viumbe hivi tumepewa mamlaka ya kuvitawala kihalali na si kuvinyanyasa ama kuvitesa, viumbe hivi kuvifanyia ubaya ni sawa na kumtemea mate usoni alietuumba.
unakuta tu mtaani mbwa anapita mtu anaanza kumrushia mawe.
nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!!
kuku anatafuta chakula kwenye jua kali, mara mtu anaanza kumkimbiza tu bila sababu.
mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga
usiombe kukutana na mtu anatumia ng'ombe kulima, yani hizo stiki huyo ng'ombe anazokula na matusi juu ni balaa.
Punda anabebeshwa mizigo mizito yani hata kuibeba unaona wazi jinsi anavyoteseka lakini mtu wala hajali.
Mbwa anakulindia maisha yako, nyumba na mali zako ila haogeshwi amejaa kupe, kibanda chake hakijasafishwa mda mrefu viroboto kibao, kumlisha ni ugali na dagaa kila siku yani hata kusema umpe nyama mara moja moja kama shukrani ya ulinzi wake hamna.
Hivi hawa wanyama wanakosa lipi?