#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

Yaani watu na akili zao chanjo wanayo na bado wanakufa!
Nyie ndo mnajifanya mnajua kuliko hao?
 
Chomeni tuanze kuwaz.....
India wenyewe wamesanda nyie ndo mnajua sana kuliko wao?
 
Wajinga wanataka kujaza watu ujinga... hawajiulizi ni "wakubwa" wangapi walidondoka mmoja baada ya mwingine... hawajiulizi yuko mkubwa mmoja alipinga sana barakoa lakini ghafla tukamuona ameivaa!!! Akili mkichwa...
Alipinga barakoa na sasa anavaa?
 
Wazee ambao ndio wanapewa kipaumbele hawataki hata kusikia habari ya chanjo, ushauri wangu pengine viongozi wetu ngazi za juu wangeanza kuchanjwa kwanza wao ili kuleta hamasa na kuwadhibitishia wananchi kuwa haina madhara.
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Mapendekezo yangu

1) Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa

2) Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea

3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo

4) Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
Wengi tunakataa sababu hakuna chanjo ambayo wanachanjwa watu bila kufanyiwa majaribio ya muda mrefu na kujua athari zake pia,hii ni biashara ya wahuni ambao wanataka watufanye mazombie, hao hao ndio walitangaza mwaka jana kwamba bara la Afrika litatapakaa maiti barabarani, matokeo yake sote tunajua hakuna maiti hao waliosema ndio haohao wametengana kwa ajili ya ujinga wao na hadi walifikia kutaka kuhonga au kujipendekeza kwa watoa tuzo ya Nobel ili wapewe tuzo hiyo maarufu duniani, ndio maana tunasita kuwaamini na hizo chanjo zao ambazo wao ndio watoa fedha.
 
Wazee ambao ndio wanapewa kipaumbele hawataki hata kusikia habari ya chanjo, ushauri wangu pengine viongozi wetu ngazi za juu wangeanza kuchanjwa kwanza wao ili kuleta hamasa na kuwadhibitishia wananchi kuwa haina madhara.
Watachanjwa ya vitamini halafu utaambiwa ni ya corona, wanasiasa hawaaminiki mkuu.
 
... siku hizi Mataga wanatambulika kama watanzania "wengi"? Be serious ndugu; labda hayajawahi kukukuta; nenda hospitalini uone wagonjwa wa Covid wanavyoteseka utatamani chanjo ije muda huu huu! Tuwaonee huruma wazee wetu na wengine wenye matatizo ya kiafya; corona ni hatari sana kwa uhai wao! Mataga achana nao hawafagi Corona wale!
India ndiyo walikuwa wasambazaji wakubwa wa chanjo unafahamu kinachowakabili?
 
Wazee ambao ndio wanapewa kipaumbele hawataki hata kusikia habari ya chanjo, ushauri wangu pengine viongozi wetu ngazi za juu wangeanza kuchanjwa kwanza wao ili kuleta hamasa na kuwadhibitishia wananchi kuwa haina madhara.
Wakichanja ipite miezi 6 ndiyo na wengine wafuate

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Chanjo ikija ni hiari ..hakuna mtanzania atakayelazimishwa..kuchanjwa..labda mahitaji yake tu ndio yamlazimishe..kwa mfano Nimesikia nchi inayopokea watu kuhiji..imesema atakayeruhusiwa kuingia kwenye nchi hiyo Ni aliyechanjwa..
Ila tusisilishane matango pori kwamba chanjo ni mtego kwetu Africa wakati watoto wetu wanadungwa chanjo kuanzia siku ya kwanza ya maisha yao..na hakuna chanjo hata moja inatengenezwa na wa Tz
Halafu unaweza kuta wenyeji hawajachanja hiyo chanjo, bali wageni ndiyo wachanje, halafu kile kipimo kipya cha China kina tumika kwasasa?

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Ile kamati ya Corona haikuja na majibu ya maswali kadhaa ambayo ni lazima yajibiwe kwanza kabla ya kutumia hiyo chanjo. Maswali hayo ni:-

(1) Mtu akipata hiyo chanjo hawezi kuambukizwa au kuambukiza Corona?

(2) Kama kweli hiyo chanjo inasaidia, kwa nini basi waliopata chanjo huko Duniani wanaendelea kuvaa barakoa na vifo vinaendelea kama kawaida?

(3) Ni Nchi gani Duniani wananchi wake wamepata chanjo na sasa Corona imetoweka katika Nchi hiyo?
Tunaomba kwanza Maswali haya yajibiwe kabla ya kutumia hiyo chanjo.
 
Ile kamati ya Corona haikuja na majibu ya maswali kadhaa ambayo ni lazima yajibiwe kwanza kabla ya kutumia hiyo chanjo. Maswali hayo ni:-
(1)Mtu akipata hiyo chanjo hawezi kuambukizwa au kuambukiza Corona?
(2) Kama kweli hiyo chanjo inasaidia, kwa nini basi waliopata chanjo huko Duniani wanaendelea kuvaa barakoa na vifo vinaendelea kama kawaida?
(3)Ni Nchi gani Duniani wananchi wake wamepata chanjo na sasa Corona imetoweka katika Nchi hiyo?
Tunaomba kwanza Maswali haya yajibiwe kabla ya kutumia hiyo chanjo.
Kamati ya kihuni ile na mabarakoa yao!
 
Back
Top Bottom