Kwanini watu wanaezeka paa linaenda juu hadi nyumba inakuwa kama piramidi?

Kwanini watu wanaezeka paa linaenda juu hadi nyumba inakuwa kama piramidi?

Nyingi sababu zinakuwa kutoruhusu matope ya maji kukaa hata sekunde ili kupunguza kuntu, kingine hata joto pia linapunguza panakuwa na distance kutoka kweny paa mpaka kweny Gypsum kwa eneo la katikati.
Mnajiongelesha Mambo yasiyo na msingi,ukuta standard Ni kuanzia mita 3 na madirisha walau ya 5*5 ft kulingana na Hali ya hewa ya mahala..

Sasa kwa kina Cha mita 3 ,Hilo joto linatoka wapi?
 
Ni:-
1. Ni nzuri kimuonekano/Fashion
2. Ukiwa ndani hutazisikia kelele za kwanye paa e.g. mtanuko (expansions na contractions) yoyote kwenye paa hutaisikia japo iko, kelele za mvua na radi
3. Ni rahisi kupita ili kufanya shughuli mbalimbali ndani ya paa e.g. wiring, kudhibiti wadudu/wanyama e.g. popo, nyuki n.k.
4.Joto litokanalo na bati linadhibitiwa(Control) i.e. halifiki chini wanakoishi watu kutokana na umbali uliopo kati ya ceiling na bati
5.Paa haliezuliwi kirahisi na upepo mkali/kimbunga
Ni:-
1. Matumizi mabovu ya rasilimali fedha (it is uneconomical) kwani unatumia bati nyingi, mbao nyingi na misumari kgs.nyingi bila sababu za kimsingi
2. Kutokana na mteremko mkali (Slope/angle of inclination), maji yatiririkayo kutoka kwenye paa e.g. ya mvua huwa na kasi kubwa(speed) na hivyo huchimba sana ardhi-mzunguko wa nyumba na wakati mwingine husababisha uharibifu mkubwa katika mazingira yazungukayo nyumba hiyo.
3. Ni vigumu au huwa ni changamoto kubwa kufanya ukarabati juu ya paa e.g. roof filling au kufagia (Usafi) wa takataka/vumbi ziletwazo na upepo na kunasa juu kwenye paa
##4**Paa hilo likishika moto kwa kweli hakuna rangi utaacha kuona kwani kuna fuel(Mbao/kuni) za kutosha na sio rahisi kupanda huko kama wewe sio jasiri au mtaalam ili ukapambane na moto kichaa utakaokuwepo.
-Kwa maoni yangu wewe Lycaon pictus(mbwa mwitu), akili za kupewa ongezea na za kwako. Je, katika mazingira unayoishi ni lazima paa la nyumba yako liwe hivyo? (Unaiga tu kama fashion ili umpendezeshe nani), Je utamudu gharama husika bila kuathiri/kukwamisha shughuli zingine za kimaendeleo za familia yako?
Ni hayo tu. (Samahani lakini kama nimekuudhi hapo juu kwa kulitaja jina lako kwa kiswahili/kibongo)
Nakataa paa refu kushinda ukuta Wala huwa sio nzuri kimuonekano..

Ukitaka muonekano mzuri paa liwe na urefu pungufu ya ukuta..

Ukuta mita 3 afu paa mita 6 Kuna uzuri gani hapo zaidi ya kuwa Kama kitu kimefunikwa? Shepu ya Uyoga.
 
Huo ni ushauri wa Kitaalam.

Mimi nilishauriwa kuwa Paa la chini ni British Style ya zamani sana.

Na Paa la juu ni ya kisasa ya French Style.

Eng aliendelea kueleza kuwa King Post ya Paa inatakiwa iwe na urefu sawa na Nusu lipenyo cha Boma la nyumba. Let say kama nyumba ni ya mraba upana 10M ×10M then King post inatakiwa iwe 5metres above. Hii ni kwa mujibu wa vipimo vyao vya researched evidences na sio porojo za mafundi.

Baada ya kunishawishi ilibidi nikubaliane na ushauri wa kitaalam


Hata hivyo kuna ishu ya utashi na mapenzi unaweza kuezeka unavyotaka
Porojo hizo zisizo na msingi..
 
Wengi tunajenga hivyo sababu kuu ni muonekano mzuri
Niwekee nyumba yenye paa refu afu tulinganishe na hizi zenye paa la wastani yaani ukuta mrefu kuliko kingpost 👇
 

Attachments

  • NDENJE LAST PLAN1.png
    NDENJE LAST PLAN1.png
    112.4 KB · Views: 26
  • NDENJE LAST PLAN-1.png
    NDENJE LAST PLAN-1.png
    115.7 KB · Views: 24
  • MWAMBESO FINAL PLAN.png
    MWAMBESO FINAL PLAN.png
    44.9 KB · Views: 25
  • MWAMBESO FINAL PLAN1.png
    MWAMBESO FINAL PLAN1.png
    51.2 KB · Views: 26
  • MWAMBESO FINAL PLAN2.png
    MWAMBESO FINAL PLAN2.png
    47.2 KB · Views: 24
  • MWAMBESO FINAL PLAN3.png
    MWAMBESO FINAL PLAN3.png
    62.7 KB · Views: 21
  • MWAMBESO FINAL PLAN4.png
    MWAMBESO FINAL PLAN4.png
    32.9 KB · Views: 29
Back
Top Bottom