Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha wazi kutoridhika na utendaji kazi wapiga picha walioko kwenye msafara wake kwa kushinda kupiga picha nzuri zinazoonyesha umati wa watu wanaofika kumpokea.

Rais Samia akiwa Njombe amelazimika kuwaagiza wapiga picha kupanda juu ya magari ili waweze kuchukua picha za umati wa watu na kuzifikisha kwenye umma ili kuondoa uzushi unaosambazwa kwenye mitandao kwamba mikutano yake haina watu wanaokwenda kumpokea zaidi ya maafisa wa Serikali tu.

"Watu wa kamera pandeni juu ya gari chukueni huu umati wa watu labda hawawaoni ndio maana wanaandika na kila mkifika kila kituo chukueni umati wa watu" amesema Rais Samia.

Sote tunajiuliza iweje hao wapiga picha washindwe kutekeleza majukumu yao hadi kufikia hatua ya Mkuu wa nchi kuwalalamikia kwamba wanashindwa ku Cover mikutano yake vizuri.

Je tukisema wapiga picha hao wanaendesha hujuma nzito dhidi ya ziara za Rais ili aonekane kwenye umma hapokelewi na watu wa kutosha au tutakuwa tumekosea?

Mnaofahamu zaidi tuambizane.
Ni kweli mkuu watakuwa ni wale Sukuma gang..

Amewatolea uvivu pale Mtwango kwamba hawawaonyeshi watu Hali Halisi ya mikutano ya Rais kwa sababu wanazozijua Wao..
 
Hujuma za waziwazi hizi wako ambao wanaumia kweli juu ya urais wa MH. SAMIA, alipaswa kubadilisha timu yote ya mwendazake mara moja, ndio wanaohujumu kwani hamfahamu katika ziara za namna hii hapo baadae hupunguza UGUMU wa kampeni maana mama anakwenda kila chochoro nyanda za juu kusini huku akifungua miradi mingi kweli tena mizito lakini maredioni hatuoni zile taarifa zilizotufikia wakati huu kama ilivyokuwepo wakati hule.
SSH sio mzuri katika suala zima la mtandao wa kumuandika vizuri kumlinganisha na hayati JPM. Hazifahamu na haziwezi zile siasa za kuvimiliki vyombo vya habari na vikawa chini ya amri zake.

Akiuweza upande huo wa uongozi wake hakika atakuwa katika viwango sawa na hayati JPM. Kakubali kuruhusu media zifanye kazi kadri zinavyoweza na hiyo ni kwa hasara ya urais wake.

Achape tu kazi apunguze malalamiko.
 
SI KILA NYOMI INAMAANISHA KUPENDWA. Kuna wengine huwa wanakuja eneo husika kwa sababu zingine nje ya kutaka kumsikiliza, mfano;
1. Mtu anataka kumuona LIVE aliyesema UKIZINGUA NAKUZINGUA
2. Mwingine anataka kujua idadi ya magari kwenye msafara
3. Mwingine anataka kujua ulinzi wa rais unafananaje
etc
Hapo kwenye namba 3 ndio palikuwa panafanya niende mikutano ya jiwe coz kuna jamaa alikuwa ni mwanatimu ya ulinzi wa jiwe alafu namfahamu vzr
 
Tatizo letu Kitaa sio Umati...

Ni Mfumuko wa Bei.., Kushindwa mpaka leo kuwakabili maadui zetu watatu, tukiongezea na Adui mwingine wa ukosefu wa ujira...., Nadhani aki-concentrate huko hata ziarani akiwa peke yake bila kupokewa bado litakuwa sio tatizo..

By the way huenda huo Umati badala ya kumpokea ungekuwa unafanya issues productive huenda tungepiga hatua chanya
 
Debe la Mahindi 18,000/- hadi 23,000/
Petrol 3,456/-
Debe la mchele 38,000/- hadi 45,000/- n.k
Mita ya Umeme kutoka 27,000/- hadi kufikia 370,000/-kwa new connection

Kwa mfumko huo wa gharama za maisha alafu unategemea watu watajaa kwenye mikutano yako, wafate nini kama umeshindwa kuudhibiti?
 
Kulikuwa hakuna haja ya kuwaita wapande juu ya magari ili kupata picha.

Umati unaonekana tu hata ukiwa chini.

Watu wana njaa, maisha yamepanda mno, ashughulikie hilo,
Sasa mbona Kuna umati ila kwenye picha za mitandaoni haonyeshi,hiyo ndio concern ya Rais..

Nimefuatilia ziara yote toka Mbeya,Kote huko Rais amepokelewa kwa shangwe na umati mkubwa sana..

Ila pale Makambako ilikuwa noma zaidi.
 
Niliona kwenye ITV walijaribu kuhariri alipokuwa Kyela ila la, picha ilikuwa ikichezacheza tofauti na picha ya mama, nilichoka.
Ukimaanisha nini? Watu walikuwa wachache au wengi? Maana video ziko YouTube unaweza kuona..

Concern ya Rais ni sahahi anachokutana nacho kwa watu ni tofauti na anachokiona kwenye picha..

Angalizo,kama wanahabari walikuwa ni Sukuma gang amekwisha awabadilishe haraka Sana.
 
Debe la Mahindi 18,000/- hadi 23,000/
Petrol 3,456/-
Debe la mchele 38,000/- hadi 45,000/- n.k
Mita ya Umeme kutoka 27,000/- hadi kufikia 370,000/-kwa new connection

Kwa mfumko huo wa gharama za maisha alafu unategemea watu watajaa kwenye mikutano yako, wafate nini kama umeshindwa kuudhibiti?
Aisee kwa Mazao hata 100,000 mtanunua,hutaki kalime..

Yaani nikulikie mimi wewe unenepeshe kitambo mjini? Kuwa serious.
 
Wapiga picha wa ziara zote za rais wanatoka Ikulu (hivyo wapiga picha wale ni wana-usalama.) Ni masikitiko makubwa kuona mpiga picha wa Ikulu hujui namna nzuri ya kupata picha.
 
Raisi kama ana fanya kazi yake ana anzaje kulilia nyomi ye si apite zake tu kimya kimya
Rais halilii nyomi analilia ukweli ndio maana hao Wana habari wapo..

Wewe ukienda kwenye msiba ukakuta nyomi na mwingine hakuna nyomi utapata picha gani hapo?
 
Back
Top Bottom