Kwanini wengine wawe na vitambi au wanene nawakati tunakulanao aina moja ya chakula?

Kwanini wengine wawe na vitambi au wanene nawakati tunakulanao aina moja ya chakula?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Hii hoja naileta kwenu kwa wataalum wa afya ili mpate kutuletea majibu stahiki,kwani asilimia kubwa ya watu tunaokaanao tunafanana lifestyle ya chakula, lakini utakuta mtu anahangaika na kupunguza unene ama kitambi na wakati huohuo kuna mtu anakaanae na kwa asilimia kubwa wanashare kinachutua mezani lakini mmoja ni mnene/anakitambi na mwengine hana!.

Doctors kwanini iwe hivyo?
Au na sisi binadamu ni species zenye aina tofautitofauti katika kukabiliana na chakula?

Nasubiri majibu yenu yenye maelezo ya kina, hii itasaidia wengi nakujua mtu aishi life style ipi ili aepuke mambo fulanifulani ya kiafya karibuni.
 
huku tukiwa tunawasubiri,niliwahi kusoma mahali wanadai sababu kubwa ni kwamba miili yetu inatofautiana na pia sababu nyingine unakuta mmoja anajishughulisha hivo mwili unapata mazoezi kuliko wa mwingine
Haha! Mkuu Kuna watu hawajishughulishi na hawana vitambi mlo anaotafuna Sasa.. nyama choma kwa wingi,bia,wanga Kama wote,tuweke na mdudu au tumtoe..?😂
 
Haha! Mkuu Kuna watu hawajishughulishi na hawana vitambi mlo anaotafuna Sasa.. nyama choma kwa wingi,bia,wanga Kama wote,tuweke na mdudu au tumtoe..?😂
basi hiyo inaweza kuangukia sababu ya kwanza niliyoitaja hapo juu kwamba mwili wa mtu tu,kuna kajamaa pia nilikaa nako nyumba fulani tulipanga kanapiga ugali mkubwa sana asubuhi kama break first alafu around saa nne kanakula nusu mkate
 
basi hiyo inaweza kuangukia sababu ya kwanza niliyoitaja hapo juu kwamba mwili wa mtu tu,kuna kajamaa pia nilikaa nako nyumba fulani tulipanga kanapiga ugali mkubwa sana asubuhi kama break first alafu around saa nne kanakula nusu mkate
Usikute tunatafuta alien kumbe tupo nao humuhumu!,halafu tumtu twa hivyo hata nguvu huwa hawana ila mikwara sasa kuugua hata korona ni shughuli pevu..😂
 
Hii hoja naileta kwenu kwa wataalum wa afya ili mpate kutuletea majibu stahiki,kwani asilimia kubwa ya watu tunaokaanao tunafanana lifestyle ya chakula,lakini utakuta mtu anahangaika...
Ni kuwa wengi wana ma-minyoo,tegu na safura tumboni ndo maana hawanenepi
 
Kiufupi wanamifugo..?😂
Doctors ya kweli haya..?
Tegu.jpg
 
Hii hoja naileta kwenu kwa wataalum wa afya ili mpate kutuletea majibu stahiki,kwani asilimia kubwa ya watu tunaokaanao tunafanana lifestyle ya chakula...

Kitu cha kwanza kuelewa ni:
Unene wa mtu hutokana na vyakula vyenye asili ya wanga(wali, ugali, viazi, ndizi etc). Hii hutokana na uwiano uliopo kati ya aina ya kazi unayoifanya/matumizi ya nguvu dhidi ya kiasi cha chakula/nguvu/wanga unazoingiza mwilini.

Mwili unapopokea nguvu hizi/ kutoka kwenye wanga, kuna vitu viwili tu ambavyo huweza kufanyika:
1: nguvu kutumika/kwa kufanya kazi
2: nguvu kutunzwa kwa pale zinapokuwa ni za ziada.

Ili kutunza nguvu hizi ambazo hutunzwa kwenye mfumo wa mafuta, miili yetu ina receptors/ vipokea maagizo ya kutunza mafuta.

Kuna watu wana receptor ambazo zina njaa zaidi/uwezo zaidi/hazishibi haraka hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kila kiasi cha mafuta yanayipatikana. Hapa ndipo masuala ya urithi wa unene huanzia. Ukirithi hizi receptor zenye kiu/njaa sana ya kutunza mafuta, ujue ni rahisi sana wewe kunenepa maana kila jinachopatikana hutunzwa kwa kiasi kikubwa.

Hivyo, utunzaji wa mafuta huamriwa pia na amri iliyoko nyuma ya hizi receptors.
Screenshot_20220111-073834.png
20220111_074823.png
 
Kitu cha kwanza kuelewa ni:
Unene wa mtu hutokana na vyakula vyenye asili ya wanga(wali, ugali, viazi, ndizi etc). Hii hutokana na uwiano uliopo kati ya aina ya kazi unayoifanya/matumizi ya nguvu dhidi ya kiasi cha chakula/nguvu/wanga unazoingiza mwilini...
Duh! Ahsante kwa ufafanuzi mkuu.

Tuttie receptors zako zenyewe ni korofi mbona..?😂
 
Back
Top Bottom