Kwanini watu wanachukia sana Ugali. Kwani ugali una kosa gani jamani?, Wanasayansi njoeni basi mtupe Elimu

Ugali wa dona una viritubisho vingi vya protein. Huu ni mzuri sana.

Tatizo ukikoboa unaondoa protein yote unabakisha wanga tu, usio na virutubisho. Ni nishati tu isiyo na virutubisho.

Na Watanzania wengi wanakula ugali wa kukoboa.
 
Ugali ungekua ni chakula cha maana basi ungekua unaukuta kwenye sherehe,

Ulishaenda kwenye sherehe ukakuta Ugali na Bamia?

Wewe mwenyewe ukikuta Ugali harusini lazima uwaseme wahusika,ugali unaliwa ili kujaza tumbo tu.
ugali mbona mtamu ukipata mboga nzuri?

nakumbuka shule waliluwa wananiita mr bean kwa jinsi nilivyokuwa nafakamia ugali maharage

na sijawahi tena kula ugali maharage mtamu kuliko ule wa pale tengeru boys sekondari

#ugalimenukali
 
Ugali unadumaza akili ndo mana Africa hatunaga akili. Je akili ni nn? ukitoa kile ulichofundishwa kinachobaki kichwani mwako ndo akili. Ndo mana hatuna ubunifu kama wazungu kila kitu tunasubiri wazungu wabuni kisha na ss tutumie. Mfano kadhaa ni cm, gari, meli, ndege, na vitu vngine kibao
 
Ukiwatoa waarabu wa afrika, nadhani Ugali ndio chakula kinacholika zaidi na wafrika wenye ngozi nyeusi...hata mimi binafsi bila ugali maisha yatakuwa hayaendi poa, wali huwa unanikinai mapema mno...
 
ugali mbona mtamu ukipata mboga nzuri?

nakumbuka shule waliluwa wananiita mr bean kwa jinsi nilivyokuwa nafakamia ugali maharage

na sijawahi tena kula ugali maharage mtamu kuliko ule wa pale tengeru boys sekondari

#ugalimenukali
Kumbe umesoma tengeru boys
Enzi hizo tulikuwa tunawaona wakaka wa pale ni mahandsome tunaawashindanisha na wakaka wa ilboru 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…