Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Mbona ameeleweka au mnataka maneno tu?
 
Kama ilivyo suala la sensa, mtu una njaa utasubiri hadi uhesabiwe huku ukiulizwa maswali karibu 100
 
Namsubiri masuod kipanya na kibonzo chake juu ya huu ujumbe wa maushungi.
 
Na hili nalo mkalitizame kwa ukaribu
 
Mimi nilidhani Jiwe alikuwa na watu wenye kumuogopa tu.
 
Ukiwa na nchi ambayo matatizo yanatatuliwa na rais kwa mfumo wa hapo kwa papo, una tatizo kubwa kuliko rais wako.

Una tatizo la kukosa mfumo.

Na ndiyo maana huyo Magufuli mnayemsifia kwa kutatua matatizo yeye mwenyewe hapo kwa papo kama jambo hilo ni zuri, wengine tuliona jambo hilo ni baya.

Kwa sababu hakutengeneza mifumo endelevu inayoweza kudumu hata yeye akifa, alijilimbikizia madaraka.

Tatizo, watu wetu wengi wenye akili fupi walioshindwa kuona mbali waliona rais kutatua matatizo kwa style ya hapo kwa papo bila kuimarisha mifumo ni kitu kizuri.
 
Mama yetu anapenda sana promo za mitandaoni
 
Kiukweli Mh, anafanya kazi kubwa sana, changamoto kubwa ni hali ya uchumi mtaani, watu wako busy kutafuta chochote cha kuweka kinywani.
 
Bush unamchukuliaje mkuu
 
Bush unamchukuliaje mkuu
Katika lipi mkuu?

Watu wana pande nyingi sana ambazo zinakinzana.

Rais George W. Bush alikuwa rais mkubwa wa Africa, na alisaidia sana harakati za kutokomeza Malaria Tanzania.

Kwa hilo namuheshimu sana.

Ila kuna mambo ya kijinga kama kuiingiza Marekani kwenye vita Iraq, kwa ushahidi wa uongo wa WMD, naona alisababisha vita isiyo na sababu na kupelekea watu wengi - Wamarekani na wasio Wamarekani- kufariki.
 
Kama Raisi ana mandate! Alikua sawa kwa mtazamo wake
Hata kwa aliyo na mandate nayo, kuna calculus inatakiwa kuangalia.

Nini cha kufanya, nini cha kutofanya.

Hata cha kufanya, kipi cha kufanya wazi, kipi cha kufanya nyuma ya pazia na wasaidizi wake.

Rais kugombana sana na wapigapicha wake waziwazi anaweza kuonekana kama Kim Kardashian.
 
Anatumia ule wadhifa alionao bila kujua Kuna vitu anawakisea na kuwakwaza sana raia wake! Huyu mama 2025 akigombea tena atatumia pesa / nguvu nyingi sana!!
 
Anatumia ule wadhifa alionao bila kujua Kuna vitu anawakisea na kuwakwaza sana raia wake! Huyu mama 2025 akigombea tena atatumia pesa / nguvu nyingi sana!!
Tatizo si huyu rais, tatizo ni uongozi mzima wa Tanzania.

Huyu unaona mapungufu yake kwa kuwa yuko juu anamulikwa sana tu, ukimtoa na kumuweka mwingine naye utaona mapungufu yake hivyo hivyo.

Kikwete na Magufuli nao walikuwa hivyo hivyo.

Sasa utamtoa huyu umuweke nani ambaye atakuwa tofauti?
 
Ikiwezekana kila anapoenda aongozane na nguzo au miti ile mirefu akifika kwa mkutano aisindike,wapiga picha wapande wachukue picha umati wa watu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…