bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Bustani ya Eden ilikua Duniani watafiti na wachimbuzi wa maandiko wanathibitisha ilikua nchini Iraq,baada ya Mwanadamu kutenda dhambi akafukuzwa Bustani yaani ndani ya uzio akaletwa Duniani ambapo tayari Duniani shetani na malaika zake tayari walikuwepo Duniani baada ya kufukuzwa mbinguni.Mkuu sijajua unaposema bustani ya eden unamaanisha ilikuwa wapi.
Je haikuwa duniani?
Halafu kama aliumba ulimwengu ukaenda tofauti na alivyotamani (kwamaana aliumba ulimwengu ikawezekana watu kuzingua kisha akaamua kuwafukuza, means wasingezingua asingewafukuza,
the whole storyline tuliyonayo tusingekuwa nayo)
Sasa huoni kama huyu Mungu pia anajipinga kuwa si mjuzi wa yote?Hiyo mbingu ambayo ameiandaa (kwamujibu wako)
unauhakika gani kwamba itakuwa ya raha, amani furaha na isiwe na mabaya kuja kuanza tena?Hujawaza kuwa inawezekana kwa watu kuzingua tena huko huko na tukawa kwenye ulimwengu kama huu huu na uovu ukatokea mbinguni?
Hoja kuu ni kuwa, Huyu Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kwanini kaumba huo ulimwengu wenye uwezekano wa mwanadamu kuzingua?
Naona hatuelewani hujawaza kwa upana dhana hii, Embu pitia mfano huu :
Wewe (Mungu) umejenga nyumba yako na kudesign robot lako(mwanadam) , programming umefanya mwenyewe kwa ujuzi wako (unajua kila kitu kuhusu kutengeneza roboti na kujenga nyumba ) ili liwe linaenda kuchota maji ya kunywa na kukuletea chumbani,
chumba hicho umekijenga mwenyewe then uli_run lisikupe matokeo (lizingue) uliyoyatarajia,
likawa linatembea linafika linakuta mlangoni ni mwembamba linashindwa kuingia,
halafu hapo hapo bado liwe linakosea kuulenga mlango vizuri, liwe linalenga mlango nusu ya kulia, nusu ya kushoto linalenga ukuta hata kulenga center ya mlango linashindwa kwasababu ya programu uliyoliwekea wewe mwenyewe halafu ulitupe likajifanyie matengenezo ya programu yake ili lije kukuletea maji.
wakati uwezo unao wote
(uliweza kuliumbia mazingira {ulimwengu} ambayo hayaruhusu kuzingua, yaani ile nyumba na njia ya roboti wako kufika chumbani. ulikuwa na uwezo wa kujenga mlango mpana zaidi ama kutengeneza robot 🤖 mwembamba zaidi aweze kufit mlango huo ili liwe linaingia chumbani kirahisi tu, lakini hukufanya hivyo
Una ujuzi wote
(ulikuwa na uwezo wa kufanya best programing na ikakupa matokeo uliyotaka na lisiwezekane kugonga nusu ya kushoto kwenye ukuta, sasa bado pamoja na kuwa na ujuzi wa kujua kila kitu ulikosea programing likawa haliwezi kuulenga ule mwembamba kwa 100% likawa halilengi mlango vizuri kana kwamba hata kama ungekuwa mlango ni mpana bado lilikuwa haliwezi kuulenga vizuri hivyo lingejikwaa upande na Lingeshindwa kuingia chumbani
Eti ulitupe likajitengeneze jenyewe
halafu bado useme wewe unalipenda sana na unajinasibu unaupendo wote kabisa.
- Kwanini mlango wa chumba ulichojenga wewe mwenyewe kwa kuweka mlango ulio mwembamba kuzidi robot 🤖, umelisababishia lisiweze kupita?
- Kwanini umeliprogram vibaya lilenge obstacle na usababishe maji chumbani kwako lisiyafikishe?
Halafu ukasirike ulitupe likajitengeneze
WTF!!!
Mwanadamu Duniani yupo kwa ajili ya kufanya matengenezo kwa kupewa free will atachagua wapi awe baada ya ukomo wa maisha ya dunia.
Wema wataishi milele paradise na waovu na shetani wataishi jehanamu milele.