Watoto wa Nyerere wengine wamejikita kwenye utawa na parabolic thinking, kuna mmoja binti alikuwa ama sista ama anataka kuwa sista wa Roman Catholic. I am not sure if that was Rose.Kuna siku nimekutana naye kwenye Daladala Palm beach. Kakosa kiti kasimama, watu hata hawamjui, na yeye wala hajali yuko na hamsini zake. Yani hii sio zile za kuchonga za kina Lowassa apigwe picha na waandishi wa habari, hayo ndiyo maisha yake mwenyewe kakubali.
Sasa, dada kama huyu, hata interest ya uongozi na vyeo inaonekana hana.
Rafiki yangu Andrew yeye ndiye tulikuwa tunakutana Buddhist Temple kutafsiri Dhammapada (Buddhist Holy Book) iende Kiswahili, he was an ordained Buddhist monk at some point.
Charles Makongoro ndiyo huyo kawa mpaka Mbunge, kagombea urais kashindwa.
Madaraka alikuwa anafanya kazi zake tulikuwa tunamtembelea kwenye ki flat chake pale Upanga between Zanaki Secondary and Olympio Primary, yeye aliingia bungeni by proxy kupitia mkewe Leticia, alikuwa hataki makuu.
Kwani lazima kila mtoto wa rais awe Waziri au Rais?
Huyo kaka Mako ku serve ubunge haijatosha?