saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Rais Mh. Samia Suluhu Hassan ameonyesha wazi kutoridhika na utendaji kazi wa wapiga picha waliokuwa kwenye msafara wake kwa kushindwa kupiga picha nzuri zinazoonyesha umati wa watu wanaofika kumpokea. Rais Samia akiwa Njombe amelazimika kuwaagiza wapiga picha kupanda juu ya magari ili waweze kuchukua picha za umati wa watu na kuzifikisha kwenye umma ili kuondoa uzushi unaosambazwa kwenye mitandao kwamba mikutano yake haina watu wanaokwenda kumpokea zaidi ya maafisa wa serikali tu.
"Watu wa kamera pandeni juu ya gari, chukueni huu umati wa watu. Labda hawawaoni ndio maana wanaandika, na kila mkifika kila kituo chukueni umati wa watu" amesema Rais Samia. Sote tunajiuliza, iweje hao wapiga picha washindwe kutekeleza majukumu yao hadi kufikia hatua ya mkuu wa nchi kuwalalamikia kwamba wanashindwa ku cover mikutano yake vizuri. Je tukisema wapiga picha hao wanaendesha hujuma nzito dhidi ya ziara za Rais ili aonekane kwenye umma hapokelewi na watu wa kutosha tutakuwa tumekosea?
Mnaofahamu zaidi tuambizane.