Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Ni tabia mbaya sana, Wanyama ni viumbe ambao kutowaheshimu huleta laana maana ni vimbe walioumbwa na Mwenyezi Mungu, viumbe hivi kuvifanyia ubaya ni kumdhihaki Mwenyezi Mungu.

unakuta tu mtaani mbwa anapita mtu anaanza kumrushia mawe.

nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!!

kuku anatafuta chakula kwenye jua kali, mara mtu anaanza kumfukuza tu bila sababu.

mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga

Mbwa anakulindia maisha yako, nyumba na mali zako ila mwaka mzima unashindwa kujiongeza hata kumpa msosi wa maana kidogo kama shukrani, huu ni uungwana kweli?


wanyama wanakosa lipi?
Ni ujinga tu....hapa mtaani kwetu kuna watoto walikuwa wanatoka shule siku moja nikawaluta wanasalandia mbwa wangu aliyekuwa kwenye kibanda chake tena ndani ya geti wameshika mawe wamtungue. Nikawavizia na nikabahatiak kumkamata mmoja. Nikamuingiza ndani na kumfungulia mbwa amrarue na alimng'ata vizuri tu. Akaenda kwao kisha akarudi na wazazi wake kuja kulalamika na kunishitaki. Nikawaambia ukweli kilichotokea, baba wa mtoto kwa ujinga alionao alkasema eti huu ni mtaa wa Kiislam unafuga mbwa wa nini? Nikamjibu tu vibaka wengi wa hapa mtaani ni waislam Mze baba akanishangaa, wakaenda nishitaki Polisi Mabatini ila kesi haikufika mbali, ilifutwa. Yule dogo ni mwaka sasa hajathubutu kuja kurusha mawe tena, yuko tu makovu yake ya kujitakia.
 
Roho ya Huruma,na roho ya ukatili hujidhihirisha vile tunavyoishi na hawa wanyama kwa hyo na rahisi kumtambua mtu ni wa aina gani vile anavyo mtreat mnyama
Utotoni kulikuwa na michezo ya watoto kwenda kuwinda mijusi then kuwachezea na kuwaua.

Mzee alinifundisha si vizuri kuua kiumbe bila sababu. Walikuwa wananiita mlokole. sababu nilikuwa nikiwakataza nikisema sio vizuri.😂
 
Kwahiyo ata nyoka tusimuue?..panya je? ....sema hii tabia mbaya kweli, kuna siku nilimbutua mbwa mpaka leo namuonea huruma
 
Ukitaka kujua wabongo wengi ni sadists angalia wanavyoshangilia raia wa Ukraine kuuwawa wakati karibu dunia yote inasikitishwa na mauaji yanayoendelea huko.
 
🐒🤣👇

 
Back
Top Bottom