Aliyekuambia Elimu ya Jiografia ni Elimu ya baadaye ni Nani?
Kasome Geomorphology ndio utajua kazi ya matetemeko, volcano, tsunami n.k. katika huu Ulimwengu. Uache ujinga na umbumbumbu kwenye mambo usiyoyajua.
Unafikiri pasipo volcano(ambayo pia husababisha tetemeko la Ardhi) milima Kama mlima Kilimanjaro ungekuwepo?
Visiwa vingekuwepo?
Hii Dunia kuna michakato inaendelea kama vile mwilini mwako mifumo ya mwili unavyofanya kazi.
Sasa Kwa vile hujui ukisemacho, basi tunasema sio kosa lako.
Ila elewa kila kinachotokea kwenye Dunia kinafanya kazi Fulani ambayo ni muhimu katika mustakabali wa Ulimwengu.
Unataka kunambia watu wa kale walikuwa wanajua kabisa kwamba tetemeko linatokeaje?
Naona umeanza Ad hominem argument, unaatack mtu ili tu kuharibu attention.
Hujui nimesoma hadi level gani ama nina uwezo gani wa uelewa. Lakini unaniatack
Sawa
Unaelewa kuwa mimi sizungumzii kiwa matetemeko hayakuwepo zamani?
Unaelewa kuwa nazungumzia hii elimu (knowledge) ya geography kuhusu hayo matetemeko na kuanalyse sehemu zenye mabonde ya ufa na athari zake hizo kama uwezekano wa matetemeko kwenye maeneo hayo kiwa haikuwepo zamani na hivyo elimu/ujuzi huu (geography) imekuja baada ya maendeleo ya science na technology?
Unaelewa kuwa mimi nakuhoji kama hao watu wa kale waliojikuta tu wamezaliwa katika maeneo hayo, kwanini Mungu hakuwaepusha na majanga kama hayo?
Unasemaje kuwa walichagua.
Na hata kama ukisema Mungu aliumba hayo maeneo kwa ajili ya hiyo michakato kama unavyodai kwanini hakudesign kerbs ama kingo kwa ajili ya kuzuia mtu asiingie kuishi maeneo kama hayo?
Iweje wakandarasi wajenge barabara milimani waweke kingo kwenye mipaka ya barabara halafu mungu huyu kashindwa kuweka hata utepe kama wa kipolisi kuonesha kuwa maeneo kama hayo yenye bonde la ufa, maeneo haya yenye uwezekano wa kutokewa Tsunami?
Huyo Mungu si wa upendo kama msemavyo,
Huyo Mungu hayupo.
Nijibu kuhusu vimondo vinavyodondoka na kuumiza watu na mali zao then husianisha na kwamba kifo ni maamuzi au michakato ya dunia.