Kwanini Watutsi wanapendelewa sana huku wahutu wakipuuzwa, kudharauliwa ili hali wao ni wengi. Je, kuna madhara yoyote kwa hili?

So alipata nafasi ya kumnyoosha mobutu baadae kwa kutumia wale vijana wake aliyowalea huku Tz. Ndio maana nchi zote kasoro kenya zikuja kuongozwa na vijana wa mchonga
Huu ushawishi Nyerere aliokuwa anautaka ulitusaidia/umetusaidia hata kidogo kiuchumi?..
 
Umenifungua macho mkuu
 
Nakusoma mkuu! Aliyeandika hii barua ni Jaji Gerlad Gahima, aliyewahi kuhudumu kule The International Criminal Tribunal For The Former Yugoslavia (ICTY). Siku hizi amekuwa mkimbizi akidai anataka kuuwawa na General Paul Kagame.

Kuna mahojiano yake alifanya na Tshaka Salli kuhusu makosa ya kimataifa yanayofanyika ukanda huu wa maziwa makuu (Great Lake Regions), na udhaifu wa makakama za kimataifa kama The International Criminal Court (ICC).

Humo ndani amekiri kwamba General Kagame na Museveni wamefanya uhalifu mkubwa mno dhidi ya binadamu. Kumbuka huyu alikuwa ni mwanachama kindakindaki wa RPF, hivyo anafahamu fika anachokisema.

Nikirudi kuhusu siasa za Rwanda Circa 1994: Kuna maswali mengi yameachwa zaidi ya majibu. Machache ni hayo niliyokuuliza hivi punde. Ila kusema kwamba Tanzania ilikuwa haifahamu kwamba Marekani, Uingereza na Israel zilikuwa zinahusika nyuma ya Rwanda na Uganda napata ukakasi.

Serikali ya Tanganyika ina mkono mrefu mno kuliko ambavyo wengi tunapenda kukashifu na kudanganyana humu ndani. Kwamba Mzee Nyerere alikuwa hafahamu kinachoendelea nyuma ya pazia na hawa vijana wake Kagame na Museveni aliowakuza mwenyewe. Nazidi kupata ukakasi.

Swali jingine: Wakati mauaji ya Raisi Juvenile na Cyprian yanafanyika, Umoja wa Afrika (O.A.U) walipendekeza iundwe kamati maalumu ya uchunguzi. Kuuwawa wakuu wawili wa nchi, tena kwa kombora ni jambo zito ambalo ilibidi litiliwe mkazo. Kule O.A.U mambo yalienda kimaajabu. Unafahamu nani alikuwa ni Katibu Mkuu (Secretary General) wa O.A.U wakati wakulungwa wanapendekeza uchunguzi ufanyike ???

Kijana mwingine wa Mzee Nyerere kutoka visiwani: Dr Salim Ahmed Salim....

NB: Come to think of it, the Great Lake Region is another Wild-Wild West. Full of lawlessness, megalomania, greed, political fiascos and military adventurism. You look at Kagame, Museveni, Tsishikedi and Kiir is like I'm watching The Movie: Mad Max, Furry Road (It's just diabolical)

Binafsi ningekuwa na mamlaka makubwa ningeifunga kabisa Tanganyika, isijuhusishe hata kidogo na hizi siasa za Uganda, Rwanda, Burundi na Kongo bila sababu maalum. EAC ingebaki na nchi tatu tu za mwanzoni. Hawa wengine wangekuwa waalikwa tu (Observers)

Watutsi, Wahutu, Wasudani na Wakongo wayamalize matatizo yao wenyewe. Sisi nasi (Tanganyika) tufanye yetu, maana ni mengi mno tena mazito...
 
Kuna siku Mwalimu Nyerere aliwahi kualikwa na Raisi Mobutu kule kijijini kwao Gbadolite. Ilibidi apande ndege ili kufika lakini baadaye Mwalimu Nyerere akatoa udhuru wa ghafla kwamba hatafika. Raisi Mobutu alionesha kukasirika sana...

Kwanini Mobutu alikasirika vile ???....

NB: Hivi kwanini kile kitabu ambacho Mzee Nyerere alikiandika mwishoni wa uhai wake, yule jamaa wa Lupaso alikipiga kiberiti. Alikuwa anaficha madudu gani ???
 
Ila kusema kwamba Tanzania ilikuwa haifahamu kwamba Marekani, Uingereza na Israel zilikuwa zinahusika nyuma ya Rwanda na Uganda napata ukakasi.
👍
Ila MIMI mwenyewe nafikili hata Tanzania wangejaribu kuzuia genocide SIDHANI kama wangefanikiwa kutokana ile issue ilikuwa ni mkakati kabisa.
 
Mzee Nyerere alikuwa hafahamu kinachoendelea nyuma ya pazia na hawa vijana wake Kagame na Museveni aliowakuza mwenyewe. Nazidi kupata ukakasi.
NIMEWAHI KUONA DOCUMENTARY MOJA KUHUSU Kifo cha mwanzilishi wa RPF and RPA rafiki wa MU7 mejar general fred rwigema. Ambapo PK alihusika na kifo kile.
Niliiona kuwa MU7 na wenzie na PK na mwenzako wameishi WOTE hapa DSM mpaka nyumba yao walionyesha.
 
Mkuu mkoa wa Tabora ni mkubwa sana. Rwanda inalingana na wilaya ya Sikonge. Google alafu tuletee mrejesho!
 
Sasa inatuhusu nini sisi watanzania?
Fungua medula yako mkuu, duniani tunaishi kama kijiji sasa hivi. Rudi shule ukasome maana naona bado ujinga uliokuwa nao haujafutika hata for 2% only.
 
YAO NAKUELEWA.
ISSUE YA MAUAJI YA KIMBALI RWANDA NI ISSUE PANA SANA UKIANZA KUCHUNGUZA UTAKUTA WAHUSIKA NI WENGI SANA HASA NCHI KUBWA.
USA NDO MUHUSIKA MKUU UNDER BILL
CLITON.
NA ndo maana bill CLITON na kagame ni marafiki sana tena sana na ndie anayemtetea mpaka leo. Anamuita SHUJAA.


Na issue ilikuja kwa nini wahutu wakimbizi walikimbilia congo pamoja na millitia(interahamwe) na ex far.
Ila ikaonekana RPA walikuwa wanapigana kuelekea kigali kwa UPANDE wa mashairiki yani kutoka kaskazini kwenda mashairiki kuelekea kusini mwa rwanda then kwenda magaidi.
Na ikaonekana kumbe ilikuwa na mchezo ulipangwa ililenga congo(zaire)
 
On a side note, hivi unakumbuka katika maadhimisha ya miaka 100 ya Maisha ya mwalimu Nyerere, familia ya Nyerere ilialika watu wengi sana waliofanya kazi na mwalimu, na watu waliokuwa karibu na mwalimu ikiwemo familia ya kawawa, mzee Mwinyi na watu kedekede lakini hakukuwa na mtu kutoka familia ya Mkapa!.
Na kitu kingine, Mkapa alipokufa, Familia ya Mwalimu ni kama vile ilijieweka mbali, hatukumuona mama Maria akienda ila alipokufa Magufuli mama Maria huyohuyo akaenda msibani
HIVI KUNA SIRI GANI KATI YA MKAPA NA NYERERE?
 
Kagame angetupasua bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…