Ni tabia mbaya sana, Wanyama ni viumbe ambao kutowaheshimu huleta laana maana ni vimbe walioumbwa na Mwenyezi Mungu, viumbe hivi kuvifanyia ubaya ni kumdhihaki Mwenyezi Mungu.
unakuta tu mtaani mbwa anapita mtu anaanza kumrushia mawe.
nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!!
kuku anatafuta chakula kwenye jua kali, mara mtu anaanza kumfukuza tu bila sababu.
mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga
Mbwa anakulindia maisha yako, nyumba na mali zako ila mwaka mzima unashindwa kujiongeza hata kumpa msosi wa maana kidogo kama shukrani, huu ni uungwana kweli?
wanyama wanakosa lipi?