Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

Mimi nafikiri TISS wenyewe ndiyo wameharibu taswira ya Chombo hicho kwa jamii! Wengine wanajisahau na kujionyesha kuwa ni Usalama!

Enzi za Mwalimu walikuwa waadilifu hata kuwajua ilikuwa kazi kweli kweli.Hata raia wa kawaida alikuwa hajui kama kuna chombo hicho.
 
haujanielewa mkuu, rudi kasome uzi. Mimi sijasema TISS ni magenius infact nimesema kinyume yani ni wakawaida wamejawa tu majigambo na wananzania washamba huwatukuza, kasome tena
Hii ni tabia au niseme utamaduni uliojijenga tangu zamani wakati wa mkoloni wakati kuna vibaraka wa kupeleka habari kwa watawala. Walipoingia waafrika watawala nao wakaendelea kutumia hii njia ili kuwafanya wananchi wawaogope. Hili likafanya matapeli kuiga. Kwa kifupi hii ZAIDI ni kwa Afrika kwa sababu hawa wapelelezi hutumika.
 
We vaa tu sutiKaunda nyoa kipara nenda kaunta kunywa WINDOKU ukiwa umesimama kaunta...macho yako yanaangaza angaaza kila kona
Utaona Wabongo wananong'onezana wengine hata kukimbia kaunta.....

MAUJIKO ..teh teh teh....yani kutisha tu watu
Mtaani tunatishana sana na hzo kaundasut😁
Juzi kati kuna kituo Cha afya nilienda pande za bunju, nilipofika pale nikakuta Kuna mishemishe nyng manes madocta wako bize sana sio kawaida yao nikaaulizaa nikaambiwa Kuna wageni wazungu wanakuja hapo hospital

Sasa Kuna Docta akawa kavaa hzo kaundasuti Kuna nesi akamuuliza yule Docta "ebhna vip Leo mbona suti kubwa ... Jamaa akajibu sii unajua Leo Kuna wageni wanakuja Kwa hyo nimevaa hv kutishia kidogo daahh
Nikacheka sana😁😁
 
We vaa tu sutiKaunda nyoa kipara nenda kaunta kunywa WINDOKU ukiwa umesimama kaunta...macho yako yanaangaza angaaza kila kona
Utaona Wabongo wananong'onezana wengine hata kukimbia kaunta.....

MAUJIKO ..teh teh teh....yani kutisha tu watu
😅

Miaka ile polisi walikuwa wanaogopwa sana basi walikuwa na kile kiswahili chao ili aonekane polisi ,utasikia "Aroo wee ,hili lijamaa linajifanya jeurii"

Basi mtu akiongea hicho kiswahili watu wanamuogopa wanajua ni polisi.
 
Peace upon ya'all,

Ebwana ni ajabu sana mtaani ukipita mtu anaesemekana ni TISS hutukuzwa na hata watu wengine wengi hujifanya TISS ili kuonekana maalumu na kutafuta maujiko

Hata hapa jf wengi hujifanya TISS ili kujipatia ujiko ajabu ni kwamba kama ilivyo nesi, daktari, mfamasia, dentist n.k wako katika kada ya afya (health sector) au walimu, wakufunzi wako kada ya elimu (education sector) au kama marubani, airhostess, astronuts n.k wako kada ya aviation ndivyo pia askari magereza, polisi, askari jeshi, mgambo na TISS wote ni kada ya ulinzi.

Kimsingi TISS ni kada ya ulinzi kundi moja, taaluma moja na mgambo wametofautiana juristiction chache ila wana mengi ya pamoja kuliko utofauti. Hata kimaslahi TISS ni wakawaida sana na wamepitwa na kada nyingi tu na hamna maajabu yoyote kwa hawa walinzi.

Kama reporting TISS officer analipwa 1,850,000 (1.8M) mbona ni kamshahara kadogo kuliko hata lecturer wa chuo cha umma achilia mbali daktari mwandamizi au hata tu mkandarasi wa electrical installation wa mradai wa pale Stigler anaelipwa zaidi ya 3M.

Ni ushamba tu wa Watanzania kuona ati walinzi hawa ni watu wa hadhi kubwaaaa, na ujinga huo ndio unawafanya watu kama Sabaya mwaka 2018 - 19 kujifanya TISS huku akisafiri bure, na kupata huduma katika mahotel makubwa bure akiwaonyesha kitambulisho tu.

Kitu ambacho hata angekua kweli ni TISS hana upendeleo wa kupata huduma bure.
ZAMANI
-Walibeba magazeti na kujidai kusoma sehemu kwa utulivu,
-kuishi sehemu kimachalemachale hata kama ni kwake,
-kujidai mkimya na mwenye kutafakari sana hata ujinga,
-kuzoea kuwahi kwenye matukio hata arobaini mitaani.
KUMBE
-Ni akina Yahaya wote.
Walinzi oyeeeeee!
 
Peace upon ya'all,

Ebwana ni ajabu sana mtaani ukipita mtu anaesemekana ni TISS hutukuzwa na hata watu wengine wengi hujifanya TISS ili kuonekana maalumu na kutafuta maujiko

Hata hapa jf wengi hujifanya TISS ili kujipatia ujiko ajabu ni kwamba kama ilivyo nesi, daktari, mfamasia, dentist n.k wako katika kada ya afya (health sector) au walimu, wakufunzi wako kada ya elimu (education sector) au kama marubani, airhostess, astronuts n.k wako kada ya aviation ndivyo pia askari magereza, polisi, askari jeshi, mgambo na TISS wote ni kada ya ulinzi.

Kimsingi TISS ni kada ya ulinzi kundi moja, taaluma moja na mgambo wametofautiana juristiction chache ila wana mengi ya pamoja kuliko utofauti. Hata kimaslahi TISS ni wakawaida sana na wamepitwa na kada nyingi tu na hamna maajabu yoyote kwa hawa walinzi.

Kama reporting TISS officer analipwa 1,850,000 (1.8M) mbona ni kamshahara kadogo kuliko hata lecturer wa chuo cha umma achilia mbali daktari mwandamizi au hata tu mkandarasi wa electrical installation wa mradai wa pale Stigler anaelipwa zaidi ya 3M.

Ni ushamba tu wa Watanzania kuona ati walinzi hawa ni watu wa hadhi kubwaaaa, na ujinga huo ndio unawafanya watu kama Sabaya mwaka 2018 - 19 kujifanya TISS huku akisafiri bure, na kupata huduma katika mahotel makubwa bure akiwaonyesha kitambulisho tu.

Kitu ambacho hata angekua kweli ni TISS hana upendeleo wa kupata huduma bure.

Wewe una chuki binafsi na hao TISS pengine una mgogoro na mtu hicho kitengo. Myamalize tu nyie kiutuzima uache kupiga kelele hapa jukwaani.
 
Moja kati ya chief spymasters kwenye utawala wa stalin miaka ile aliyeitwa pavel sudoplatov, alikuwa alitoa ushauri huu katika kuwapata wale ambao wangejiunga na idara za usalama wa taifa la urusi kwa wakati huo likiitwa . Nkvd. Namnukuu ' search for people who are hurt by fate or nature-the ugly, those suffering from INFERIORITY COMPLEX, craving power and influence but defeated by unfavourable circumstances.... In cooperation with us, all these find a peculiar compensation. The sense of belonging to an influential and powerful organization will give them a feeling of SUPERIORITY over the handsome and prosperous people around them'... Kwa hiyo ukiona mtu ana pretend yeye ni tiss , tatizo linaanzia ndani kabisa!
 
Sabaya ni TISS kweli Wala siyo kujifanya.

Tatizo kubwa mmejengwa vichwani kwenu TISS ni watu genius na akili kubwa sana na hivyo mtu Kama Sabaya hawezi kuwa na kiuhalisia ndio usalama wenu hao.

Kwa lugha rahisi Sabaya nanyule aliyemtolea Nape bastola ni usalama ni vichwa pa
......Tatizo Kubwa Mmejengwa Vichwani Kwenu T-I-S-S Ni Watu GENIUS Na Akili Kubwa Sana......
 
Intelligence...aliyebobea utamtambuwa kwa Ufunguo unaoitwa INTEGRITY
Hata akiwa baa kuanzia unywaji wake ukaaji interaction yake na walevi wahudumu omba omba wanaopita kwenye baa ...kimatendo utaona kabisa kuna Nidhamu katika matendo yake...Hajikwezi...Hujiamini ..hutoa heshima bila kujali Mwonekano wako...Kifupi huyu mtu hujifyuzi kwa kila mtu iliye kwenye Duara lake.....anaweza kwenda kwa Dj akamwambia piga ngoma flan...then hiyo ngoma ikivurumishwa unaona baa yote IMEFAYAA....Kifupi hutumia saikoloji UMEME kujuwa uwepo wa kila mmoja hapo....

Hawa watu wanauwezo kutimba hata huko Goma na kuchukuwa Taarifa anayoitaka bila Valuvalu zozote.....

Cc Yericko Nyerere
 
Back
Top Bottom