Kwanini watu wanapata shida na dhiki duniani, Mungu hana huruma?

Mkuu sijajua unaposema bustani ya eden unamaanisha ilikuwa wapi.
Je haikuwa duniani?​

Halafu kama aliumba ulimwengu ukaenda tofauti na alivyotamani (kwamaana aliumba ulimwengu ikawezekana watu kuzingua kisha akaamua kuwafukuza, means wasingezingua asingewafukuza,
the whole storyline tuliyonayo tusingekuwa nayo)
Sasa huoni kama huyu Mungu pia anajipinga kuwa si mjuzi wa yote?​
Hiyo mbingu ambayo ameiandaa (kwamujibu wako)
unauhakika gani kwamba itakuwa ya raha, amani furaha na isiwe na mabaya kuja kuanza tena?​
Hujawaza kuwa inawezekana kwa watu kuzingua tena huko huko na tukawa kwenye ulimwengu kama huu huu na uovu ukatokea mbinguni?​

Hoja kuu ni kuwa, Huyu Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kwanini kaumba huo ulimwengu wenye uwezekano wa mwanadamu kuzingua?
Naona hatuelewani hujawaza kwa upana dhana hii, Embu pitia mfano huu :

Wewe (Mungu) umejenga nyumba yako na kudesign robot lako(mwanadam) , programming umefanya mwenyewe kwa ujuzi wako (unajua kila kitu kuhusu kutengeneza roboti na kujenga nyumba ) ili liwe linaenda kuchota maji ya kunywa na kukuletea chumbani,

chumba hicho umekijenga mwenyewe then uli_run lisikupe matokeo (lizingue) uliyoyatarajia,

likawa linatembea linafika linakuta mlangoni ni mwembamba linashindwa kuingia,

halafu hapo hapo bado liwe linakosea kuulenga mlango vizuri, liwe linalenga mlango nusu ya kulia, nusu ya kushoto linalenga ukuta hata kulenga center ya mlango linashindwa kwasababu ya programu uliyoliwekea wewe mwenyewe halafu ulitupe likajifanyie matengenezo ya programu yake ili lije kukuletea maji.

wakati uwezo unao wote
(uliweza kuliumbia mazingira {ulimwengu} ambayo hayaruhusu kuzingua, yaani ile nyumba na njia ya roboti wako kufika chumbani. ulikuwa na uwezo wa kujenga mlango mpana zaidi ama kutengeneza robot 🤖 mwembamba zaidi aweze kufit mlango huo ili liwe linaingia chumbani kirahisi tu, lakini hukufanya hivyo

Una ujuzi wote
(ulikuwa na uwezo wa kufanya best programing na ikakupa matokeo uliyotaka na lisiwezekane kugonga nusu ya kushoto kwenye ukuta, sasa bado pamoja na kuwa na ujuzi wa kujua kila kitu ulikosea programing likawa haliwezi kuulenga ule mwembamba kwa 100% likawa halilengi mlango vizuri kana kwamba hata kama ungekuwa mlango ni mpana bado lilikuwa haliwezi kuulenga vizuri hivyo lingejikwaa upande na Lingeshindwa kuingia chumbani

Eti ulitupe likajitengeneze jenyewe
halafu bado useme wewe unalipenda sana na unajinasibu unaupendo wote kabisa.

  • Kwanini mlango wa chumba ulichojenga wewe mwenyewe kwa kuweka mlango ulio mwembamba kuzidi robot 🤖, umelisababishia lisiweze kupita?
  • Kwanini umeliprogram vibaya lilenge obstacle na usababishe maji chumbani kwako lisiyafikishe?

Halafu ukasirike ulitupe likajitengeneze

WTF!!!​
Bustani ya Eden ilikua Duniani watafiti na wachimbuzi wa maandiko wanathibitisha ilikua nchini Iraq,baada ya Mwanadamu kutenda dhambi akafukuzwa Bustani yaani ndani ya uzio akaletwa Duniani ambapo tayari Duniani shetani na malaika zake tayari walikuwepo Duniani baada ya kufukuzwa mbinguni.
Mwanadamu Duniani yupo kwa ajili ya kufanya matengenezo kwa kupewa free will atachagua wapi awe baada ya ukomo wa maisha ya dunia.
Wema wataishi milele paradise na waovu na shetani wataishi jehanamu milele.
 
Mwanadamu aliumbwa na Mungu kwa kutumia udongo kama sanamu kisha akaulizia pumzi akaipa uhai.
Unaweza kunithibitishia hayo madai yako.

Back to 1²
Thibitisha huyo Mungu basi kama yupo!?

roho na nafsi uchukua mwili mwingine na kwenda ulimwengu mwingine.
Unaweza kuthibitisha hiyo roho kama ipo?

Thus mwanadamu ana husiana na udongo kupitia vyakula vipandavyo udongoni ili tupate asili yetu yaan madini na virutubisho toka udongoni,thus mwanadamu akifika ukomo yaan miaka ya kibiblia kuanzia 70 asizidi 120 ni lazima afe.Aoze mwili udongoni
Inaonekana huelew mchakato mpaka kuoza unatokea vipi.
♦️ 1. Unajua kwanini mwili huwa unaoza.?

Unaposema lazima mwili ufe uoze ukiwa udongoni,

♦️ 2. Kwani mtu hawezi kuoza akiwa hayuko udongoni?

Na kama kuoza kwa miili ya binadamu ndiyo uthibitisho wako kuwa mtu kaumbwa kwa udogo,

♦️ 3. kwanini skeleton kila siku inafukuliwa inakutwa haijaoza.?
Au material ya mifupa hayakuwa udongo?
 
Unaweza kunithibitishia hayo madai yako.

Back to 1²
Thibitisha huyo Mungu basi kama yupo!?

Unaweza kuthibitisha hiyo roho kama ipo?

Inaonekana huelew mchakato mpaka kuoza unatokea vipi.
♦️ 1. Unajua kwanini mwili huwa unaoza.?

Unaposema lazima mwili ufe uoze ukiwa udongoni,

♦️ 2. Kwani mtu hawezi kuoza akiwa hayuko udongoni?

Na kama kuoza kwa miili ya binadamu ndiyo uthibitisho wako kuwa mtu kaumbwa kwa udogo,

♦️ 3. kwanini skeleton kila siku inafukuliwa inakutwa haijaoza.?
Au material ya mifupa hayakuwa udongo?
Kila kiungo kina muda wa kuoza.
Thibitisha wewe Mungu hayupo
Nini uupa nguvu mwili
Ukijibu haya umepata majibu ya maswali yako
 
baada ya Mwanadamu kutenda dhambi akafukuzwa Bustani yaani ndani ya uzio akaletwa Duniani ambapo tayari Duniani shetani na malaika zake tayari walikuwepo Duniani baada ya kufukuzwa mbinguni.
Kwani kwenye hiyo bustani (uzio) mwanadamu alitenda dhambi gani, hyo dhambi ilianzaje anzaje mkuu, embu nifunze nipate kitu kipya (kwa mujibu wako wewe unavyojua)
 
Dhambi ilikuja baada ya kukiuka maagizo ya Mungu,alipoambiwa asile tunda la mti wa katikati yeye akala baada ya kupotoshwa na shetani
 
Kila kiungo kina muda wa kuoza.
Thibitisha wewe Mungu hayupo
Nini uupa nguvu mwili
Ukijibu haya umepata majibu ya maswali yako
Kwanza hujanijibu swali langu la pili hapo.
Ngependezwa unijibu.

1♦️Kisichopo hakithibitishiki kuwa hakipo.
Ila naweza kukuonesha kwa udhihirisho mzuri tu kuwa hakipo.

Katika kutambua uwepo wa vitu, viumbe hai hutumia mifumo yao ya utambuzi kama msingi wa kwanza kuthibitisha vilivyopo.

1.Mungu sijawahi kumuona.
2.sijawahi kumlamba
3. sijawahi kumnusa
4. sijawahi kumsikia
5. sijawahi kumhisi

Hivyo kuhusu mifumo ya fahamu hapo juu katika kutambua uwepo wa kitu, Mungu hajatambulika.

Lakini pia tunaweza kujaribu kutumia njia za vipimo ili kutambua uwepo wake.
Katika hili pia Mungu hayupo hawezi kupimwa popote pale.

Hata ukishika science tu, utaona Mungu wako huyu anaekutaka ukamwabudu hayupo na hana uwezekano wa kuwepo.
Ukipitia vitabu vinavyodaiwa alivitunga yeye ukacompare na science ya anga jinsi mambo yalivyo katika uhalisia unaona kabisa Mungu muweza wa yote, Mungu mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.

Udhihirisho ambao ni mkubwa zaidi ambao hauna chenga chenga ni kuhusu dhana ya uwepo wake kuingia kwenye mzani wa mantiki

Kwa kutumia Proof by logical consistency, Dhana ya uwepo wa Mungu inacontradiction kubwa sana ambayo hata wewe hujaweza kuitatua.

Hivyo huo ni udhihirisho mwingine kuwa Mungu huyo hayupo na wala hana uwezekano wa kuwepo.

2 ♦️kinachoupa mwili nguvu

kuna njia kadhaa ambazo huupa mwili Nguvu kuna michakato mingi na mifumo ya mwili. Hapa kuna vyanzo muhimu cha nguvu za viumbe hai:
  1. Metaboliki: Nguvu za viumbe hai zinategemea uwezo wa kubadilisha nishati ya kemikali inayopatikana kutoka kwenye chakula na kuifanya kuwa nishati ya kimetaboliki. Katika michakato ya metabolic, sukari na mafuta huvunjwa kuwa adenosine triphosphate (ATP), ambayo ni chanzo kikuu cha nishati ya seli. ATP hutoa nguvu inayotumiwa na seli za mwili kutekeleza kazi zake, kuanzia kazi za msingi za kimetaboliki hadi shughuli za kimwili na kiakili.
  2. Mfumo wa upumuaji: Nguvu za viumbe hai zinahitaji oksijeni ili kutokea. Mfumo wa upumuaji una jukumu muhimu katika kusambaza oksijeni kwa tishu zote za mwili. Wakati wa kupumua, hewa yenye oksijeni huingia kwenye mapafu na oksijeni hiyo huvuka kwenye kuta za mapafu na kuingia kwenye mfumo wa damu. Hapo ndipo oksijeni inakusanywa na seli za mwili kwa ajili ya kutengeneza ATP kupitia michakato ya kemia ya seli

Unafahamu respiration?
 
Dhambi ilikuja baada ya kukiuka maagizo ya Mungu,alipoambiwa asile tunda la mti wa katikati yeye akala baada ya kupotoshwa na shetani
Kumbe shetani alikuwapo ndani ya huo uzio.

Sasa hapa ulikuwa unajenga hoja gani hii mbona haina maana tena.
baada ya Mwanadamu kutenda dhambi akafukuzwa Bustani yaani ndani ya uzio akaletwa Duniani ambapo tayari Duniani shetani na malaika zake tayari walikuwepo Duniani
Au bustanini sio duniani ambamo pia shetani alikuwamo humo humo kwenye uzio.

Huo uzio ulikuwa wa nini, kumkinga na nini.

Kwanini Mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na mwenye upendo wote amtupe mwanaye kwa huyo shetani ili ateseke?

Huyo shetani kwanini asingepelekwa hata sayari nyingine huko?

Mwanadamu Duniani yupo kwa ajili ya kufanya matengenezo kwa kupewa free will atachagua wapi awe baada ya ukomo wa maisha ya dunia.
Wema wataishi milele paradise na waovu na shetani wataishi jehanamu milele
Mkuu unaelewa jehanam ni nini, ama ni wapi?
 
Dhambi ilikuja baada ya kukiuka maagizo ya Mungu,alipoambiwa asile tunda la mti wa katikati yeye akala baada ya kupotoshwa na shetani
Unaweza kubatilisha madai yangu kuwa unachonambia hapa ni hadithi za kutungwa na watu na hazina uhalisia wowote?
 
Evolution of man ni andiko la binadamu, sawa au sio sawa? Tafiti zake una kiwango gani cha usahihi hata niwe na hoja madhubuti za kukana uwepo wa mungu?
Mkuu kwanza naomba nkuhakikishie kuwa maandishi yote ni ya mwanadamu.

Kwahyo ni sawa evolution ni andiko la mwanadamu, biblia ni andiko la mwanadamu, quran ni andiko la mwanadamu,

Umesoma evolution of man vzuri ya Darwin?
Kama umesoma Unataka uthibitisho gani sasa wakati kuna uthibitisho mpaka wa vinasaba humo.
 
Utamu wa maisha utegemea na tafsiri yako mwanadamu si zaidi ya kula na kunywa mengine ni ziada.
Kila jambo ni ili Mungu apewe utukufu,mateso na magonjwa ni matokeo ya dhambi either za kurithi au kutenda mwenyew binafsi.
Karibu nikupe shule
Nimekupa scenario hapo za watu ambao hawana huo utamu hata nusu.
Na umeshindwa kujibu vizuri hoja nlizokupa.

Bado unataja habari za Mungu ambae umeshindwa kumthibitisha!

Unaweza kumthibitisha kama yupo kweli na si hadithi tu za kutungwa na watu zikarithishwa vizazi hadi vizazi?

Kushindwa kwako kumthibitisha hapo, kushindwa kwako kumtolea hata contradiction kwenye dhana ya uwepo wake pia ni udhihirisho mzuri kabisa kuwa huyo Mungu hayupo, na wala hawezekani kuwepo.
 
Mkuu kwanza naomba nkuhakikishie kuwa maandishi yote ni ya mwanadamu.

Kwahyo ni sawa evolution ni andiko la mwanadamu, biblia ni andiko la mwanadamu, quran ni andiko la mwanadamu,

Umesoma evolution of man vzuri ya Darwin?
Kama umesoma Unataka uthibitisho gani sasa wakati kuna uthibitisho mpaka wa vinasaba humo.
Mimi nimeuliza chanzo cha huyo mnyama wa kale, ukiwa wewe umeielewa vyema nadharia ya D

Hujajibu swali langu zaidi ya kuniambia tafiti zinaendelea kufanyika bila kunitajia hao watafiti. Pili, fahamu leo dini kupinga nadharia ya Darwin, pia huko nyuma wanasayansi walimpinga kwa maandiko miaka ya 1940 kurudi nyuma na kubomoa msingi wa hoja zake.
Kwa mfano, WHAT DARWIN GOT WRONG by Jerry Fodor na Massimo Piattelli-Palmarini. Na mwanasayansi Thomas Nagel kupitia kitabu chake MIND AND COSMOS: WHY MATERIALIST NEO-DARWINIAN CONCEPTION OF NATURE IS ALMOST CERTAINLY FALSE.
Hawa ni kwa uchache tu. Mana Darwin analazimisha dhana yake ikubadilike wakati imejiegemeza katika msingi wa "survival" bila kueleza asili "arrival of those hamo habilis".
Toa proof na sio kunilazimisha kuiitakidi evolution of man kijuu juu.
Mwisho, sitaki kutumia kitabu changu cha dini kukujibu, nataka twende kwa kumtumia huyo huyo Darwin na wapinzani wake
 
Moto au baridi. Mungu hataki mtu awe vuguvugu.

UFUNUO 3:16

YESU NI BWANA NA MWOKOZI
Asante mkuu, nilitaka isomeke hivyo...

Nafikiri hapo chini niliposema kwa shetani hawapo kwa Mungu hawapo ilieleweka...
 
Moto au baridi. Mungu hataki mtu awe vuguvugu.

UFUNUO 3:16

YESU NI BWANA NA MWOKOZI
Sasa kwa wanaume inakuwaje wakisema Yesu ni bwana wao.

Yesu ni mwokozi wanini? Anaokoa kitu gani majengo yanaungua moto tunasaidiwa na zimamoto, ndege ilitumbukia ziwani tukaokoa wenyewe tukiongozwa na Majaliwa.

Yesu anaokoa nini?
 
Mimi nimeuliza chanzo cha huyo mnyama wa kale, ukiwa wewe umeielewa vyema nadharia ya D

Hujajibu swali langu zaidi ya kuniambia tafiti zinaendelea kufanyika bila kunitajia hao watafiti. Pili, fahamu leo dini kupinga nadharia ya Darwin, pia huko nyuma wanasayansi walimpinga kwa maandiko miaka ya 1940 kurudi nyuma na kubomoa msingi wa hoja zake.
Kwa mfano, WHAT DARWIN GOT WRONG by Jerry Fodor na Massimo Piattelli-Palmarini. Na mwanasayansi Thomas Nagel kupitia kitabu chake MIND AND COSMOS: WHY MATERIALIST NEO-DARWINIAN CONCEPTION OF NATURE IS ALMOST CERTAINLY FALSE.
Hawa ni kwa uchache tu. Mana Darwin analazimisha dhana yake ikubadilike wakati imejiegemeza katika msingi wa "survival" bila kueleza asili "arrival of those hamo habilis".
Toa proof na sio kunilazimisha kuiitakidi evolution of man kijuu juu.
Mwisho, sitaki kutumia kitabu changu cha dini kukujibu, nataka twende kwa kumtumia huyo huyo Darwin na wapinzani wake
Wewe hujajibiwa hilo swali?

Post #218 nmekujibu.

Halafu mbona unaandika mengi bila kujibu swali langu ili tuelewane.

Umesoma hyo nadharia ya evolution vzuri?
 
Kwanini usisome na hayo maandiko ya wanasayansi nliokutumia ujue nao hoja zao. Mana hao sio wadini, ni wanasayansi tu. Kuhusu kuisoma vzuri hiyo nadharia, nmeisoma na nikatafuta hayo maandiko ya ziada, kwa iyo nasimamia ktk upande wa kumpinga Darwin.
 
Nimekupa scenario hapo za watu ambao hawana huo utamu hataUwepo nusu.
Na umeshindwa kujibu vizuri hoja nlizokupa.

Bado unataja habari za Mungu ambae umeshindwa kumthibitisha!

Unaweza kumthibitisha kama yupo kweli na si hadithi tu za kutungwa na watu zikarithishwa vizazi hadi vizazi?

Kushindwa kwako kumthibitisha hapo, kushindwa kwako kumtolea hata contradiction kwenye dhana ya uwepo wake pia ni udhihirisho mzuri kabisa kuwa huyo Mungu hayupo, na wala hawezekani kuwepo.

Kwanza hujanijibu swali langu la pili hapo.
Ngependezwa unijibu.

1♦️Kisichopo hakithibitishiki kuwa hakipo.
Ila naweza kukuonesha kwa udhihirisho mzuri tu kuwa hakipo.

Katika kutambua uwepo wa vitu, viumbe hai hutumia mifumo yao ya utambuzi kama msingi wa kwanza kuthibitisha vilivyopo.

1.Mungu sijawahi kumuona.
2.sijawahi kumlamba
3. sijawahi kumnusa
4. sijawahi kumsikia
5. sijawahi kumhisi

Hivyo kuhusu mifumo ya fahamu hapo juu katika kutambua uwepo wa kitu, Mungu hajatambulika.

Lakini pia tunaweza kujaribu kutumia njia za vipimo ili kutambua uwepo wake.
Katika hili pia Mungu hayupo hawezi kupimwa popote pale.

Hata ukishika science tu, utaona Mungu wako huyu anaekutaka ukamwabudu hayupo na hana uwezekano wa kuwepo.
Ukipitia vitabu vinavyodaiwa alivitunga yeye ukacompare na science ya anga jinsi mambo yalivyo katika uhalisia unaona kabisa Mungu muweza wa yote, Mungu mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.

Udhihirisho ambao ni mkubwa zaidi ambao hauna chenga chenga ni kuhusu dhana ya uwepo wake kuingia kwenye mzani wa mantiki

Kwa kutumia Proof by logical consistency, Dhana ya uwepo wa Mungu inacontradiction kubwa sana ambayo hata wewe hujaweza kuitatua.

Hivyo huo ni udhihirisho mwingine kuwa Mungu huyo hayupo na wala hana uwezekano wa kuwepo.

2 ♦️kinachoupa mwili nguvu

kuna njia kadhaa ambazo huupa mwili Nguvu kuna michakato mingi na mifumo ya mwili. Hapa kuna vyanzo muhimu cha nguvu za viumbe hai:
  1. Metaboliki: Nguvu za viumbe hai zinategemea uwezo wa kubadilisha nishati ya kemikali inayopatikana kutoka kwenye chakula na kuifanya kuwa nishati ya kimetaboliki. Katika michakato ya metabolic, sukari na mafuta huvunjwa kuwa adenosine triphosphate (ATP), ambayo ni chanzo kikuu cha nishati ya seli. ATP hutoa nguvu inayotumiwa na seli za mwili kutekeleza kazi zake, kuanzia kazi za msingi za kimetaboliki hadi shughuli za kimwili na kiakili.
  2. Mfumo wa upumuaji: Nguvu za viumbe hai zinahitaji oksijeni ili kutokea. Mfumo wa upumuaji una jukumu muhimu katika kusambaza oksijeni kwa tishu zote za mwili. Wakati wa kupumua, hewa yenye oksijeni huingia kwenye mapafu na oksijeni hiyo huvuka kwenye kuta za mapafu na kuingia kwenye mfumo wa damu. Hapo ndipo oksijeni inakusanywa na seli za mwili kwa ajili ya kutengeneza ATP kupitia michakato ya kemia ya seli

Unafahamu respiration?
Kisayansi mifumo ya utambuzi ipo mitano lakini nje ya sayansi ipo kumi.
Sayansi si pekee ndio ya mwisho kutoa majibu lakini tu kama utaki kukua kimaarifa.
Evolution theory ya Darwinism ni uongo mtupu usio na chembe ya ushahidi ukilinganisha na viumbe vya Sasa mbona haviendelei na huo mchakato wa kubadilika.
Pia Dunia Haina umri wa hayo ma miaka millions yanayotajwa
 
Back
Top Bottom