Kwanini watu wanachukia sana Ugali. Kwani ugali una kosa gani jamani?, Wanasayansi njoeni basi mtupe Elimu

Kwanini watu wanachukia sana Ugali. Kwani ugali una kosa gani jamani?, Wanasayansi njoeni basi mtupe Elimu

Ugali ni cheap food.
Kitu chochote kikiwa cheap kinapoteza mvuto.

Lakini hata anayechukia ugali hawezi kula chakura akipendacho mfululizo.
 
Ugali uupige na nyamachoma, ndimu na kachumbari ya kwenda.

Ugali ule na kambale alioungwa na nazi 🤣

Ugali na kitimoto rosti acha kabisa.
Yesssss ugali una mboga zake bwanaa
 
Cha kushangaza,

Nilivyoanza kuishi morogoro na dar es salaam, nilishangaa sana watu kudharau dona na kusema ni chakula cha masikini. Eti dona inanenepesha.

Halafu ni kama ugali unachukiwa zaidi huku dar es salaam kuliko mikoani.
Tuna ubaguzi wa rangi mpaka kwenye ugali 😂😂😂.
 
Nadhani tungeongeza ubunifu katika mapishi yetu. Hivi waafrika kabla ya ukoloni tulikuwa tunakula nini, mbona vyakula vyote tunavyokula vina asili ya nje? Ugali unaonekana jau kwa sababu ya jinsi tunavyoupika. Tuuongezee ubunifu.
 
Bado hamjasema wazee bado hamjasema! Alisikika mwanaume wa dar mmoja pale kibaha
 

Attachments

  • 20241005_171740.jpg
    20241005_171740.jpg
    746 KB · Views: 6
Back
Top Bottom