Kwanini wazee wa zamani waliweza kuishi na ndugu wengi nyumbani, lakini kizazi hiki ni ngumu kuishi na ndugu?

Kwanini wazee wa zamani waliweza kuishi na ndugu wengi nyumbani, lakini kizazi hiki ni ngumu kuishi na ndugu?

Lakini tulizaliwa mjini sio vijijini, ndugu ndio walitoka vijijini kuja kutafuta maisha mjini, sema utakua sahihi kwa maana nakumbuka magunia ya mahindi na mihogo yalikua yanatoka kijijini, maramoja moja.
Nilitaka niseme na mimi hapa nakumbuka mzee ndugu wote walikuwa walija dar kutafuta maisha wanafikia home chumba na sebule watapewa kazi na kula kulala bure wakifajipata waneenda wanajitegemea kwa kifupi mzee alikuwa anajiweza angekuwa ana exposure hata 4/10 mzee angekuwa tajiri sana miaka hiyo 2000 mzee anachinja ng'ombe 6 na wanaisha chapu pombe yake ilkuwa serengeti
kiwanja chake ni vipub vidogo vidogo .....sahivi hao ndugu wanajikuta mastaa.
 
Ukisoma nyuzi nyingi humu JF unasoma watu wengi wanasema hawataki ndugu, hawawezi kuruhusu ndugu alale kwake na watoto wako radhi wampeleke akalale guest house mtaani ila sio kwake. Leo kwenye uzi huu naona wengi mnatamami muishi na ndugu majumbani kwenu.
Honestly nilikulia kwenye maisha ya ndugu kuchangamyika ila sasa hivi wala siwezi kusema natamani maisha yale. Sijawahi kuwakataza ndugu wasije lakini maisha yamebadilika kila ndugu na mpango wake.
 
Sio zamani tu mimi nikija kuamua kutulia nitakuwa na mke wangu watoto pamoja na whoever atakayekuwa na uhitaji wa kukaa kwangu awe wa upande wa ukweni au wa familia yangu, it takes chakula cha kutosha (kisiwe cha kibaba, kiwe ni kile cha kununua wakati wa mavuno, chukua gunia zako 5 za mahindi na 5 za mchele na maharage 60Kg-70Kg uone kama utalia njaa for a year.)

Sisi tumeishi hivyo nyumbani kwetu na moja kati ya mbinu niliyojifunza ili kufanikisha hilo ni manunuzi ya chakula cha jumla sio cha kupima kwa Mangi dukani, pale home kukuta gunia za mahindi,
mchele, maharage na mazaga mengine store ni kawaida sana, hiyo inasaidia kupunguza makali ya matumizi kwasababu mnabaki kujazia vitu vodogovidogo, hulazi watu njaa.
 
Back
Top Bottom