Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 13,149
- 6,994
Ni sawa na kusema,nimejikuta nimezaliwa,na nimekuwa nisifanye kazi yoyote,nisubiri kulishwa itakuwa ni ujinga huo.Shetani sie tumemkuta, kosa letu liko wapi? Mungu amuondoe kama anaweza.
Huyo shetani,ni wewe mwenyewe unamfuata,uifuate gari ikugonge,uumie,halafu useme gari ziondolewa barabarani,wakati hizo zinamanufaa.
Shetani ni mtihani,kama mtihani wa shule,chuo,kazini na kwingineko,ili ufauli mtihani upate malipo mazuri,ukifeli mtihani shule,chuo ndio umeanguka kimasomo,ukifeli interview hupati kazi,utalaumu Mwalimu?.Na katika maisha hivyo hivyo,shetan ni mtihani,ukimfuata utaanguka kimaisha.Acha kumfuata shetani,unakwenda zini bila ndoa,unapata mtoo,unamlaunu Mungu,wakati umekwenda mwenyewe kufanya tendo lililokatazwa na Mungu.Unakwenda kunywa pombe,Unapata ajali,unamlaumu Mungu ,wakati ulishakatazwa na Mungu usilewe.