sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Hebu chukulia mfano yanayoendelea Ukraine, mtu unamkuta anaenda kutafuta hifadhi pamoja na mnyama wake, leo hii sitashangaa hapa kwetu mtu akihamia hata mtaa wa nne basi atamtelekeza mbwa wake.
kuwatesa wanyama ni kumtemea mate usoni Mwenyezi Mungu alieumba viumbe vyote,
kuna hizi tabia mbaya sana zimezoeleka na watanzania wengi kwa wanyama 👇👇
-unakuta tu mtaani mbwa anajipitia zake, mtu anaanza kumrushia mawe.
-nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!! aende wapi sasa wakati hapo ni kwao ?
-Mtu kavimbiwa nyama, zile zilizobaki ambazo hata hajazila anaenda kutupa badala ya kumpa hata mbwa au paka wanaeishi nae
-kuku yupo bize anatafuta chakula, mara mtu anaanza kumkimbiza tu bila sababu.
-Mbuzi ameletwa kwajili ya nyama ya sherehe, usiku umefika anaachwa ukutani, yani mtu hata hajali kama kuna baridi, mvua, mbuzi angalau apumzike vizuri siku yake ya mwisho, n.k.
-usiombe kukutana na mtu anatumia ng'ombe kulima, yani hizo stiki huyo ng'ombe anazokula na matusi juu ni balaa.
-Dume limempanda jike, mtu anaanza kuwarusha mawe.
-mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga.
-Punda anabebeshwa mizigo mizito yani hata kutembea inakuwa shida lakini mtu wala hajali.
-Mbwa kila usiku anakulinda wewe, familia yako na mali ila kibanda chake hakijasafishwa mwaka mzima kimejaa viroboto, chakula chake ni makombo kila siku, yani mtu hajiongezi hata kumpa nyama mara moja kama shukrani ya ulinzi anaompa.
Hivi hawa wanyama wanakosa lipi?