Kama ulikuwa hujui kuna watu wanakesha vitandani bila kupata usingizi basi miliki Xtrial, Morano au Dualis ndio utaelewa.
Ni zaidi ya maumivu ya mgongo.
Yaani mtu anamiliki gari ya milioni 25 kutoka Japan, anatembelea miezi miwili tu anajikuta anatakiwa kufanya services ya 1.3milioni, anapambana anafanya, hajatulia kidogo ndani ya wiki mbili anatakiwa services ya laki 6, anapambana anarekebisha, hajatulia anambiwa akishatembea kama wiki mbili zingine ajipange kwa service nyingine ya laki 7, akitulia kidogo anaambiwa kuna utitiri wa vidubwasha vya kuja kubadilisha ndani ya miezi sita ijayo vyenye thamani ya 3.5milioni ili chuma ikae sawa kuweza kupiga route mbili tatu ndefu au kumpush kwa mwaka hivi ili isisumbue sana. Na hapo hapo fundi wake makini kabisa anayemwamini anamwambia hizo ni karaha za kawaida kabisa za Nissan na kama zinamkera ni bora auze tu mapema ali anunue kitu kingine. Kwanini asiuze mapema?
Mtu anaona gari ya 25milioni bora aisukume chap chap sasa hata kwa 18milioni ili ajazie kiasi na kuvuta mchuma wowote mwingine wa chap chap.