Hhah napenda paka alikuwa akiona hujatandika kitanda haji kulala ukitandika tu anakuja lala weeeeee akiamka anaenda sehemu yake ya kukojoa anakojoa hajawah kukojoa kitandani au kujisaidia popote ndani kisha huyo anakufata umfatie nyama,kuna siku nikamkuta chooni anakojoa [emoji23][emoji23][emoji23] nilicheka mno
Ikifika usiku wakati wa kulala nae anaenda kupanda kitandani kulala kile kile kitanda habadilishi,anajiingiza kwenye blanket basi hicho kitanda ni aunt yangu,muda mwingine aunt kapitiwa usingizi paka anaenda penyeza kwenye blanket analala akamtengenezea sehemu yake ya kulala akawa anamuekea alale lakin sasa mkiaka asubuhi anapanda kitandani analala ndani ya blanket nikija kutoa blanket anakuwa mkali tunaanza kuvutiana blanket nilikuwa nacheka jamani,mkifunga mlango kama hajaingia ndani wee atapiga piga huo mlango na kulia mpaka mtamfungulia aje alale ndani eti kulala nje hawezi