Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Mwl. Augustine Moshi,
Ninarudia swali lako la pili unapotaka kuona mwalimu kajenga shule 25 za secondary.. Mkuu wangu mimi nafanya biashara, mtaji wa kwanza ni mgumu sana kuzalisha unaweza kabisa chukua mwaka kabla kuhaona faida.. na siku biashara ikianza kunoga ndipo unapoweza kununua mali zaidi na kulijaza duka.. Hata siku moja huwezi kudandia mali iliyokwisha kuwa na msingi ukasema umezalisha zaidi na kusahau kazi nzito ya mtu aliyeweka msingi huo..
Kuchukulia takwimu za Andindile:-
By 1961, 490,000 students were attending primary education and most of them ending up in STD IV but by 1967, 825,000 children were attending such schools up to STD VII.
-In 1961, there were 11,832 children in secondary schools, only 176 of whom were in Form IV. By 1967 there were 25,000 and 880 were in form IV..
-in 1973 about 106,000 pupils completed primary education,whereby 18,5OO or 8% were selected for entry to secondary schools (TANU, 1974)..
Mkuu binafsi nishafanya uchunguzi na nadhani unakumbuka miaka ya nyuma tumewahi kuzungumzia hili.. Hadi wakati wa Mkapa asilimia ya wanafunzi waliojiunga na shule za sekondary ilikuwa 7 kama ile ya Nyerere hakuna tofauti zaidi ya hesabu ya wanafunzi kuonekana kubwa.
Nikiwa na maana kama Nyerere alipeleka wanafunzi 7 sekondary kwa kila 100, Mkapa alipeleka wanafunzi 70 kwa kila 1,000...Hapo hujajenga kitu mkuu wangu kama tutataka kuitazama elimu kwa kiwango kinachotakiwa...tunashindwa kutazama wali fail kwenda mbele kama kigezo cha uzembe wa mfumo wa elimu..Ndilo tatizo kubwa la takwimu zetu siku zote.
Mwaka 1973 wanafunzi waliomaliza darasa la saba walikuwa 106,000 na akasifiwa ktk kufuta ujinga leo hii tunazungumzia millioni 1 na upupu, mara kumi ya hesabu ya mwalimu sasa hapa unahitaji shule ngapi!.. mkuu wangu tulichobadilika ni ukubwa wa umbo tu hivyo unachoona sasa hivi ni ukubwa wa nguo.. wakati wa mwalimu tukiwa wachanga tulivaa nepi ktk elimu leo hii tunavaa suruali ukubwa wa nguo hiyo usikutishe ni feki - made in China..
Nyerere anaondoka ni 3 percent tu walikuwa wanakwedna sekondari. Vilevile Mzee Mwinyi ku-ruhusu private schools kuliongeza sana wanafunzi. Labda wewe ujarudi Tanzania ndio maana unafikiri kwenda form I bado ni sherehe ya kijiji ya kuchinja mbuzi.