Kwanini watu wanapata shida na dhiki duniani, Mungu hana huruma?

Kwanini watu wanapata shida na dhiki duniani, Mungu hana huruma?

Mwanadamuu bhanaaa Akiwa anakulaa bataa maisha yanaendaa poaaa ndo anaona Mungu yupooo.. kikiumanaaa sasaa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] kenge kabisaa shukuruu hata Unapumuaa muda huuu maana bila Mungu ungekuwaa maiti now..!
 
Naona ni mwendo wa logical non sequitur.

Sasa kuzidiwa kulala mara kifo.. Kunathibitisha vipi uwepo wa Mungu?
Umeshaelewa.Kila linalofanyika popote,hata kama hukumuona mfanyaji ukiwa na utajua yupo aliyefnya hivi,ukiona unyao wa simba hata kama hayupo,utasema hapa kapita simba.Hutasema huu unyao umejifanya wenyewe.Utaanza kuchukuwa tahadhari,kuwa eneo hili lina simba.
Ukiingia darasani,!!ukiona ubao umeandikwa,utajua wazi yupo aliyeandika,hata kama hukumuona.
Iweje upate usingizi na uone watu wanakufa,halafu useme havina mfanyaji.Tumia akili,!!japo akili huioni,lakini utaambiwa huyu ana akili sana,ni kutokana unayofanya ya ki akili.
 
Mwanadamuu bhanaaa Akiwa anakulaa bataa maisha yanaendaa poaaa ndo anaona Mungu yupooo.. kikiumanaaa sasaa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] kenge kabisaa shukuruu hata Unapumuaa muda huuu maana bila Mungu ungekuwaa maiti now..!
Vitisho no silaha ya mwisho ya mjinga.

Unaweza kututhibitishia kuwa huyo Mungu yupo walau hata kwa kuondoa contradiction kwenye dhana ya uwepo wake?
 
Vitisho no silaha ya mwisho ya mjinga.

Unaweza kututhibitishia kuwa huyo Mungu yupo walau hata kwa kuondoa contradiction kwenye dhana ya uwepo wake?
Wewe unaamini kuna Hewa ya Oxygen??? Unaamini Kuna roho???
 
Hayo ni majina ya kilugha tu,waswahili twaita Mungu,wazungu God,wahindi Baguwan nk

Kwahyo brahma ambaye ulimwengu uliumbwa kupitia mchakato wa brahma ndoto ambaye alijipata mwenyewe paspo jitambua katika bahari isiyo na mwisho ya nirguna brahman ni Sawa na mungu aliyeumba kwa udongo? Unafahamu kwamba kuna african mythology takibrani30 zote zikiwa na stori tofauti jinsi mungu wao alivyoumba ulimwengu?

Unathibitisha vipi brahma, au titan, au zeus ni jehovah au allah? Huku wakiwa na stori tofauti?
 
It's not the issue about believe it's concrete evidence that needed to support your claims god exist?
Huwezi thibitisha mungu yupo sababu hayupo
Ila unaweza thibitisha kuna uchawiii...kuna rohoo...[emoji28][emoji28]
 
Umeshaelewa.Kila linalofanyika popote,hata kama hukumuona mfanyaji ukiwa na utajua yupo aliyefnya hivi,ukiona unyao wa simba hata kama hayupo,utasema hapa kapita simba.Hutasema huu unyao umejifanya wenyewe.Utaanza kuchukuwa tahadhari,kuwa eneo hili lina simba.
Ukiingia darasani,!!ukiona ubao umeandikwa,utajua wazi yupo aliyeandika,hata kama hukumuona.
Iweje upate usingizi na uone watu wanakufa,halafu useme havina mfanyaji.Tumia akili,!!japo akili huioni,lakini utaambiwa huyu ana akili sana,ni kutokana unayofanya ya ki akili.
Ngoja nikupe kisa kimoja.

Almasi ni aina ya madini yanayopatikana zaidi sehem moja inaitwa Mwadui_kishapu _Shinyanga.

Kuna migodi kadhaa, ukiwemo mmoja maarufu unaenda na jina la kampuni ya Williamson Diamonds limited.

Hapo awali kabla ya uhuru, almasi ilikuwa inapatikana juu tu kama mawe na wazee wa pale mwadui walikuwa wakichezea bao kama mawe.
Hivyo almasi ilikuwa ya kuokota.

Mpaka alivyokuja mzungu (Williamson) kuzichukua hadi kuanza kufanya uchimbaji.

Kwasasa almasi haipatikani juu tena, ni uchimbaji wa mashimo marefu sana.

Kupitia historia hii

Ukamkuta mzee aliyekuwa amepoteza fahamu kipindi wanachezea almasi kwenye bao amezinduka leo, na katika kuzinduka huko akaja na almasi zake alizokuwa ameziacha kwenye chumba chake.

Na akakwambia kuwa aliziokota, utakataa umlazimishe kuwa ni lazima ziwe zimechimbwa kisa wewe unadhani kuwa ni lazima ziwe zimechimbwa kwasababu umelazimishwa na mawazo yako kuamini ni lazima kama unavyoona muda huo?

Nnachokwambia wewe ni kwamba, unataka kulazimisha Uende kama mawazo yako yalivyo.

Cha kukuongezea ni kwamba:

Hata zamani ilikuwa ni inajulikana kuwa jua ndo linazunguka dunia na dunia ndiyo center ya universe.
Hapo usingeweza kumwambia mtu kitu akakuelewa kama ulivyo wewe na imani kuwa ni lazima kuwepo na kilichotengeneza ulimwengu.

Ni mawazo hayo hayo watu walitumia kulazimisha kuwa dunia ni flat, na ilichukua muda mpaka watu wakafanya proof kujua kuwa dunia sio flat, bali ni umbo tufe.
Hapo pia usingeweza kumwambia mtu tofauti akakuelewa kama ulivyo wewe na imani kuwa ni lazima kuwepo na kilichotengeneza ulimwengu.

Kwasababu hapo watu walikuwa na anthropic bias katika kutafsiri na kulazimisha mambo yawe ni lazima kama wanavyoona muda huo.

Sasa hiyo anthropic bias ndio hii hii unayoilazimisha wewe hapa uitumie.

Ukiambiwa uthibitishe uwepo wa Mungu huwezi na umeshindwa umebaki na mawazo haya haya ya kulazimisha kadri wewe unavyoweza kuona.

Nijibu hapa.

Kama kila tukionacho kina aliyetengeneza, huyo Mungu yeyee alitengenezwa na nani?
 
Ila unaweza thibitisha kuna uchawiii...kuna rohoo...[emoji28][emoji28]
You trying to twist the topic
Nionyeshe niliposema naweza thibitisha uchawi upo au roho ipo?
Hakuna mungu wala shetani ni stori za kutungwa, kama vile unicorn au hippogriff nikikwambia nimekutana na fire breathing dragon leo utakubali pasi ushahidi??
 
Wewe unaamini kuna Hewa ya Oxygen??? Unaamini Kuna roho???
Hapana, siamini kuna hewa ya oxygen.

Ila nnajua kuwa kuna hewa ya oxygen.

Hapa kuna sifa za hewa ya oksijeni (O2):
  1. Rangi na Harufu: Gesi ya oksijeni ni isiyo na rangi na haina harufu. Inapatikana katika hali ya gesi katika mazingira ya kawaida.
  2. Ugumu na Kuyeyuka: Oksijeni ina kiwango cha kuyeyuka cha -218.79 °C (-361.82 °F) na kiwango cha kuganda cha -222.65 °C (-368.77 °F). Katika hali ya gesi, ina uwezo wa kuyeyuka na kuganda katika joto la chini sana.
  3. Uwiano wa Masi: Masi ya atomi mbili za oksijeni hufanya gesi ya oksijeni (O2). Kila atomi ya oksijeni ina uzani wa atomi 16 au ni mara kumi na sita zaidi kuliko atomi ya hidrojeni.
  4. Inategemea Kemia: Oksijeni ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 8 katika Jedwali la Masi. Ina elektroni 6 za valensi, ikimaanisha kuwa inahitaji elektroni 2 zaidi kufikia hali thabiti.
  5. Kiwango cha Kuchomwa: Oksijeni inachukuliwa kama mhimili wa kuchochea moto. Inasaidia kuchochea na kuongeza kiwango cha mwako wa vitu vingine. Ina uwezo wa kuchochea moto na kuwasha vitu vinavyohitaji oksijeni kwa kuchoma, kama vile kuni, mafuta, na wanga.
  6. Kazi katika Upumuaji: Oksijeni ni muhimu katika michakato ya kupumua kwa viumbe hai. Wakati tunavuta oksijeni, inapita kupitia mfumo wa upumuaji na kufikishwa kwenye mapafu, ambapo inachukuliwa na seli nyekundu za damu na kusambazwa mwilini ili kuongeza michakato ya kuzalisha nishati kwa seli.
  7. Utumiaji katika Huduma za Afya: Gesi ya oksijeni hutumiwa sana katika huduma za afya. Inapatikana katika matanki ya oksijeni na hutumiwa kutoa tiba ya oksijeni kwa wagonjwa ambao wana upungufu wa oksijeni au matatizo ya kupumua.
  8. Utumiaji Viwandani: Oksijeni hutumiwa katika viwanda mbalimbali, kama vile tasnia ya chuma na madini, tasnia ya kemikali, na utengenezaji wa glasi. Inaweza kutumika kama gesi ya kulisha katika mchakato wa kuchoma na kuongeza kiwango cha mwako wa vitu vingine
Unaweza kuthibitisha na kuchunguza zaidi sifa hizo na uwepo wa hewa hiyo
Kupitia Uchunguzi wa Kimaabara

Unaweza kuchukua sampuli ya hewa inayofaa kwa uchunguzi zaidi. Unaweza kutumia vifaa kama vile spektrometa ya infra-redi (IR) au chromatography ya gesi (GC) ili kutambua uwepo wa oksijeni na viwango vyake katika sampuli ya hewa.
♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️♦️

Siamini kama kuna roho
Unaweza thibitisha kama roho ipo?
 
Hayo ni majina ya kilugha tu,waswahili twaita Mungu,wazungu God,wahindi Baguwan nk
Wewe sehemu nyingi wanalimungu lao la kujitungia.

Tena wengine wana Mamungu mengi zaidi ya 20,

Wewe unao wangapi?
 
Kuamini kwetu au kutokuamini kwetu hakibadilishi kitu. Mungu anabaki kua ni Mungu. Uwepo wako au kutokuwepo kwetu hakimshughulishi. Kikubwa Ukimtii na kumsikia atakubariki mwilini na rohoni.
Toka hapa na Mungu wko wa mchongo,,,
 
Kile kilichofanya chanzo cha maisha ya binafamu...na viumbe vyote vilivo hai..na visivyo hai...basi hicho ndo MUNGU
 
Mkuu umeandika mambo mengi sana kujaribu kumnasua Mungu wako ambae hayupo, na hawezi kujinasua kwenye hii mitego.

Hyo elimu unayoisema ni zao la baadae sana baada ya watu kujifunza kuhusu matetemeko,

Je kabla ya elimu hii ya tetemeko kwanini Mungu hakuwajulisha kwa kuwapa allert msiishi maeneo hayo?

Na kama anaupendo wote kwanini ameweka tetemeko, tetemeko ni la kazi gani yeye sasa kuliweka?


Hapo ni unajitetea tu, na hoja yako haina mashiko.
Kama mungu ameyaumba yote hayo, kwanini hajawapa nauli watu wahame wasiishi hayo maeneo yenye matetemeko kama unavyodai.

Huoni wale watoto wasio ma uwezo wa kujiamlia kuhama maeneo hayo, wakikumbwa na matetemeko utasema wamechagua?
Watoto walichagua kuzaliwa hayo maeneo.

Sijakuelewa na hoja yako haina mashiko.

Sasa nijibu hapa chini nikubali kama kweli mabaya ni uchaguzi, 👇👇

Vipo visa vya vimondo kuua watu ni pamoja na tukio la meteoriti lililotokea mnamo mwaka 2013 huko Chelyabinsk, Urusi. Kimondo kilichoingia angani kilipasuka juu ya mji huo, kusababisha vioo vingi kuvunjika na watu wengi kujeruhiwa kutokana na vipande vya vioo.

Moja ya visa maarufu ni lile la Tunguska huko Siberia, Urusi mnamo tarehe 30 Juni 1908. Kimondo kikubwa sana kilipasuka angani na kusababisha mlipuko mkubwa,

Je hapa unasemaje kuhusu dhana yako ya uchaguzi?
Yaani wewe unataka Mungu akufanyie kila kitu kama mtoto mchanga,vip na hyo akili amekupatia ya kazi gani sasa? Wewe siyo Roboti
 
Kuna watoto wanateseka kutokana na uovu ambao wazazi wao walifanya...

Kutoka 20: 5

Biblia inasema nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi chaa tatu na cha nne...
Unasahau kuwa hiyo hiyo bible inasema kuwa "mwana hatoubeba mzigo wa babaye wala baba hatoubeba mzigo wa mwanae''.

kiufupi hayo mambo ya kurithi maovu ya watu waliopita kibiblia ni uongo mybe kwa kulogwa, kibiblia ni uzushi tu, mnaponukuu vifungu vya biblia muwe mnajuwa kuvitetea na mujue vinamaanisha nini,

Kila linalotokea dunian ni matokeo ya athari za maisha ya binadamu huyo Mungu hausiki.

Magonjwa, vita, njaa, majanga ya asili+yasiyo ya asili ni matokeo ya maisha ya mwanadamu baada ya kwenda kinyume na Mfumo wa asili ya maisha inavyotakiwa kuwa.

Unapokata miti unategemea ukame utakuacha?(majanga)

Unapowachonganisha ndugu, ama jamii zinapotofautiana na kukakasirikiana unategemea hawatopigana na kuuwawa ama kufarakana?(vita)

Unapoachana na mifumo asili ya ulaji na kukumbatia masumu na makemikali unategemea magonjwa, madhaifu ya mwili na kupata vizazi vyenye watoto wadhaifu unategemea hili jambo likuache?(Magonja+madhaifu)

Kiufupi huyo Mungu alipomuumba binadamu na kumpa akili(UWEZO) alimalizana nae akimaanisha lolote atakalolifanya kutokana na akili yake litamletea matokeo HASI au CHANYA na matokeo yatampata na akihitaji msaada ni kuurudia mfumo aliowekewa anaotakiwa kuufuata.

Mnamlaumu Mungu bure hata kama yupo au hayupo wakulaumiwa by 90% ni binadamu wenyewe maana wao ndio chanzo cha matatizo.

Hata mzaz anapomfundisha mtoto akawa hasikii basi huadhibiwa ama huachwa ili apate matokeo ya kile akifanyacho kimfunze, ama anaachwa afunzwe na ulimwengu.

Matatizo yatupatayo by90% ni matokeo ya ujinga wetu, upumbavu wetu na ushenzi wetu wa kutotumia akili na kufuata mfumo wa maisha wa asili.

Asili ndio kila kitu hakuna kumsingizia shetan wala Mungu, binadamu ndie chanzo cha matatizo.

Tuamke, mambo ya dini ni upuuzi wa kumchelewesha mtu kufikili mambo ya msingi ya kuujenga ulimwengu na kupambana na changamoto.
 
Back
Top Bottom