Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Rais George Bush wa Marekani aliambiwa na waanndishi wa habari kwamba kiwango cha kukubalika kwake, yani, "approval rating", kiko chini sana, akaulizwa kama hilo linamtatiza na analifanyia kazi vipi.

Rais akajibu kwamba yeye huwa hajishughulishi kuangalia approval rating, kwani ana kazi nyingi sana za muhimu za kufuatilia, na watu wanaomkubali watamkubali kwa kazi yake tu, na wasiomkubali, hata akijaribu kuwapendeza inawezekana ana pishana nao kifalsafa pakubwa sana.

Rais alionesha kwamba, hasumbuliwi na maneno madogo madogo yanayohusiana na muonekano wake, kuliko mambo ya msingi ya utendaji kazi wake.

Hili ni jambo la msingi. Kila dakika anayotumia rais kujikita kwenye kuuza sura, ni dakika ambayo haitumii kuangalia mambo ya msingi.

Inawezekana wapiga picha hawafanyi kazi yao vizuri, hilo si jambo ambalo rais anatakiwa kulipa headlines katika mazungumzo ya kitaifa. Hilo ni jambo la kuongea vikao vya ndani kifupi tu.

Kwa kujikita kuendekeza mazungumzo hayo, Rais Samia amejionesha anajali sana mambo ya muonekano kuliko mambo ya msingi.

Na ndiyo maana hata mambo ya maendeleo yanakuw magumu, kwa sababu Rais anapenda picha za kuonesha maendeleo ku;liko maendeleo yenyewe.
Kuwajua wanawake aitaki uende darasani, anataka aonekane alivyokuwa mrembo kwenye mahala pakupiga kazi. Rais maskini wa fikra sana huyu. Tanzania nchi yangu yenye maajabu ya karne.
 
Kuwajua wanawake aitaki uende darasani, anataka aonekane alivyokuwa mrembo kwenye mahala pakupiga kazi. Rais maskini wa fikra sana huyu. Tanzania nchi yangu yenye maajabu ya karne.
Hili si suala la wanawake, marais wote wa Tanzania wameuza sura.

Na kwa kweli, kuuza sura ni sehemu ya kazi ya urais.

Wanasheria wana msemo wao kwamba haki si tu ifanyike, bali pia ionekane kwamba imefanyika.

Kwenye siasa nako ni hivyo hivyo, watu wana haki ya kikatiba ya kujulishwa habari za uongozi wa nchi yao.

Kwa hivyo, kwa upande fulani, rais asiyejali image ni rais asiyejua kazi yake.

Ila, kuna namna ya ku handle image bila ya kufanya habari ya image iwe ina derail mazungumzo.

Samia kashindwa kuweka proportion, inaonekana kuwa anakereka sana na anavyosemwa, na hana kifua cha kupuuzia maneno asiyajibu wakati hapohapo anayafanyia kazi.

Kwenye kujali image ni sawa rais kujali image. Na marais wote wamekuwa so careful kwenye image.
 
Rais yupo concerned na mambo yasiyo na tija mitandaoni ilhali kuna issues kibao tu humu ambazo hata hazizungumzii.

Wastaafu wengi wanadai mapunjo ya pensions zao na waziri anacheza reggae tu.

At anasafiri akisikiliza mtu mmoja mmoja.
 
Baada ya awamu ya kwanza ya Kikwete wananchi wengi wanaokwenda kwenye mikutano ya kiserikali wanavutwa yeye si wa kwanza. Kwa Magufuli walikuwa wanasombwa kwa malori kupelekwa wilayani.
Wasombaji wamehamia UKAWA eti?
 
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha wazi kutoridhika na utendaji kazi wapiga picha walioko kwenye msafara wake kwa kushinda kupiga picha nzuri zinazoonyesha umati wa watu wanaofika kumpokea.

Rais Samia akiwa Njombe amelazimika kuwaagiza wapiga picha kupanda juu ya magari ili waweze kuchukua picha za umati wa watu na kuzifikisha kwenye umma ili kuondoa uzushi unaosambazwa kwenye mitandao kwamba mikutano yake haina watu wanaokwenda kumpokea zaidi ya maafisa wa Serikali tu.

"Watu wa kamera pandeni juu ya gari chukueni huu umati wa watu labda hawawaoni ndio maana wanaandika na kila mkifika kila kituo chukueni umati wa watu" amesema Rais Samia.

Sote tunajiuliza iweje hao wapiga picha washindwe kutekeleza majukumu yao hadi kufikia hatua ya Mkuu wa nchi kuwalalamikia kwamba wanashindwa ku Cover mikutano yake vizuri.

Je tukisema wapiga picha hao wanaendesha hujuma nzito dhidi ya ziara za Rais ili aonekane kwenye umma hapokelewi na watu wa kutosha au tutakuwa tumekosea?

Mnaofahamu zaidi tuambizane.
Aachane na hao waandishi kama hana imani nao Raisi awe anatembea na kamera yake anajipiga mwenyewe akiwa na umati amesimama juu ya gari na kurusha mitandaoni atakuwa amemaliza fitina
 
2025 wala asigombee. Hana haiba ya leadership. Kina Mwigulu wanamgeuza geuza kama chapati.
Hatogombea Hilo liko wazi, tatzo Hasa ni muda uliobaki Hadi kufika 2025 pareeeefu sana, ni safari inayochosha akili na mwili.

Ameanza kukosa USINGIZI kama uncle.
 
Kulikuwa hakuna haja ya kuwaita wapande juu ya magari ili kupata picha.

Umati unaonekana tu hata ukiwa chini.

Watu wana njaa, maisha yamepanda mno, ashughulikie hilo,
Yaani uuvizie umati kuupiga picha.?!
 
Kazi anayofanya Mama Samia ni kubwa mno. Au hamwoni Mbowe na chama chake wako kimya wanafurahia kishindo cha Mama Samia?
 
Ndiyo kwanza Agosti, sijui ikifika Mwezi Disemba hali itakuwaje 🙆
Itakuwa hivyo hivyo,kwanza mshukuri Bei zimeshuka kidogo maana natamani gunia lifike laki Ili nipige hela ila sioni likifika hata hiyo disemba au mwezi wa 2 unless mvua zizingue.
 
Hiyo inatusaidia nini kupambana na ugumu wa maisha?
 
Back
Top Bottom