Kwanini watu wanaziuza Nissan Xtrail kwa wingi sana?

Ongea point ueleweke we pimbi
 
Still ur Soo nothing in our mindset brow wasingetengeneza na watu wasinge nunua stupid that's what u say
 
Kwenye avatar Yako hiyo ni gari Gani mkuu😄😄
 
Nissan xtrail ni gari nzuri sana kama ni mtunzaji, nilimiliki xtrail T30 karibu miaka 7 sijawahi kujuta. Niliuza kwa kubadili tu gari.
 
Haya maelezo yamejitosheleza kabisa!
 
Na hapo anakuwa katembea kilomita ngapi? Maana isije ikawa safari za mkoani daily alafu mtu alalamike service inawahi wakati anaenda za masafa daily.
Hicho kimbembe mara nyingi huanza mapema mnoo (na hii ndio sababu kuu ya wamiliki wake kuziuza mapema mnoo), huwa kinaanza baada ya kufanya service ya pili ya kawaida, hapo kinakuwa kimeshatembea wastani wa km 5000 hivi tangu mtu amiliki chombo. (Kumbuka service ya kwanza hufanyika mara tu chuma kilipotua nchini kutoka Japan kabla ya mmiliki kuanza kupiga misele nacho).

Mara nyingi huwa ni mizunguko ya hapa na pale mjini humu humu, na mara chache labda route moja au mbili (To&fro) ya mkoani (Dar-Arusha, Dar-Dom, Dar-Mwanza).
Mara nyingi hizo chuma zikiwa zimetoka Japan unakuta zimeshatembea kati ya km elfu 70-120, nadra kukuta milleage iko chini ya Km elfu 50.

Sasa, mhusika anakuja kugundua mambo haya, ambayo hakuyategemea.....
1. Fuel consumption sio rafiki (tofauti kabisa na alivyoaminishwa na watu kabla ya kumiliki chuma)

2. Vipuri vingi vidogo vidogo ni rahisi kuharibika na vinagharama kubwa ukilinganishwa na gari pendwa Toyota! Gari ni delicate kuliko alivyotazamia, kashikashi kidogo tu, tukutane kwa fundi. Kuna vidubwasha vinaitwa 'sensor' hizo ni muhimu mnoo kwa hiyo gari na vinapasua vichwa balaa.

4. Gari inapenda services za mara kwa mara, na service zake zimechangamka kiasi.

5. Gari haitaki wala haipendi janja janja za kuokoteza vipuri holela na mafundi wa kidananda.
 
Wanaume pia wanachambana hivi?
Ina
Kiongoz umetisha sanaa 👍👍 sio watu wanatutukana bila evidence bila kuangalia mfuko wako Aya magari yapo na yanuzwa hapa nchin shida ni mazingra ya mtu aliyopo Hali ya kimazingira kiuchumi n.k
 
Xtrail ni gari yenye muonekano mzuri wa SUV na bei ya kumiliki ni rafiki kabisa, hilo limepelekea watu wenye kipato cha kati kukimbilia kumiliki. Kimbembe kinakuja kwenye gharama za services and maintenance, ambapo ni kubwa zaidi isiyooana na urahisi wa kuimiliki, na hapo huleta majuto kwa wamiliki, suluhisho kwao ni kuuza haraka mnoo kabla gari haijamfilisi.
 
Mnawachanganya vijana wanaanza kumiliki magari.....any way kijana anza katoyota mi nitàanza na ist
 
Gari imetembea 120,000km ndio ikanunuliwa na kuletwa nchini. Leo tunasema Xtrail ni gari mbovu na haifai, sidhani kama hilo ni jibu sahihi.

Kama ilitembea 120k km huko maana yake tuna shida katika maintenance, caring na/au ubovu katika miundombinu yetu, haiwezekani gari itembee 120k km huko, ije hapa itembee 5k km na tayari isumbue.

Tatizo lipo kwa wamiliki, wananunua vipuri sio sahihi, tatizo lipo kwa mafundi, hawapo competent kutengeneza hizo gari, tatizo lipo kwenye miundombinu ya barabara, hazifai kwa matumizi ya SUV-LUXURY.
 
Mnawachanganya vijana wanaanza kumiliki magari.....any way kijana anza katoyota mi nitàanza na ist
Mkuu,
Hata mitsubishi ni gari imara tu, sio lazima Toyota japo ni gari zinazoweza kuhimili sana mazingira yetu na uchumi wetu.
 
Sasa mbona unamtukana wakati kiuhalisia komenti yako imeunga mkono komenti yake?
 
Heri yako wewe mwenye gari expensive, heri yako wewe ambae unajitoa kwenye kundi la wa Tanzania sjui wewe ni wa nchi gani kiongozi🥶
 
Kweli kabisa.
Unakutana na gari namba E imesha bondwa bondwa mpaka unashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…