Wakuu
Kuna wazungu flan nilikua nao kwenye kuwasaidia project yao flani,so tukawa tuna ukaribu ambao mara nyingi tulijikuta muda wa lunch tunakua pamoja.
Wazungu pamoja na kuwa na mamiili makubwa but sio walaji wa chakula kingi kama sisi waafrika. Utakuta muda wa lunch mzungu anakula sandwich moja tu na juisi nusu glass anashiba. Back to sisi waafrika sasa.
Kwanza kuna mwingine bila kula ugali anaona hajala kabisa na muda huo huo afya zetu ndio hizi mgogoro.
Je, kuna siri gani kwa wazungu kula msosi kidogo?
Kula sana ama kula kidogo ni suala ambalo hata mimi pia hunishamgaza sana.
Kusema kwa mzungu ama mwafrika, hapana ni hulka tu ya mtu na mazingira yake pia, siyo kwa sababu ya race.
Mbona mitandaoni huwa tunawaona akina "pawa mwanakulya"kibao tu huko ulaya na wanafukia misosi ya kujaza ndoo?
Mimi si mlaji sana wa vyakula, ila kuna mambo nime experience kuhusu jambo hilo kama ifuatavyo:
Nikiwa nina pesa hamu ya chakula hupungua sana ama kupotea.
Kuna wakati nilipata zali la kudaka mamilioni kimasihara, nilisahau kula siku mbili hadi nikajistukia na kuanza kutengeneza kumbukumbu za ni lini nilikula kwa mara ya mwisho, nikajikuta nina siku2 sijala na sijaumwa na njaa, nikashangaa sana!
Nikiwa nyumbani kwangu kuwa nnauhuru wa kutaka kula chakula fulani na kukipata kwa wakati, basi njaa huwa hainikamati sawa sawa ninakuwa nimeridhika muda wote.
Njaa hunisumbua nikiwa safarini ama kwenye mialiko ambayo huwa sina uwezo wa kujiamria kula muda niutakao mimi.
Pia nikifanya kazi ngumu, scale ya ulaji huongezeka tofauti na ninapokuwa mapumziko ambapo hula kidogo na kukinaiwa.
Kwenye hili nadhani kila mtu ana experience yake, wengine hukiona chakula kama ni mkombozi na msuluhishi wa matatizo yao binafsi.
Maana kuna wengine, akiudhiwa ama kugombezwa, hasira zake ama mtero huuondoa kwa njia ya kula kama kujifariji.
Ama mwengine akifurahishwa sana na jambo fulani basi huishia kula kama njia ya kujipongeza.
Sent using
Jamii Forums mobile app