Weengi wanaamini mweusi ni mpenda njia za mkato 'shortcuts' tena hata hajali kama kuna mahali anaharibu au kuna watu anawaumiza
Weeengi humu wanaamini mtu mweusi ni ungaunga mwana
weengi humu wanaamini mweusi ni mtu wa dilidili za hapa na pale za kimjinimjini yaani almradi bora liende
weengi wanaamini mweusi ni mtu wa hadaa na konakona na usipokaa sawa anaweza kukuuza hata wewe kama fungu la nyanya
weeengi wanaamini mweusi ni full janjajanja na usanii mwingi
weengi wanaamini mweusi ni wa ahadi lukuki zisizotimizika
weengi humu wanaamini mweusi ni mtu wa maneno meeengi matamu kama asali lakini yasiyo na hata chembe ya tija
wakuu tatizo ni nini hasa mbona kuna weusi wengi tu wamenyooka hawana konakona mfano mzuri mimi mwenyewe hapa