Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 3,114
- 6,309
Habari wadau,
Nianze na mzizi wa umaskini unatoka wapi: Na mzizi wa umaskini haupo katika aina ya kazi, haipo katika chanzo cha kipato. Uhusiano kati ya unachotengeneza na unachokitumia ndio mzizi ulipo.
Je unachotengeneza na unachotumia inamaana gani?
Kutengeneza thamani maana yake ni kwamba kupata matokeo ambayo output ni zaidi ya ulichokiwekeza(input). Mkulima aliyepanda mahindi na kupata mahindi mengi ametengeneza thamani. Dalali ambaye ananunua mahindi Sumbawanga na kuuza Dar es salaam ametengeneza thamani. Kutengeneza thamani(Value Creation) ni shughuli yoyote inayozalisha matokeo makubwa zaidi kuliko uwekezaji.
Kutumia thamani maana yake ni kuchukua ulichokipata(matokea baada ya uwekezaji) na kutumia. Mfano: Unalipa kodi, Nguo unazovaa, Burudani unazoangalia, Gari ulilonalo la kutembelea, Chakula unachokula.
Kihisabati tunaweza kuwakilisha maana hizi kama ifuatavyo:
Kama Thamani iliyotengenezwa > Thamani iliyotumiwa --> Utajiri unatengenezwa
Kama Thamani iliyotengenezwa = Thamani iliyotumiwa --> Unaishi lakini hamna maendeleo
Kama Thamani iliyotengenezwa < Thamani iliyotumiwa --> Unaingia katika madeni na kukaribisha umaskini.
Watu wengi maskini, licha ya kipato wanachotengeneza, wengi wanaishi kwenye mstari wa tatu au wa pili wa equation zetu hapo juu sio kwasababu ni wavivu, wala sio kwasababu hawafanyi kazi. Lakini kuna gap kati ya thamani wanayotenengeneza wana wanayotumia.
Mfano ambao mwepesi unaoelezea maelezo hapo juu: Baraka na Hassan
Hassan na Baraka ni wafanyabiashara wote wapo Pwani. Wana mtaji sawa(500k, bidhaa sawa, location sawa, wateja sawa.
Baada ya miezi 6, Baraka yupo sokoni na 500,000. Haendelei. Hakui. Anafanya kazi kila siku kama alivyoanza.
Hassan sasa ana Million 1 na laki 2 kama mtaji wake. Na amefungua sehemu ya pili ambayo inaendeshwa na mdogo wake.
Ni nini kimetokea?
Angalia gap kati ya uzalishaji na matumizi.
Baraka anatengeneza 80, 0000 kama faida week ikiwa vizuri. Samaki wake wanatengeneza pesa nzuri, ananunua kwa bei ya ziwani na kuuza kwa bei ya sokoni, utofauti ni thamani iliyotengenezwa. Lakini, Baraka ananunua nguo mpya za weekend, anatoka na marafiki zake out na kuspend pamoja, anatuma pesa nyumbani kwa ndugu zake kwasababu walisikia anaendelea vizuri, amebadlisha simu yake na kununua mpya na kila Jumatatu anahitaji mtaji wa kuchukua samaki ziwani tena. Matumizi yake yamekula kila alichozalisha. Anaendelea kuishi lakini hamna utajiri anaoutengeneza.
Hassan anatengeneza sawa na Baraka 80,000 Tsh kwa week nzuri. Lakini amejitengenezea sheria: anatumia 35,000 ya faida tu. Inayobaki 45,000 anafanya kama haijawahi kutokea. Hasherikei hela yake kwenye umati. Anajishusha na kujifanya kwa ndugu zake "Biashara haiendi hadi mwezi ujao". Baada ya miezi sita na kuwa na hela ya kutosha kununua jokofu la kutunzia samaki, ambalo linamfanya anunue samaki wengi na wakae muda mrefu, hii inamaanisha Hassan anaweza kufanya mauzo kwa ukubwa zaidi. Anawekeza faida anayoipata kwenye uwekezaji wake apate zaidi.
Hapo wazee hamna cha bahati. Wala kipaji. Wala Connection yeyote. Wala roho/laana.
Huu ni mfano wa umaskini ulivyo na utajiri kwa namna rahisi zaidi.
Wadau tutaendelea kipindi kijacho: Usisahau kuweka maoni, kuongezea point au kama kuna swali tafadhali tushirikishe hapo chini.