#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

#COVID19 Kwanini Watanzania wengi wanakataa chanjo ya Corona?

Unazungumzia kuvaa mask kama kielelezo cha kuchanjwa!!!!sisi hatuvai,tumechanjwa lini ndugu yangu??

Unajua israel ni % wamechanjwa!!!UK nako je??
Uk na Israel wako katika 60% huko sisi Tanzania hatujawahi kuwa serious katika lolote ni siku hizi tu unaona wanavaa mask sababu tu wameambiwa ukweli kiburi cha leo kina gharama zake huko mbele hakuna mtalii atakuja nchi hii ndio maana umesikia tusifiche data haingii akilini nchi yenye watu Million 60 eti Lab moja tu ya kupima. Watu wengi wameumwa huku miili yetu na population yetu kubwa vijana imesaidia huu ugonjwa ungekuwa ni wetu tu hakuna mtu angejali tatizo huu ugonjwa wa dunia unaweza usiumwe wewe lakini mwenzako unamletea shida sio suala la Tz hii ni WHO ni wa dunia. Rais kasema sisi sio kisiwa katika hili. swali lako la mask nchi nyingi ilikuwa kuvaa mask ni lazima public area sababu vaccination imekuwa na mafanikio sheria zinalegezwa. Sisi tujifananishe na Burundi tu katika hili. Leo airport ukifika unapimwa corona unajuwa kwanini? wameambiwa serikali hii jeuri yenu in gharama huko mbeleni. Kiujumla tumesalimu amri.
 
swali langu ni moji tu, Na hakuna hata mmoja amenijibu.. ikiwa chanjo ina ufanisi kwanini maambukizi bado yanaendelea duniani especially zile nchi zilizochanja wananchi wake? Mfano India na Brazil.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
India hawana ufanisi wala Brazil, India ni 2% tu wamechanja na Brazil 10% tu nchi zenye mafanikio makubwa katika chanjo ambazo wako kama 50 to 60 % ni Israel, UK, US, Canada na baadhi ya EU wako 35% na wagonjwa kwa kiasi kikubwa wamepungua au hakuna kabisa husikii tena watu kufa. India walidhani ugonjwa hauko tena wingi wa watu wao 1.2 Billion ni 2 % tu wamechanja sasa hivi ndio wana speed mchakato wa chanjo baada ya majanga haya.
 
Mtu anatishia kukataa chanjo ya corona wakati amechanjwa na tunandelea kuchanjwa (watoto kwa wakubwa) chanjo lukuki kama ya kifua kikuu,surua,polio, tetanus,homa ya ini, dondakoo, homa ya manjano na nyinginezo na zote zinatoka kwa mabeberu
 
Na hakuna anayehoji ubora wala usalama wa hizo chanjo...
 
swali langu ni moji tu, Na hakuna hata mmoja amenijibu.. ikiwa chanjo ina ufanisi kwanini maambukizi bado yanaendelea duniani especially zile nchi zilizochanja wananchi wake? Mfano India na Brazil.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Israel wamechanja 60%.... Maambukizi yamepungua toka malaki hadi mmoja kufikia 16 May.

Una swali jingine
 
Ww uli doubt effectiveness ya chanjo na ukaanza satire kwamba huko kwenye chanjo mbona maambukizi yanapaa na vifo vinaongezeka???

Sasa una maoni gani kuhusu case study ya Israel?
Mie sijawahi kuzungumza hivyo vitu, halafu cha ajabu bongo huku huwa mnasema corona ni ugonjwa wa kuja na kuondoka ndio sababu sasa bongo inaonekana hakuna corona ila huko vaccine ndio mnaisimia kuondoa maambukizi.
 
Mtu anatishia kukataa chanjo ya corona wakati amechanjwa na tunandelea kuchanjwa (watoto kwa wakubwa) chanjo lukuki kama ya kifua kikuu,surua,polio, tetanus,homa ya ini, dondakoo, homa ya manjano na nyinginezo na zote zinatoka kwa mabeberu
Sasa ameamua kuikataa chanjo ya corona kama alivyokuwa anaamua kuchanja hizo zengine kwa hiari.
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Mapendekezo yangu

1) Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa

2) Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea

3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo

4) Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi

Corona ipo, na uzuri mama yetu mpendwa halazimishi mtu apate chanjo, wewe na hiari yako.. ..lakini kuna baadhi ya wabantu washaanza mikelele yao ya kupinga hii chanjo, kwani umelazimishwa?

🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Mapendekezo yangu

1) Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa

2) Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea

3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo

4) Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
Watu wanaokataa chanjo wana sababu mbalimbali, zikiwemo zifuatazo:-
1. Kwa kutumia ule msemo wa akili za kuambiwa changanya na za kwako, wajanja wengi wamefuatilia trend ya kuzuka kwa ugonjwa huo Wuhan, China, hawaamini kabisa kuwa mpango wa chanjo hizo una nia njema kwa binaadamu, hasa wa nchi maskini na za dunia ya tatu.

Wanajihisi kutaka kugeuzwa bidhaa za kuyatajirisha makampuni ya chanjo, ambayo yanamilikiwa na mabepari wakubwa wenye uchu wa kutawala dunia kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Wanahoji, iweje hukotunakoambiwa wanakochanjwa, wanajifungia, na wanavaa mabarakoa ili kudhibiti ugonjwa huo, bado hakuoneshi dalili za kupata afueni, wakati sisi tusio na tahadhari wazitakazo, tukiwa bado salama zaidi?

Pia inastusha kuona eti "wataalamu" wetu waliopewa jukumu la kutathmini hali ya ugonjwa huo nchini wanakuja na majibu yaleyale yaliyokuwa yanatangazwa na kupigiwa debe na "Walanguzi wa kibishara wa kimataifa', bila hata kujipinda kutumia akili za ziada zinazoakisi mazingira na hali halisi ya Mtanzania!!.

Labda ni kweli mfumo wetu wa elimu ni duni kwa vile unakaririsha zaidi na kulisha matango pori ili wahitimu wendelee kuwa watwana wao perpetually, kuliko kuchochea uthubutu, udadisi, kujiamini na uzalendo.

Mganga aliyeturoga kama bado yu hai, atakuwa anatusikitikia sana kwa kuendekeza dezo, badala ya kujitathimini uwezo wetu na kuutumia katika kujiletea maendeleo endelevu kwa nguvu zetu na kwa matakwa na mbinu zetu wenyewe...
 
... siku hizi Mataga wanatambulika kama watanzania "wengi"? Be serious ndugu; labda hayajawahi kukukuta; nenda hospitalini uone wagonjwa wa Covid wanavyoteseka utatamani chanjo ije muda huu huu! Tuwaonee huruma wazee wetu na wengine wenye matatizo ya kiafya; corona ni hatari sana kwa uhai wao! Mataga achana nao hawafagi Corona wale!
Acha uonge wewe. Mtu ukimkuta anapumua kwa shida unasema ni Corona. Yapo magonjwa mengi ya shida ya kupumua na siyo Corona. kuna pumu, Ugonjwa wa moyo, Ugonjwa wa Figo na Pneumonia. Ukiangalia watanzania wengi hawana utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara, kwa hiyo mtu ghafla akipatwa na magonjwa ya aina hiyon niliyotaja basi wanakimbilia ni corona na kwa sababu hali imekuwa mbaya na daktari hawezi kupima vipimo vyote kwa wakati mmoja na mgonjwa akifa basi ni wengi wanasema ni corona
 
Jiwe na serikali yake ya walamba miguu waliwabrain wash sana baadhi ya waTZ vichwa Maji kuhusu Chanjo za kovid19 hazifai.

Chanjo ni Option ,anayetaka atachanjwa asiyetaka basi sio lazima.
Mkuu mimi huwa natembea sana maeneo ya tegeta, msasani na kawe naamini na watu wa mitaa mingine wanaweza toa ushuhuda wao hapa, frankly speaking watu huko mtaani wanaishi kama ni mwaka 2017 kurudi nyuma.
Corona ipo lakini ukiona hali ilivyomtaani kwakweli hofu na hamu ya kujikinga na hayo machanjo inaisha.
Sijui nyinyi mnaishije au watu ambao wanakuzunguka huwa wanavaa barakoa na kutake all precautions.
 
Mkuu inaonyesha haujui ugonjwa wa korona ulivyo!! Hapa tunalilia protection ya 3% population wasiondoke na korona.....3% ndio wahanga wa corona ...97% wana survive kwahiyo sizungumzia hao 97% wasiojali kabisa....tuwajali hao 3% wasiondoke na korona.....

Unajua kwamba katika 100 watakaopata korona 85 wanaweza kupona bila kuonyesha dalili? Kujazana kwenye masoko au madaladala bila kuvaa korona haimaanishi kwamba watu hawaambukizani au ugonjwa haupo....

ukitaka kujua stats za ugonjwa fika hospital.....Madaktari wanajua ila mimi na wewe ambao hatupo kwenye hizo kada tutaona kwamba korona hakuna coz watu hawavai barakoa na wanajazana kwenye masoko.
 
Baada ya kamati ya corona iliyoundwa na Rais wetu Mh Samia suluhu kupendekeza Wantanzania kupata chanjo, Watanzania walio wengi wamepinga sana kupata chanjo ya Covid 19.

Kwa hali Hii serikali inatakiwa iangalie kwa namna nyingine kwa Maana nchi na uongonzi wake ni watu ambao ni watanzania wala siyo kulazimisha ,naamini kupitia Rais wetu itaangalia zaid maoni ya Watanzania.

Mapendekezo yangu

1) Serikali iwe na Msemaji Mkuu wa Covid 19 ambaye ni Dr hasa kama katibu Mkuu prof Abel Makubi , awe siyo Mwanasiasa

2) Swala la chanjo huwezi lipinga kwa maana ndio Suluhisho la Kudhibiti ugonjwa tunakoelekea

3) Kwa Hali ya uelewa chanjo kwa sasa serikali isilazimishe ielewee wananchi wengi wako kwanin hawaitaki chanjo

4) Serikali iendele kusimamia njia za kujikinga na ugonjwa ichukue hatu kali bila kujali watanzania wanasemaje kwa ajili ya faida ya afya wengi
Wajane wa dhalim ndiyo hawataki chanjo wanataka wamfuate bwana wao
 
Back
Top Bottom