Camera ni kisingizio, haiwezekani video zinazorushwa ambazo ni ndefu sana kukosa kuona umati. Kubwa ni kuwa ziara hizo hazisemi kuwa kiongozi leo ana miadi ya kufanya nini kwa manufaa ya wanaotembelewa na pia mguso mkubwa kitaifa.
Lakini ziara ikiwa imekaa kama sherehe, nderemo, vifijo na matamasha bila ujumbe basi hukosa mvuto.
Lazima idara ya Mawasiliano ikulu iseme madhumuni ya ziara siku kibao kabla ya safari na pia kiongozi ajikite katika kutatua au kubainisha mikakati ya kutatua changamoto za wananchi.
Watu hawaangalii video sababu kwanza hawana bando la kutosha kutokana na ughali wa huduma hiyo , pia hata wenyewe nchi wamiliki wa YouTube, FB, Twitter , TIKTOK n.k au vituo vya televisheni hawana mtindo wa kurusha video au ziara live / mubashara ya masaa mawili, matatu au manne kama wafanyavyo waandishi wa habari wa kiTanzania wawe wa Ikulu au vituo binafsi na TV za online mitandao .
Wenzetu hurekodi, halafu wakafanya editing / review kuona ktk tukio zima ni jambo gani la msingi limeongelewa na kurusha kipande hicho.
Suala hili halina cha watu kutaka kuona umati au ulinzi au wasanii walitumbuiza nini ktk ziara ya kiongozi.
Watu wamekinai habari ndefu zilizopitiliza au mapicha picha ambayo hayatawasaidia ktk kukabiliana na ugumu wa maisha walio nao.
Watu wanahamu ya kujua serikali ina mikakati gani kutatua changamoto kibao tena kwa kifupi tu na siyo hotuba ndefu za kupitiliza ambapo pia wamechomekea sala, dua , kampeni ya CCM 2025, ngoma na tamasha hii ni kwa kutaja machache mengi yanayochomekwa ktk ziara ya rais.