Kwanini watu wanaezeka paa linaenda juu hadi nyumba inakuwa kama piramidi?

Wengi watasema ni mwonekano ila faida ni kutiririsha unyevu kwa haraka na kusaidia bati kutokushika kutu kirahisi pia husaidia kuzuia joto.
Wazungu huwa wanajenga hivyo kuzuia barafu kukwama na kushusha paa.

Pia wao kwenye dari(Attic) kunakuwaga na vyumba vya kulala kabisa.

Sasa huku kwetu, ukizingatia imeanza siku hizi bati ni za rangi, point ya maji kutuama na kushika kutu haina nguvu.

Joto ni point nzuri japo utazikuta hata Njombe na Mafinga
 
Nyingi sababu zinakuwa kutoruhusu matope ya maji kukaa hata sekunde ili kupunguza kuntu..
Pia nafikiri kwenye mambo ya ujenzi kuna standard ya umbali wa paa na dari ili kukinga nyumba na joto.

Sidhani kama tunapaswa kujenga nyumba kama mapiramidi.

Ingefaa tungejua standard ipo namna gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…