Wanadamu ndio wanachagua Maisha. Kasome Jiografia utajifunza Factors zinazopelekea Watu kuanzisha Maisha na makazi katika sehemu Fulani. Ila yote ni uchaguzi.
Mkuu umeandika mambo mengi sana kujaribu kumnasua Mungu wako ambae hayupo, na hawezi kujinasua kwenye hii mitego.
Hyo elimu unayoisema ni zao la baadae sana baada ya watu kujifunza kuhusu matetemeko,
Je kabla ya elimu hii ya tetemeko kwanini Mungu hakuwajulisha kwa kuwapa allert msiishi maeneo hayo?
Na kama anaupendo wote kwanini ameweka tetemeko, tetemeko ni la kazi gani yeye sasa kuliweka?
Huwezi ishi Jangwani au sehemu yenye matetemeko(iliyopitiwa na blonde la Ufa, au lenye Plate movements Kwa Chini) alafu siku tetemeko kilitokea mkifa useme hukuchagua.
Huwezi ishi eneo la mabondeni kama Pale Jangwani alafu yatokee mafuriko Watu wafe(mfe) alafu useme haukupenda.
Huwezi amua ishi maeneo yenye Tufani na vimbunga vya baharini alafu siku tsunami ikitokea useme Mungu kawaadhibu.
Huwezi ishi sehemu yenye Mvua chache au yenye ujangwa alafu useme Mungu anataka mfe na Njaa. Utakuwa punguani wa mwisho Kabisa
Hapo ni unajitetea tu, na hoja yako haina mashiko.
Kama mungu ameyaumba yote hayo, kwanini hajawapa nauli watu wahame wasiishi hayo maeneo yenye matetemeko kama unavyodai.
Huoni wale watoto wasio ma uwezo wa kujiamlia kuhama maeneo hayo, wakikumbwa na matetemeko utasema wamechagua?
Watoto walichagua kuzaliwa hayo maeneo.
Sijakuelewa na hoja yako haina mashiko.
Sasa nijibu hapa chini nikubali kama kweli mabaya ni uchaguzi, 👇👇
Vipo visa vya vimondo kuua watu ni pamoja na tukio la meteoriti lililotokea mnamo mwaka 2013 huko Chelyabinsk, Urusi. Kimondo kilichoingia angani kilipasuka juu ya mji huo, kusababisha vioo vingi kuvunjika na watu wengi kujeruhiwa kutokana na vipande vya vioo.
Moja ya visa maarufu ni lile la Tunguska huko Siberia, Urusi mnamo tarehe 30 Juni 1908. Kimondo kikubwa sana kilipasuka angani na kusababisha mlipuko mkubwa,
Je hapa unasemaje kuhusu dhana yako ya uchaguzi?