Kwanini Watutsi wanapendelewa sana huku wahutu wakipuuzwa, kudharauliwa ili hali wao ni wengi. Je, kuna madhara yoyote kwa hili?

Vita vya 1990-1993 vilikuwa baina ya majeshi pinzani, sio vya kulenga kuangamiza jamii fulani tu.

Ila naamini hata Drc inastahili mahakama ya aina hiyo juu ya uhalifu uliotendeka huko.

mtu chake zitto junior Moronight walker
JokaKuu
Huwezi kutenga vita na siasa zilizopelekea hivyo vita. Kitaalamu tunaita, Jus Ad Bellum na Jus In Bello. Kwenye Jus Ad Bellum tunachunguza sababu za kisiasa ambazo zimepelekea vita kutokea. Tunaangalia nani ni mhusika (Belligerents), kwanini nchi au makundi yamepigana vita, nani ni mkorofi na sheria za kimataifa hasa zile za umoja wa mataifa (UN) zinasemaje kuhusu hili.

Kwenye Jus In Bello, tunachunguza jinsi ambavyo hivyo vita vimepiganwa (Means and Methods of Warfare) na kufanya tathmini ya madhara yake kwa raia wa kawaida, mali zao na mazingira kwa ujumla. Hapa sasa ndipo tunachunguza jinai za kimaitaifa (Core International Crimes) ambazo mara nyingi hutokana na vita.

Jinai kama Uhalifu dhidi ya binadamu (Crime Against Humanity), Uhalifu wa kivita (War Crimes) na Mauji ya kimbari (Genocide), ambazo mara nyingi hufanyika wakati wa vita kwa maksudi au uzembe wa wanajeshi na maafisa wao (Commanding Officer).

Ukitaka kutengenisha siasa za kikabila za Rwanda ambazo zilianza tokea mwaka 1958 na vita kilichotokea mwaka 1990, 1994, 1997, 1998 na kuendelea mpaka sasa ni sawa na kumtenganisha TEMBO NA PEMBE ZAKE.

Lakini pia, historia ya siasa za nchi kama Rwanda husaidia kwenye suala zima la kutafuta haki na suluhu (Transitional Justice and Reconciliation) ambalo huanza punde baada ya mgogoro kuisha ili kuweza kujenga jamii imara ambayo haina migogoro.

Hapa ukitenganisha siasa za nchi husika na mgogoro wa kivita, huwezi kukata mzizi wa fitina. Maana watusi hawakuamka tu kutoka usingizini na kuanza kuchinja watutsi, au RPF hawakuanza tu kuua maelfu ya wahutu kule Kibeho mwaka 1990. Kuna sababu ambazo zilipelekea vitendo hivyo kutokea....

NB: Kuhusu DRC kuwa na mahakama kama ICTR nadhani ni utani mwingine ambao utatupotezea muda, rasilimali na kutuachia mijadala isiyo na mantiki. Miaka 28 tokea 1994, mahakama ya ICTR imewafunga wahalifu 61 tu (Convicted 61 members only) huku ikiwaachia (Acquitted ) wengine 14 kwasababu mahakama ilikosea kuchambua ushahidi.

Serikali ya DRC ishapeleka kesi kwenye mahakama ya haki ya dunia (The International Court of Justice) kuomba dunia ikemee uvamizi wa Rwanda na Uganda na kudai fidia za uvamizi wa kijeshi, wizi wa rasilimali, uuaji wa raia na uharibifu wa mazingira, lakini hakuna kilichofanyika mpaka leo hii. Unadhani mahakama kama ICTR nchini DRC ndiyo itafanya chochote cha maana ???

Mkuu ACHA MZAHA......
 
umeelezea kwa weledi
 
Kibeho ilikuwa 22/4/1995
Kuna mauaji makubwa yalifanyika baada ya uvamizi wa ghafla wa RPF, kabla hata ya mwaka 1994. Mimi nimeona picha zake za mauaji kule ICTR-Arusha kutoka kwa mawakili upande wa utetezi. Mahakama kwasababu zake izijuazo iliukataa ule ushahidi...

Hii ni moja ya hoja ambayo upande wa utetezi wakina Prof Juan Mwaikusa walijaribu kuitumia kuwanasua watuhumiwa, lakini mahakama ilikataa kusikiliza ikisema haina mamlaka (Jurisdiction) kusikiliza kesi kabla ya mwaka 1994.

Hivyo mauaji ya Wahutu yaliyofanywa na RPF hayakuguswa kabisa.
 
Hata ukiwaambia ni kazi bure. Mtusi ni mbaguzi na mwenye dharau kwa kabila zingine. Ni waroho wa mali na wachoyo. Wanapenda kufa na kupona madaraka ya kisiasa. Wanatafuta madaraka na mali popote nje ya nchi yao ya asili.
Kwa Mtutsi ukweli ni kile anachotaka yeye. Kwa hivyo ni watu wabishi kupindukia. Tabia yao ni kama wayahudi.
Afrika hasa maeneo ya maziwa makuu wanapopatikana inabidi kuwatambua hawa watu ili kuwadhibiti. Tabia yao inasababisja kuchukiwa na wengine na hata wengine kufikia kutaka kuwaangamiza.
Binafsi nafikiri watutsi wanapaswa kujitafakari kwa mustakabali wao.
Wapo exceptions wachache watu wema tu. Tungependa kuishi kwa amani na hawa jamaa ila wana kazi kubwa kujirekebisha maana ni tabia yao ya asili.
 
Kila uchaguzi majeshi aliyoleta Nyerere yanamwaga damu za Wazanzibari
Kumbe wewe ni zanzibar.
Mimi NASHANGAA sana NYIE, hakuna makubaliano ya Kushare resources na TZ bara.
Lkn pesa zikikopwa NYIE mnapewa lkn SISI ndio tunalolipa hilo deni. Na hatufanyi lolote. MZanzibar anauwezo wa kuja huku hata kununua ARDHI na kufanya mambo mengine. Lkn wa huku aende Kule kama ARDHI atapewa. Labda awe mwekezaji.
Kuna siku KULIKUWA na tetesi kuwa kuna mafuta zanzibar kwenu huko. MKAPIGA KILELE KUWA MNATAKA KUJITENGA KISA MAFUTA , KWA UDHAHIFU WA AKILI ZENU MLIFIKILI TUNATAKA MAFUTA YENU WQKATI WALA.
SASA NANI MWENYE SIDA.
NA ZANZIBAR WANATEGEMEA VITU VINGI SANA KUTOKA BARA KUANZIA CHAKULA NA CITU VINGI SANA , HATA VIONGOZI WENU HUKO WANAJUA PEKEENU MTAPATA SHIDA SANA.
 
Ya Kabla ya 1994 kutoka October 1990 mpaka October 1993 waliuwa wahutu kama 40,000. Na watutsi baadhi ikiwemo watutsi wa bagogwe tribe.
 
Naona hakuna upendeleo, ni vigezo tu. Watusi karibu wote ni wasomi na fani zao za uhakika. Wakati wa interview hawaangalii usoni.
 
Ya Kabla ya 1994 kutoka October 1990 mpaka October 1993 waliuwa wahutu kama 40,000. Na watutsi baadhi ikiwemo watutsi wa bagogwe tribe.
Hoja ya msingi ni kwamba mauaji makubwa ya Wahutu yamefanyika nchini Rwanda kabla na baada ya mwaka 1994. Haikuishia hapo, RPF wakishirikiana na serikali ya Burundi walifanya mauaji makubwa ya wakimbizi wa kihutu nchini Zaire na Tanzania.

The UN Mapping Report iliyoandaliwa na Dr. Koffi Annan na kuzuiwa kuchapishwa na wakubwa wa dunia hii imeandika madhambi mazito yaliyofanyika DRC/Zaire na serikali ya Kabila, Rwanda, Uganda, Angola, Zimbabwe pamoja na makundi ya Kihutu na Kitutsi.

Unyama wa hali ya juu mno. Hadi nafikia sehemu kujiuliza hivi Baba wa Taifa anavyoratibu kupanga mipango ya kuvamia DRC kule Kampala mwaka 1996 na vijana wake wakina Museveni, Kabila na Kagame, alikuwa haoni kwamba yatatokea madhara makubwa kwenye huu ukanda ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…