Hicho kimbembe mara nyingi huanza mapema mnoo (na hii ndio sababu kuu ya wamiliki wake kuziuza mapema mnoo), huwa kinaanza baada ya kufanya service ya pili ya kawaida, hapo kinakuwa kimeshatembea wastani wa km 5000 hivi tangu mtu amiliki chombo. (Kumbuka service ya kwanza hufanyika mara tu chuma kilipotua nchini kutoka Japan kabla ya mmiliki kuanza kupiga misele nacho).
Mara nyingi huwa ni mizunguko ya hapa na pale mjini humu humu, na mara chache labda route moja au mbili (To&fro) ya mkoani (Dar-Arusha, Dar-Dom, Dar-Mwanza).
Mara nyingi hizo chuma zikiwa zimetoka Japan unakuta zimeshatembea kati ya km elfu 70-120, nadra kukuta milleage iko chini ya Km elfu 50.
Sasa, mhusika anakuja kugundua mambo haya, ambayo hakuyategemea.....
1. Fuel consumption sio rafiki (tofauti kabisa na alivyoaminishwa na watu kabla ya kumiliki chuma)
2. Vipuri vingi vidogo vidogo ni rahisi kuharibika na vinagharama kubwa ukilinganishwa na gari pendwa Toyota! Gari ni delicate kuliko alivyotazamia, kashikashi kidogo tu, tukutane kwa fundi. Kuna vidubwasha vinaitwa 'sensor' hizo ni muhimu mnoo kwa hiyo gari na vinapasua vichwa balaa.
4. Gari inapenda services za mara kwa mara, na service zake zimechangamka kiasi.
5. Gari haitaki wala haipendi janja janja za kuokoteza vipuri holela na mafundi wa kidananda.