Kwanini Waziri January Makamba anaongoza majadiliano ya Wizara peke yake?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari zenu Wana wa JF.

Ukiingia katika ukurasa wa Twitter wa Mheshimiwa January Makamba Waziri wa Nishati, utabaini Jambo.

Jambo hilo sio jingine bali ni yeye kualika wataalamu na wadau wa Nishati kutoka maeneo mbalimbali duniani. Wataalamu hawa wamekuwa wakija wizarani ama waziri kukutana nao popote.

Jambo lisilo la kawaida humuoni Makamba akiwa na Katibu Mkuu Wizara, Naibu Waziri, Naibu Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Nishati, au Wa TANESCO, Wataalamu wa Mazingira, Mwanasheria nk.

1. Je hataki ushirikiano?

2. Hawaamini wenzie?

3. Wenzake ni wala rushwa?

4. Anajiamini kuwa Mbunifu na msimamizi Bora kuliko wote wizarani na wizara za kisekta?

5. Anataka kujizolea sifa pekee?

6. Wenzie wamemsusa na wamekaa pembeni kumsubiri aharibu?

7. Waziri pekee kiitifaki ndiye anayepaswa kuongoza mijadala?

8. Iko wapi dhana ya Collective responsibility au uwajibikaji wa pamoja?
 
Interesting question...
Manake hata akifanya sahihi akija kuondoka tunarudi kule kule...
Akikosea ndo kabisa hakuna wa Ku explain vision ilikuwa ipi...

January awe makini na hii wizara..inaongoza kwa kuua career za wanasiasa..

Karamagi
Msabaha
Muhongo
Kalemani..

Orodha ndefu
 
January hajawahi kuwa msafi kama mnavyo sema .
 
Inawezekana ikawa ni hatua za awali za kufahamiana.
 
Madili yao yanabrejeshwa maana yalikatiliwa mbali sana
 
Ufisadi tu
 
watanzania kwa majungu hamjambo.
nadhani maofisi yote ya umma uzooefu mlio nao ni kupigana majungu na fitina.
Badilikeni watanzania, punguzeni majungu makazini na fitina.
majungu na fitina makazini hupunguza ufanisi na husababisha migogoro na migongano.
 
Huyu awe makini sana
 
"Ukiingia ktk ukurasa wa Twitter wa Mheshimiwa January Makamba waziri wa Nishati, utabaini Jambo"

Mkuu, kwa kupitia nukuu hiyo hapo huu, hutambui kuwa akiwa ndiye waziri mwenye dhamana, yeye ndiye "figurehead & spokesman' wa wizara!? Kwa hiyo ni yeye ndiye ana wajibu wa kuzungumzia masuala muhimu ya nishati ambayo yanapaswa kuwasilishwa kwa umma.

Naibu wake anaweza kufanya hivyo kama atapata maelekezo kutoka kwake, na katibu mkuu na naibu wake humsaidia katika masuala ya kiufundi juu ya uendeshaji wa wizara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…