Kwanini wengi wanapenda kujifanya TISS wakati kazi hii ni kada ya ulinzi kundi moja na mgambo?

wanajulikana sana tu sema ni kwasababu huna ndugu anae fanya kazi huko....! lakini sio kazi yenye usiri huo mnao dhani...! japo kuna baadhi ya mission sometime it coast someone to change the identity...ila haiondoi ukweli kuwa mke na watoto wanajua kuwa baba yao anafanya kazi gani...🤭

babu yangu tu Marehemu mzee Kitandu tulijua anafanya kazi ofisi ya Rais ila yule aliishi maisha ya uharisia ambayo huwezi kukisia kazi yake huyu mzee alinyweshwa damu ya bendera na uzarendo ukamvaa haswa nadhani ni product ya mwisho ya Nyerere 😭😭😭😭

tulikuja kugundua kuwa alikuwa ni TISS siku ya msiba wake msiba uligharamiwa na kitengo na kitengo kilikusanya nyaraka, hardcopy na computer zote za nyumbani kwake walipita nazo wakidai kuwa zilikuwa ni mali za ofisi...🤣🤣🤣

walifanya upekuzi nyumba nzima...nilikuwa karibu sana na Babu nakumbuka kuna mwana kitengo mmoja baada ya kugundua wanacho kitafuta awajakipata kwenye zile hardcopy na computer walizo chukua akawa ananifuata pale msibani akiniuliza ki uzushi

"babu yako kuna kitu alikuwa anaandika amekiandika kwa muda mrefu niambie lilipo hilo andiko"
 
Sawa tithi[emoji3][emoji3]
 
mzee anaumwa hadi anafariki hajui hilo andiko liko wapi na ni la muhim hadi anakuja kuzuga kwa wewe mjukuu? Hamna Tiss hapo.
 
Raia wa kawaida wanatakiwa wajue kuna chombo hicho na kazi zao msingi
 
1,850,000 daktari anayeanza kazi hana hiyo pesa. Wapo vizuri kumbe!
 
Endapo kama wangewafahamu vizuri hao tiss pamoja na "mambo yao yanayowahusu," watu wanaojifanya kuwa ni wafanyakazi wa huko wala wasingethubutu hata kujiita kuwa wao ni tiss.Hawajui tu watu hao. Wenyewe halisi waliopo huko wengi wao hawana furaha wala amani mioyoni mwao, wanatamani sana kutoka huko lakini wanashindwa kwa sababu tayari "wameshafunga 'ndoa ya kikristo' na shetani, hakuna talaka, ni kifo pekee ndicho kitakachowatenganisha." Ukweli ni kwamba wengi wao wanatamani sana kuvunja ndoa (talaka) hiyo mbaya na shetani ili wawe huru, lakini imeshindikana.
 
Sawa tithi[emoji3][emoji3]
sina utithi wowote nahangaika tu...ila kupitia katiba yetu kama wewe na Mtanzania wewe pia ni TISS no.1. maana katiba inaweka wazi kuwa juku la kuilinda nchi yetu na mipaka yake ni la kila mtanzania.

kwa kigezo hicho wote sisi ni TISS kasoro wengi hatuna vitambulisho tu vyekundu na vyeti vya mafunzo ya nyongeza...!​
 
Mnawakuza sanaaaa
Mapopo tuuu
Mtaani tunaishi nao

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…