Kwanini watu wanachukia sana Ugali. Kwani ugali una kosa gani jamani?, Wanasayansi njoeni basi mtupe Elimu

Kwanini watu wanachukia sana Ugali. Kwani ugali una kosa gani jamani?, Wanasayansi njoeni basi mtupe Elimu

Ugali hauna shida, ugali wa mihogo na kisamvu kilochoungwa na karanga na nazi na dagaa pembeni ni chakula kitamu sana.
Naona wapenda ugali kuna kitu hamkielewi,

Ukishasema ugali unakua mtamu kwa kusifia mboga ambazo utakula na huo ugali,tayari unakubali kua Ugali sio chakula kizuri ila mpaka upate support ya mboga fulani,

Hizo mboga zikiufanya ugali kua mtamu basi ni sifa kwa mboga sio kwa ugali.
 
Hao ugali wanakataa hapa tu, utaukaataje ugali, upate ugali nyama choma, ugali nyama rost, ugali samaki rost, ugali na mlenda kah! unaachaje kula ugali?

mimi nisipokula ugali nakuwa mgonjwa,
 
Naona wapenda ugali kuna kitu hamkielewi,

Ukishasema ugali unakua mtamu kwa kusifia mboga ambazo utakula na huo ugali,tayari unakubali kua Ugali sio chakula kizuri ila mpaka upate support ya mboga fulani,

Hizo mboga zikiufanya ugali kua mtamu basi ni sifa kwa mboga sio kwa ugali.
Kawaida hiyo. Hata wali bila mboga haunogi, au ngano yoyote bila mafuta, chumvi, viungo flani hauko sawa.

Carbohydrates nyingi zinahitaji kitu cha kusindikizia ili ushuke, ukishindwa kabisa kupata mboga unaweza kushusha na maziwa, hata maji.
 
Ugali ni chakula bora sana

Una virutubisho vingi muhimu sana. Una madini mengi kama Zinc, magnesium, sodium, calcium, iron, selenium, unasaidia kuimarisha mifupa, meno, damu, cells, unakupa nguvu, hauna gluten, nk.

Inakufanya uwe umeshiba kwa muda mrefu kwahiyo inaweza kusaidia kupunguza kula hovyo hovyo kila saa na uzito.
 
Kipindi hicho nikijua ratiba ya mama usiku anapika ugali.
Nilikuwa nalala mapemaaa.
Kula mpaka niamshwe na ninaweza nisiamke.ila siku ya ubwabwa. Ahaa macho kwa macho.
 
basi ugali ni chakula bora,hii hukumu isiangalie mahindi tu!

mtu akipika ugali wa ngano asidhaniwe anakula mahindi.
Ugali wa mahindi ambayo hayajakobolewa kiafya ni chakula kizuri kuliko hivi vyakula vingi vinavyotengenezwa na ngano kama chapati, maandazi, macaroni, mikate mweupe nk.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom