Rais George Bush wa Marekani aliambiwa na waanndishi wa habari kwamba kiwango cha kukubalika kwake, yani, "approval rating", kiko chini sana, akaulizwa kama hilo linamtatiza na analifanyia kazi vipi.
Rais akajibu kwamba yeye huwa hajishughulishi kuangalia approval rating, kwani ana kazi nyingi sana za muhimu za kufuatilia, na watu wanaomkubali watamkubali kwa kazi yake tu, na wasiomkubali, hata akijaribu kuwapendeza inawezekana ana pishana nao kifalsafa pakubwa sana.
Rais alionesha kwamba, hasumbuliwi na maneno madogo madogo yanayohusiana na muonekano wake, kuliko mambo ya msingi ya utendaji kazi wake.
Hili ni jambo la msingi. Kila dakika anayotumia rais kujikita kwenye kuuza sura, ni dakika ambayo haitumii kuangalia mambo ya msingi.
Inawezekana wapiga picha hawafanyi kazi yao vizuri, hilo si jambo ambalo rais anatakiwa kulipa headlines katika mazungumzo ya kitaifa. Hilo ni jambo la kuongea vikao vya ndani kifupi tu.
Kwa kujikita kuendekeza mazungumzo hayo, Rais Samia amejionesha anajali sana mambo ya muonekano kuliko mambo ya msingi.
Na ndiyo maana hata mambo ya maendeleo yanakuw magumu, kwa sababu Rais anapenda picha za kuonesha maendeleo ku;liko maendeleo yenyewe.