Kwanini watu wanapata shida na dhiki duniani, Mungu hana huruma?

Kwanini watu wanapata shida na dhiki duniani, Mungu hana huruma?

Dah! [emoji848]
Nimejikuta nalia[emoji24] [emoji24] [emoji24]
Jamaa Amenitonesha kidonda kilichoanza kupona
Namemkumbuka mama yangu mlezi alivyokuwa akinisimulia jinsi alivyo niokoa mikononi mwa Mbwa waliokuwa wakiliburuza Box lililokuwa limebeba mwili wa mtoto mchanga, sauti ya mtoto kutoka ndani ya Box hilo ndio iliyomfanya mama huyo kushituka na kuomba msaada kwa wapita njia kuwafukuza hao Mbwa kisha walifungua lile Box wakamuokoa Mtoto ambaye Ndiye Mimi[emoji24][emoji24]
HATA IWAJE KWANGU MUNGU BADO NI BABA
ANAFANYA KILA KITU KWA MAPENZI YAKE, YEYE ANATOA NA YEYE ANATWAA, YEYE ANAPANGA UZALIWE KWA FAMILIA GANI, YEYE ANAANDAA ULELEWE WAPI.
MUNGU MKUU HANA BAYA
Je hadithi hiyo inauhusiano gani na uwepo wa Mungu?
 
Ana utajiri usiokwisha,,,,,

Hiyo statement ndio inamwelezea Mungu vyema,
Kama utajiri unaoujua wewe unaisha ujue sio huo unaomaanishwa kwenye statement hiyo, kama amani unayoijua wewe inaishia basi jua siyo hiyo inayozungumziwa,
 
Mungu yupo,na alikuwepo na atakuwepo,tatizo ni lako wewe,ni sawa uwe shule unasoma wewe unakuwa wa mwisho ,wakati wenzako wanakuwa kwenye kumi bora,halafu ulaumu kuwa shule haina waalimu,wakati ni uzembe wako wewe mwanafunzi,unacheza mwisho wenzako wanatoka na Div One,wewe unatoka na Ziro,halafu wasema shule ile haina waalimu.
Hujaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Fuatilia mtiririko huu,
Yaani watu wanaona mfano mtu akiwa na ulemavu fulani basi kalaaniwa au ana madhambi kumbe hamna

Sometimes nature tu na hitilafu miili ni ya nyama hii

Kama jibu ni nature na hitilafu sawa ✅

Lakini ni udhihirisho mwingine kuonesha kuwa Mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na mwenye upendo wote hayupo na wala hawezekani kuwepo.

Angekuwepo hizo hitilafu za maumbile tusingeziona
Sasa kwa mtirirko huu uliouvamia na maelezo ya wanafunzi shuleni nashindwa kukuelewa.

Umejibu mtiririko usiouelewa,
Hivyo sijakuelewa.

Unaweza thibitisha Mungu yupo?
 
Ana utajiri usiokwisha,,,,,

Hiyo statement ndio inamwelezea Mungu vyema,
Kama utajiri unaoujua wewe unaisha ujue sio huo unaomaanishwa kwenye statement hiyo, kama amani unayoijua wewe inaishia basi jua siyo hiyo inayozungumziwa,
Alfu lela ulela
 
Ni sawa na kusema,nimejikuta nimezaliwa,na nimekuwa nisifanye kazi yoyote,nisubiri kulishwa itakuwa ni ujinga huo.
Huyo shetani,ni wewe mwenyewe unamfuata,uifuate gari ikugonge,uumie,halafu useme gari ziondolewa barabarani,wakati hizo zinamanufaa.
Shetani ni mtihani,kama mtihani wa shule,chuo,kazini na kwingineko,ili ufauli mtihani upate malipo mazuri,ukifeli mtihani shule,chuo ndio umeanguka kimasomo,ukifeli interview hupati kazi,utalaumu Mwalimu?.Na katika maisha hivyo hivyo,shetan ni mtihani,ukimfuata utaanguka kimaisha.Acha kumfuata shetani,unakwenda zini bila ndoa,unapata mtoo,unamlaunu Mungu,wakati umekwenda mwenyewe kufanya tendo lililokatazwa na Mungu.Unakwenda kunywa pombe,Unapata ajali,unamlaumu Mungu ,wakati ulishakatazwa na Mungu usilewe.
Umesema shetani ni mtihani?
Unamaanisha nini
 
Kaka wewe unataka uchakate mbususu ,ukitoka kwenda kazi Hela inamwagika ,mvua ikunyeshee kwa muda ,usiibiwe ,usirogwe na kadhalika ,Yaani mteremko ndo ujue mungu yupo kazi full time ,anakupigania ???[emoji23][emoji23][emoji23]namshukuru mungu kwa mapito na mateso yote aliyoruhusu nipate .,Kuna mengi nlijifunza from them .
Ulipo unavuta hewa Bure ,usalama unao ,mlo Leo umepata ,jua kesho unauhakika lazima lichomoze na litue ,una ardhi na nguvu mpaka simu yakumtusi ukisema hajiwezi ...
Jifunze kushkuru ,utajiri ni bidii yako mwenyewe , au wataka akuletee maburubgutu ya dola uamke pap don ???[emoji23][emoji23][emoji23]
Muulize tajiri yyte analalaje usiku ,atavuta pumzi ndefu ndo akujibu .
Sijui lini nlilala nkashiba usingizi na Hela amenibariki nayo
 
Narudia kukujibu,Mungu uokoa walio wake.Iman haithibitishwi kwa macho tu,si Kila alitajale jina la Mungu au aingiaye kanisan anamuabudu Mungu pia Sio yote makanisa ni ya Mungu inakuhitaji macho ya rohoni kuyatofautisha kupitia maandiko.
 
Huyo Mungu unayemtetea hapa hayupo kwenye uhalisia, labda kama tu unabisha.

Kwasababu kama kweli angekuwepo na anauwezo wa kujua ya baadae kwa kile kiumbe amekitengeneza mwenyewe asingeweza kumuumba shetani kama kitabu chako kinavyokufunza.

Mungu mjuzi wa yote, Mungu muweza wa yote na mwenye upendo wote inawezekana vipi akaumba ulimwengu huu tunaouona wenye mabaya kuwezekana?
Nikuulize swali?!

Unaweza kunambia kitu gani ambacho mwanadamu anaweza kukiongelea na hakipo kabisa.....?! Yaani hata idea yake hakipo kama vile mwaka 1920 ukizungumiza iPhone 14 pro max nani angekuelewa na ungeilezea vipi kwa watu bila kukuona mwehu na haueleweki?!

Je, unaweza nambia sasa ni kitu gani ambacho mwanadamu anaweza kukiongelea na hakipo kabisa popote pale?
 
Zaidi ya 99.2% ya watu wote hawachagui kifo

Wanachagua wale wanaojiua wenyewe, either kwa kujinyonga or kunywa sumu etc, hakuna anayependa kufa.

99.2 ya vifo vyote si maamuzi wala chaguzi za watu, mtu kupata ajali si uchaguzi wake,

Mtoto akifa naye unasema kachagua?

Inaonekana hatuelewani kwasababu hauelewi nini maana ya kuchagua na kuamua.

Unaelewa nini maana ya kuamua?
Unaweza kuvuka highway huku unachezea simu ukitembea taratibu?!
 
Nikuulize swali?!

Unaweza kunambia kitu gani ambacho mwanadamu anaweza kukiongelea na hakipo kabisa.....?! Yaani hata idea yake hakipo kama vile mwaka 1920 ukizungumiza iPhone 14 pro max nani angekuelewa na ungeilezea vipi kwa watu bila kukuona mwehu na haueleweki?!

Je, unaweza nambia sasa ni kitu gani ambacho mwanadamu anaweza kukiongelea na hakipo kabisa popote pale?
Tunaweza kuongelea Taa ya dhahabu ing'arayo pale juani,

Tunaweza kuongelea habari za Spiderman, James bond, Mungu, wanyonya damu wa kule primary, Ngoswe, Yajuj wa Majuj, joka la dhahabu, kuna lile lidragon litakalokwangua theluthi ya nyota zote zianguke duniani n. K
 
Nenda mlimani city pale mbona yupo[emoji23][emoji23][emoji23]
Unaelewa maana ya spiderman?
Au ukikuta kinyago chake ndiyo huyo unadhani tunamuongelea?

Anaweza kutoa web huyo?
 
Unaweza kuvuka highway huku unachezea simu ukitembea taratibu?!
Uwezekano upo, na unaweza vuka gari zikasimama tu zisikugonge.

Japo Hujajibu hoja nliyowapa hapo.

Mmesema kuwa kifo ni kuchagua.

Nmewauliza mtoto nae akifa anakuwa amechagua?
 
Back
Top Bottom