Kwanini watu wanaogopa sana kuiba umeme wa TANESCO kuliko maji ya DAWASCO?

Kwanini watu wanaogopa sana kuiba umeme wa TANESCO kuliko maji ya DAWASCO?

Hivi kinachofanya watu waogope kiasi hiki kuiba umeme ni nini hasa? Mbona mitaani wanakata mabomba ya maji na ku-bypass bila uwoga?
Ukiona hawaibi ujue hawana ujuzi na umeme, nimekaa miaka 3 msewe pale hatujawahi kulipa luku tunalipa buku kila baada ya miezi miwili luku iwe active. Utoto raha sana
 
Sababu pia umeme mita kupelekwa juu ya nguzo Ni kupunguza uwezekano wa waz
 
Mwizi 34 : 7-9
Kama umeshindwa usiropoke hadharani

Adhabu yako kulingana na sheria yetu kesho tunakuja kukuibia
By katibu
 
Ukiona hawaibi ujue hawana ujuzi na umeme, nimekaa miaka 3 msewe pale hatujawahi kulipa luku tunalipa buku kila baada ya miezi miwili luku iwe active. Utoto raha sana
Aisee, Msewe sio?
 
Ukikamatwa faini ni kubwa mno tena unawezwa kutumikia kifungo pia ,kuna jamaa mmoja jirani aliachia miti ya ukuta wa fensi hadi kufika kwenye nguzo kumbe alikuwa anaunganisha nyaya kwenye umeme anapiga umeme wa bure ,mchana anazitoa usiku anaziunganisha , akajisahau akawa anaacha kabisa nyaya hata mchana ,gafla akashtukizwa alipigwa faini Kama mil 5 halafu na kifungo
 
Ukiona hawaibi ujue hawana ujuzi na umeme, nimekaa miaka 3 msewe pale hatujawahi kulipa luku tunalipa buku kila baada ya miezi miwili luku iwe active. Utoto raha sana
Huko huko Msewe miaka kadhaa nyuma hela ya umeme ya mwezi tulikuwa tunampa mwenye nyumba hela yoyote uliyonayo mfukoni. Yeye kazi yake ni kuhakikisha umeme upo muda wote.
 
Kuna best angu alitembea na nyaya za tanesco kama kg 800 hiv

Wakamdaka Dec 2021 ndio ameanza kifungo chake cha miaka 16 gerezan na ana familia ya watoto 4 na mke juu

Wahuni wameshaanza kuruka na mkewe kiroho safi tu yan
 
Hivi kinachofanya watu waogope kiasi hiki kuiba umeme ni nini hasa? Mbona mitaani wanakata mabomba ya maji na ku-bypass bila uwoga?
Usidhubutu kuiba au kuhujumu miundombinu ya TANESCO na unapoona viashiria vyovyote tupigie simu mara moja kwa namba zetu 0748550000.

Tunatoa zawadi nono kuanzia Tsh laki moja na kuendelea

Kiasi cha zawadi kinatokana na kiasi cha upotevu kilichookolewa

TANESCO, tupo Kazini
 
Hahaha dili hili hapa
 
Umeme unahitaji ufundi na utundu mwingi. Vilevile changamoto nyingine ni urefu wa nguzo au juu ukutani.

Ukianza utundu(wizi)kila mtu anakuona mubashar.

Halafu,umeme ni moto ule.Ukileta maskhara unakufa au kupata majeraha au ulemavu.

Tofauti na maji ambapo miundombinu ipo ardhini.Ukianza wizi wako wachache wataweza kugundua.

Unaunganisha kwa ulaini huku umeshika jembe kama upo bustanini.

Swali lingine,mwizi mwenzetu.
Asante sana mwizi mwenzetu. Hebu sasa tupe maujanja ili tuendelee na kazi yetu bila wasiwasi. Hapo juu mimi naona unatuogopesha ili tuache kazi hii, tupatie suluhisho basi.
 
Back
Top Bottom