Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Tatizo baadhi ya wanyama wakishakuwa kwa binadamu huwa wanajiona kama binadamu kweli, huwa wanawaletea dharau wanyama wenzao hata binadamu ambao mifukoni ni apeche alolo.
Sasa binadamu akishaona mnyama analia mbele yake, yeye anajistukia, anahisi mnyama anamn'gong'a kwa sababu hana hela. kinachofuata ni teke kubwa sana au jiwe.
 
viumbe hivi tumepewa mamlaka ya kuvitawala kihalali na si kuvinyanhasa ama kuvitesa, viumbe hivi kuvifanyia ubaya ni sawa na kumtemea mate usoni Mwenyezi Mungu.

unakuta tu mtaani mbwa anapita mtu anaanza kumrushia mawe.

nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!!

kuku anatafuta chakula kwenye jua kali, mara mtu anaanza kumfukuza tu bila sababu.

mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga

usiombe kukutana na mtu anatumia ng'ombe kulima, yani hizo stiki huyo ng'ombe anazokula na matusi juu ni balaa.

Punda anabebeshwa mizigo mizito yani hata kuibeba unaona amavyoteseka na amechoka lakini mtu wala hajali.


Mbwa anakulindia maisha yako, nyumba na mali zako ila mwaka mzima unashindwa kujiongeza hata kumpa msosi wa maana kidogo kama shukrani, huu ni uungwana kweli?


wanyama wanakosa lipi?
Kweli mkuu, kuna watu wana moyo wa ajabu sana. Na hii tabia iko zaidi huku nchi masikini. Nadhani umasikini umeathiri hadi kwenye moyo, mtu anajikuta ana "ukatili" tu usioeleweka.


JESUS IS SAVIOR
 
Hahahaaa hapa nimekutana na watu wanapiga mawe kambwa
 
Kuishi bila mnyama mbwa,paka,ndege

Naona kama nmepungukiwa kitu fulani...

Ova
 
WENGI WAMELELEWA KWENYE UJINGA UJINGA TU NDIO MAANA HAWANA MAPENZI NA WANYAMA
 
Niliua paka mwenyewe tena kwa kutumia kwanja ndani tulikimbizana nikakata mguu alijikunyata mahala nilipita kwanja kadhaa za kichwa mpk akafa nikazika.

Wanyama ni wazuri ila wakila mifugo yetu kama kuku mengine ni hatari sana.
MOYO WAKO UMEJAA GIZA TUPU.

HATA SHETANI ANAKUOGOPA
 
Unasemaje roho za kishetani na kutomtambua Mungu!?

Hujaenda nyumba ya mlokole anayemiliki maji ya Bulldozer, Hadi mende, mjusi huwa anamwagiwa maji, na kupigiwa kelele shindwaaaaah!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah hii inachekesha zaid
 
Mi napenda wanyama haswa paka nawapenda sana
Kuna siku niliona video mtu kaweka stastus inaonyesha jamaa kamkaba paka shingon anamkandamiza huku akipiga pushup jamani niliumia sana yule paka alikuwa analia jamani nahisi alimuua
 
kila mtu kuna mnayama anampenda huwa napenda sana mbwa sababu yuko mtiifu, mstaarabu ukirud anakushangilia ni kiumbe wa tofauti

I’ll be honest sipend paka, yale manyoya yake ndio changamoto kwangu kabisa, ukilala unashangaa na yeye kalala upande mwingine wa kitanda sipend hiyo tabia
 
Hii haina tofauti na wale watanzania pale kivukoni wakishashuka kwenye ferry wanaanza kukimbia, bc ujue matatizo na shida ndiyo yanawafanya watu waheuke wafanye mambo kama hayo.

Hivi nin kinawafanya wakimbie Yaan kuna mambo yanatia aibu
 
Hii haina tofauti na wale watanzania pale kivukoni wakishashuka kwenye ferry wanaanza kukimbia, bc ujue matatizo na shida ndiyo yanawafanya watu waheuke wafanye mambo kama hayo.

Wale wanakimbilia magari usafiri shida sio wanapenda kukimbia vile
 
Usiombe Wakutane na Mdada hawa,Utawaonea huruma!

images.jpg


download.jpg


images-1.jpg
 
Back
Top Bottom