Kwanini watu wanaziuza Nissan Xtrail kwa wingi sana?

Kwani hizo gari wanamnunulia mamako mpaka useme hivi? Usipangie watu namna ya kuishi. Wewe nunua unachoweza.
 
Mgongo je?
Kama ulikuwa hujui kuna watu wanakesha vitandani bila kupata usingizi basi miliki Xtrial, Morano au Dualis ndio utaelewa.
Ni zaidi ya maumivu ya mgongo.

Yaani mtu anamiliki gari ya milioni 25 kutoka Japan, anatembelea miezi miwili tu anajikuta anatakiwa kufanya services ya 1.3milioni, anapambana anafanya, hajatulia kidogo ndani ya wiki mbili anatakiwa services ya laki 6, anapambana anarekebisha, hajatulia anambiwa akishatembea kama wiki mbili zingine ajipange kwa service nyingine ya laki 7, akitulia kidogo anaambiwa kuna utitiri wa vidubwasha vya kuja kubadilisha ndani ya miezi sita ijayo vyenye thamani ya 3.5milioni ili chuma ikae sawa kuweza kupiga route mbili tatu ndefu au kumpush kwa mwaka hivi ili isisumbue sana. Na hapo hapo fundi wake makini kabisa anayemwamini anamwambia hizo ni karaha za kawaida kabisa za Nissan na kama zinamkera ni bora auze tu mapema ali anunue kitu kingine. Kwanini asiuze mapema?

Mtu anaona gari ya 25milioni bora aisukume chap chap sasa hata kwa 18milioni ili ajazie kiasi na kuvuta mchuma wowote mwingine wa chap chap.
 
Kwani hizo gari wanamnunulia mamako mpaka useme hivi? Usipangie watu namna ya kuishi. Wewe nunua unachoweza.
Wewe sema maneno yote... Mimi nipo hapa kwajil ya kuwaelimisha wajinga kama wewe ambao ni useless hamjitambui na hamna exposure ya maisha... Nikusaidie tu siku ukipata pesa za kubet au ukihongwa na mume wa dada yako, usinunue magari yasiyo na maana kwa kuogopa spares au ulaji mafuta...
Nikuambie tu hata V8 haili mafuta kama masikini wenzako walivyo kuaminisha... Wewe bado mtoto mdogo bado unanuka maziwa ya mama yako huwez kuelewa hii elimu nayokupa...
Kwani wangap wananunua hizo gari za bei rahisi mnazozipenda mnasema hazili mafuta na spares bei rahisi lakini bado wanashindwa kuzihudumia..?
Gari yoyote usipozingatia menu yake itakusumbua 🤣💩 mbona njian kuna IST SPACIO na VITZ nyingi mmetoka kununua juzi tu ila zimechoka zinapiga kelele kama vile zina miaka 10 barabarani?
Exposure na Elimu ni jambo la muhimu sana ktk maisha, nakusaidia haya ili ukiwa mkubwa usidanganywe
 
We sijui ni mdigo au mzaramoo? Unapayaya sana! Aiseee

Ila MUNGU ameumba jamani 😂
 
Alafu ukute mwamba haumiliki chombo chochote cha usafiri 😂😂😂. Ngoja nikwambie kitu, hakuna mmiliki na mpenda magari asiyewaza ulaji mafuta wa gari lake. Trust me huyo mmiliki wa hivyo hayupo.

Lazima tu atawaza consuption na power ya gari yake.
 
Umepiga Mule mule
 
Bila shaka upo kwa Ruto
 
Na hapo anakuwa katembea kilomita ngapi? Maana isije ikawa safari za mkoani daily alafu mtu alalamike service inawahi wakati anaenda za masafa daily.
 
Mimi sikupingi as long as umeamua kufikiria hivyo basi naheshimu mawazo yako, japo wewe hujataka kuheshimu yangu... Na kamwe siwezi kuthibitisha kama namiliki chombo chochote au laaaah...
Ila nikufungue akili kwa faida yako na kizazi chako, ukiona unanunua gari kwasababu ya ulaji wa mafuta au spares maana yake wewe bado huna uwezo unalazimisha maisha maana yake unalazimishwa kubakwa na maisha...
 
Shida kubwa ni transmission na engine. Kimojawapo lazma kitakusumbua. Nina ushuhuda wa Nissan Dualis ya boss wangu kasha overhaul mara moja ila matatizo hayapoi. Sahizi gari imekufa ac haipoozi🤣 na haiwez kupanda hata kreti la soda la pepsi. Yani mlima wenye inclination sawa na creti la soda gari haina nguvu ya kupanda.
 
Wewe Mjapan ongelea kuhusu gari bwana mambo ya beer tuachie wanywaji na wamiliki wa pombe shop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…