Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Rais Samia Suluhu amedai kwamba , Waandishi wa habari wanaandika kwamba kwenye ziara yake inayofanyika Nyanda za Juu Kusini watu wanaohudhuria ni wachache , Jambo analoliona kama ni Upotoshaji , Kwake yeye anaamini Umati ni mkubwa wa kutisha , amewaomba waandishi waandike uhalisia , huku akiwataka Wapiga picha wapande juu ili wapige vizuri picha za umati unaohudhuria mikutano yake .

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu hili ni jambo Jipya tangu niifahamu Tanzania , sijawahi kusikia Rais wa Tanzania akilalamikia kuhusu taarifa za ziara zake kupotoshwa na wanahabari na wapiga picha .

Hivi Ikulu haina Wapiga picha ambao wanaweza kunogesha
ziara ya Rais hata kwa Propaganda za uongo , kama enzi za akina Michuzi ?
Mods kuna Uzi kama huu humu jukwaani,kwa nini msiunganishe?

Mwisho wapigapicha wake ndio wanapotosha,kama aliwachukua wale wale wa Sukuma gang anategemea nini?

Badili safu hiyo.
 
Ukimaanisha nini? Watu walikuwa wachache au wengi? Maana video ziko YouTube unaweza kuona..

Concern ya Rais ni sahahi anachokutana nacho kwa watu ni tofauti na anachokiona kwenye picha..

Angalizo,kama wanahabari walikuwa ni Sukuma gang amekwisha awabadilishe haraka Sana.
Hawana sababu ya kuhariri hali halisi.
 
Tatizo letu Kitaa sio Umati...

Ni Mfumuko wa Bei.., Kushindwa mpaka leo kuwakabili maadui zetu watatu, tukiongezea na Adui mwingine wa ukosefu wa ujira...., Nadhani aki-concentrate huko hata ziarani akiwa peke yake bila kupokewa bado litakuwa sio tatizo..

By the way huenda huo Umati badala ya kumpokea ungekuwa unafanya issues productive huenda tungepiga hatua chanya
Tatizo la CCM ni kutokuwepo umati na ndiyo sababu hulazimika kubeba washangiliaji toka mji mwingine.
 
Mama amesahau strategy za
Jiwe za kubeba wanafunzi,
malori na ma trecta ya
wakulima kwenye mikutano.
Yaani mkutano wa Mbeya mjini
anaanda malori kutoka
Chunya, mbalizi, njombe🤣🤣
Ina maana gani hiyo ni kwamba watu wanataka kwenda ila shida usafiri ndio maana wanawapelekea magari au watu wa hilo eneo hawatoshi ndio uenda kuchukua watu wa sehemu zengine huko ili kuja kujaza?
 
Kwani ccm ishawaki kuwa na
hiyo Political Influence??
Nakwambia hivi bila vyombo
vya dola ccm ni sawa na
Chauma tu.
Ingekuwa hivyo mkuu upinzani usingekuwa inasumbuka kutafuta wagombea wa urais wenye ushawishi kiasi cha hadi kuchukua watu waliyotoka huko ccm, kwa maana kusingehitajika mtu mwenye ushawishi ili kushindna na ccm ambayo ni sawa na chauma.

Ni mtazamo wangu tu.
 
Rais Mh. Samia Suluhu Hassan ameonyesha wazi kutoridhika na utendaji kazi wa wapiga picha waliokuwa kwenye msafara wake kwa kushindwa kupiga picha nzuri zinazoonyesha umati wa watu wanaofika kumpokea. Rais Samia akiwa Njombe amelazimika kuwaagiza wapiga picha kupanda juu ya magari ili waweze kuchukua picha za umati wa watu na kuzifikisha kwenye umma ili kuondoa uzushi unaosambazwa kwenye mitandao kwamba mikutano yake haina watu wanaokwenda kumpokea zaidi ya maafisa wa serikali tu.

"Watu wa kamera pandeni juu ya gari, chukueni huu umati wa watu. Labda hawawaoni ndio maana wanaandika, na kila mkifika kila kituo chukueni umati wa watu" amesema Rais Samia. Sote tunajiuliza, iweje hao wapiga picha washindwe kutekeleza majukumu yao hadi kufikia hatua ya mkuu wa nchi kuwalalamikia kwamba wanashindwa ku cover mikutano yake vizuri. Je tukisema wapiga picha hao wanaendesha hujuma nzito dhidi ya ziara za Rais ili aonekane kwenye umma hapokelewi na watu wa kutosha tutakuwa tumekosea?

Mnaofahamu zaidi tuambizane.​
aache kujitutumua, kama anaendeleza kazi ana wasiwasi gani?
 
Ni suala tu la kufanya kazi ionekane, watu sasa hivi wanabadilika hawataki maneno mengi, huwezi kushinda muda wote unamwangalia kiongozi ilihali mtu anatakiwa kutafuta mkate, kiongozi anayefanya kazi nzuri hata njaa au kukosa pesa kwa muda huo unaweza ukaridhika tu ili mradi umsikilize.
 
I always say she is incompetent.
Mifumo ya nchi ikiwa perfect haijalish tatizo ni kusafiri kwenye mifumo mibovu.
Kuna watu wameathiriwa na kuvuli cha mtangullizi wake na hao ndio hawaishi kumlaumu.
Kiukweli mama ni binadamu na rais wa nchi. NI RAIS
 
Inaonesha Jiwe alikuwa na watu wengi sana.
Jiwe alipanga kikosi kweli kweli,hata Msigwa ni Jiwe alimuweka na Wana undugu wa kuoleana..

Ikulu na kila sehemu kulikuwa timu Jiwe na bado wako wengi Sana..

Kuwa na watu wengi ni sahihi kwa sababu alikaa miaka 5 so hata wewe lazima uweke timu yako..

SSH hawezi pangua wote at par ila atawang'oa taratibu.
 
11 Agosti 2022
Lupembe, Njombe
Tanzania 🇹🇿

Mh. Rais Samia Hassan awapiga kijembe waandishi wa habari


Watu ni wengi lakini mitandao inasema vingine, hivyo waandishi wa habari wapewa changamoto kuonesha ukweli ya kinachojiri katika safari yake ndefu ya kikazi kukagua maendeleo nyanda za juu kusini mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa
Source : mwanahalisi TV
 
Hatogombea Hilo liko wazi, tatzo Hasa ni muda uliobaki Hadi kufika 2025 pareeeefu sana, ni safari inayochosha akili na mwili.

Ameanza kukosa USINGIZI kama uncle.
Ameanza kukosa usingizi kama Uncle!!?

Umejuaje!!?

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Back
Top Bottom