina lalamiko hata moja na Mwalimu, kuhusu elimu.

FMES!
 
Nenda kwenye hii link ya Unesco. Baadaye scroll chini na kuna information kuhusu primary na secondary school historical enrollment. Kuna data za kuthibitisha yale Moshi anayosema na vilevile ya 3%.

Global Education Digest: UNESCO Institute for Statistics (3.14)

Na kwa wale wavivu nimeweka attachment.
Nakubaliana nawe ingawa data zinatofautiana maana itategemea mtu anayeandaa report anamarengo gani. Mfano Report ya Tanu ya mwa 1974 inaongelea kuwa mwaka 1975 8% ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza. za Unesco zinatuambia 3% during 1970. Nani aliwapatia hizo data ni selikari ya Nyerere, Mwinyi au Mkapa?Pamoja na hayo kwa kutumia data za Unesco, utakuta kuwa toka wakati wa Mwalimu, Mwinyi, mpaka Mkapa tumeendelea kucheza makida makida kwenye elimu ya sekondary maana kama Mwalimu aliacha 3%, Mwinyi na Mkapa waliongezea 4% tu kufikisha jumla ya 7% kwa mwaka 2000
 
Nenda kwenye hii link ya Unesco. Baadaye scroll chini na kuna information kuhusu primary na secondary school historical enrollment. Kuna data za kuthibitisha yale Moshi anayosema na vilevile ya 3%.

Global Education Digest: UNESCO Institute for Statistics (3.14)

Na kwa wale wavivu nimeweka attachment.

Shukrani kwa data.

Nikiangalia kwa haraka haraka, sioni tofauti sana kati ya 1970-1985 na 1985-2005, sijui ulikuwa unataka kututhibitishia nini.....can you elaborate please.........ningekuwa na muda ningechora graphs ili kuonyesha hali halisi.........don't forget though hizo data zinatakiwa ziwe backed na malengo tuliyokuwa nayo kulingana na mazingira both political and economical.........then you will be able to measure kwamba je tulifanikiwa au lah.......na kama tulifanikiwa kwa kiasi gani na kama tulifeli kwa kiasi gani...............then compare na tulivyo sasa ambapo suala la elimu ni vurugu mechi tupu......
 
Mwalimu Nyerere aling'atuka mwaka 1984 - hivi sasa ni miaka 25 au nusu karne toka aachie ngazi. Tukichukulia kuwa umri wa kuanza shule ni miaka 7, walioanza shule kipindi hicho hivi sasa wana umri wa wastani wa miaka 32 - ni wazazi ambao wanakaribia kupata wajukuu. Mtoto aliyezaliwa wakati huo kama amebahatika kusoma bila matatizo sasa anamaliza chuo kikuu - ni mtu mzima.

Nina wasiwasi kuwa wengi wa wachangiaji hapa wapo kwenye kundi hilo na kwa sababu hiyo wamesimuliwa tu kuhusu Mwalimu Nyerere na jitihada zake za kuiendeleza Tanzania. Wasimulizi wamegawanyika katika makundi mawili - wale wanaoelewa kuwa alifanya aliyofanya kwa nia njema na wale ambao katika kufanya aliyoyafanya aliwakwaza kimaslahi - kidini au kijamii na wana kisasi.

Ambaye alishindwa kusoma wakati huo ni kwamba alikuwa mtupu na hana uwezo maanake ilibidi ushinde mitihani na hiyo mitihani haikuwa ikisahihishwa na ndugu, wajomba ama washikaji. Kilichokufikisha chuo kikuu ni uwezo wako wa kumudu masomo na si fedha kama ilivyo sasa. Hata mpangilio wa kukaa madarasani kulizingatia uwezo wako - vipanga nyuma na vihiyo mbele karibu na mwalimu.

Je yawezekana kuwa hizi lawama anazotupiwa Mwalimu Nyerere ni mbinu za kufunika kombe mwanaharamu apite. Miaka 25 bado tunamlaumu kiongozi ambaye alithubutu kung'atuka alipong'amua kuwa kama binadamu mwenye mapungufu hawezi kuendelea kupambana na dunia ya kwanza. Hivi karibuni tumeshuhudia Mugabe naye akijaribu na watu Zimbabwe wameumia kwa kuwa vita havina macho !!

Wakuu FMES na Mag3
shukrani sana kwa maelezo yenu.......watu ambao hawaelewi nafikiri inabidi wasaidiwe.......waache mitizamo ya kibinafsi ,kidini na kibaguzi.........

TUMLAUMU MWL JKN kwa mengine sio ELIMU
 
Those who want to understand what went wrong with our education system try to read the book by John B. Knight and R.H. Sabot (world Bank Publication, 1990) titled "Education,productivity and inequality. This book can be viewed by typing the title of the book in google search engine and you will get the pages to preview which I think are enough to make you grasp what was going on in Tanzania and Kenya on education matters

Enjoy
 
Wakuu FMES na Mag3
shukrani sana kwa maelezo yenu.......watu ambao hawaelewi nafikiri inabidi wasaidiwe.......waache mitizamo ya kibinafsi ,kidini na kibaguzi.........

TUMLAUMU MWL JKN kwa mengine sio ELIMU

- Unless humu ndani kuna wanaosimuliwa kuhusu Mwalimu, mimi sihitaji dataz wala maelezo ya UN au anybody on Mwalimu na elimu, nimemuona mwenyewe na nimeona juhudi zake on elimu, nimeshiriki kwenye project mbali mbali za kuboresha elimu, under Mwalimu, hivi hizo dataz zimeandikwa na wazungu gani hao waliokuwa wakimpenda sana Mwalimu?

- Ifike mahali tumuache Mzee wa watu apumzike salama huko mbele ya haki, tumemsema vya kutosha sasa, kwa mazuri na mabaya, kwa wale msiomfahamu Mwalimu, labda mumtafute kwa mengine lakini la elimu, hapana maana tupo wengi tuliofaidika na kazi nzuri na nzito ya Mwalimu on elimu.

- Mwalimu alituletea mpaka waalimu "Wanyamwezi" yaani Wamarekani Weusi, hivi leo hata waalimu wa-China tu hakuna, muacheni mzee wa watu.

Respect.

FMES
 
- Kukosa elimu wakati wa Mwalimu, ni lazima lilikuwa ni tatizo lako na kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake Mwalimu, mimi nimefundisha Ngumbaru as part ya kuwa darasa la sita in primary school, I mean what else Mwalimu angefanya na kukuza elimu?

- Mwalimu alikuwa na mapungufu mengine lakini la elimu mnamuonea, ninakumbuka safari ya mwisho ya Mwalimu UN, tumekutana naye pale nyumbani kwa Balozi, Mwinyi akiwa rais, Mwalimu akijibu swali la Dada Anna Muganda, kuhusu elimu, akisema kwa madaha sana kwamba katika machache aliyofanikiwa elimu ni namba moja, na kwamba toka atoke urais Tanzania imeshuka kabisaa kielimu as opposed na yeye alipokuwa rais, alisema Tanzania ilikuwa inashika namba one kwa Africa, akauliza sasa what happened baada ya yeye kutoka?

- Sikutegema siku moja kusikia haya, kwamba Mwalimu ni chanzo cha bongo kutokuwa na elimu? Hapana wakuu muogopeni Mungu japo kidogo, mimi nimesoma under Mwalimu, na sina lalamiko hata moja na Mwalimu, kuhusu elimu.

FMES!

Hata mimi ningejifagilia, ningeulizwa swali kama hilo.

Kushindwa kusoma ilikuwa ni tatizo la msomaji?

Sidhani?

Watu walikua wakipasua pepa lakini kwa vile shule zao ziko vijijini hakuna aliyekuwa akienda secondari miaka nenda rudi.

Tatizo la watu kama hao ni nini?

Uzuri ni kwamba hata kule kwao Butiama Lwamkoma na Kyabakari nako hakujenga shule, watu bado wanatiana ngeu hata kuuana kwa kugombea Wasimbe( Wasichana walo zaa na hawaishi na wanaume).

Butiama imepata shule ya kwanza ya sekondari wakati mmoja na sehemu yeyote ile ilokuwa nyuma Tanzania.

Kitu alichofanikiwa mwalimu Nyerere kuliko jambo lolote lile alolifanya maisha mwake ni kutumia uwezo (akili na nguvu za waTanzania)na ushawishi wake wote kuzikomboa Nchi za kusini mwa Afrika.

Elimu alijenga jitihada kisha akazitelekeza na kuingia kwenye mitunduru na AK47.
 
Mwalimu kafanya mengi sana na makubwa kuhusu Elimu ya Watanzania kuliko Mwinyi, Mkapa na Kikwete combined. Watanzania wengi ambao ni wasomi nchi za nje wakifanya vitu vyao ni matunda ya sera za Mwalimu katika Elimu na wengi hawaoni aibu kusema hivyo. Wengi wasingeweza kutia mguu shuleni kwa sababu wazazi wao wasingeweza kumudu gharama hizo au chuo kikuu na vyuo vyetu vingine.

Nyerere alijenga mashule na vyuo na kwa kutilia maanani kwamba Watanzania wengi walikuwa na vipato vidogo na hivyo kutoweza kumudu gharama za shule akaamua kuifanya elimu Tanzania kuwa bure kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu na vyuo vyetu vingine.

Hao uliokutana nao labda walikuwa wanakimbia umande au wazazi wao hawakutilia mkazo elimu, lakini hapa kutka kumlaumu Mwalimu ni kumsingizia tu. Mwalimu hakuwa perfect lakini vision yake ilikuwa ni kubwa sana na ingawa aling'atuka miaka 24 iliyopita lakini matunda ya sera yake hadi hii leo yanaifaidisha siyo tu Tanzania bali nchi nyingi za Ulimwengu. Hebu mwacheni Mzee wa watu alale kwa amani badala ya kutaka kumlaumu kwa yale ambayo hastahili kabisa kulaumiwa.
 
Hata mimi ningejifagilia, ningeulizwa swali kama hilo.

Kushindwa kusoma ilikuwa ni tatizo la msomaji?

Sidhani?

Watu walikua wakipasua pepa lakini kwa vile shule zao ziko vijijini hakuna laiyekuwa akienda secondari mika nenda rudi.

Uzuri ni kwamba hata kule kwao Butiama Lwamkoma na Kyabakari nako hakujenga shule, watu bado wanatiana ngeu hata kuuana kwa kugombea Wasimbe.
Butiama imepata shule ya sekondari wakati mmoja na sehemu yeyote ilokuwa nyuma Tanzania.

Kitu alichofanikiwa mwalimu Nyerere kuliko jambo lolote lile alolifanya maisha mwake ni kutumia uwezo (akili na nguvu za watanzania)na ushawishi wake wote kuzikomboa Nchi za kusini mwa Afrika.

Elimu alijenga jitihada kisha akazitelekeza na kuingia kwenye mitunduru na AK47.

- Rumba lilikuwa kali, kupasi darasa la saba haikuwa mchezo mkuu, sio vijijini tu hata mijini, kama ni kujenga shule tu ndio dawa basi Mkoa wa Kilimanjaro si ndio ungekuwa namba moja kwa elimu Tanzania, Mwalimu alijitahidi ila sisi ndio tumejiua kabisaaa, mara yangu ya mwisho kwenda Mlimani ilikuwa ikiongozwa na Marehemu Chagula na Msekwa, hivi kweli unaweza linganisha Mlimani ile na ya sasa? what a joke!

Mpeni Mwalimu sifa zake on elimu, sasa hivi tungekuwa juu kielmu ningekubali.

FMES!
 
Back
Top Bottom