Hii hoja naileta kwenu kwa wataalum wa afya ili mpate kutuletea majibu stahiki,kwani asilimia kubwa ya watu tunaokaanao tunafanana lifestyle ya chakula...
Kitu cha kwanza kuelewa ni:
Unene wa mtu hutokana na vyakula vyenye asili ya wanga(wali, ugali, viazi, ndizi etc). Hii hutokana na uwiano uliopo kati ya aina ya kazi unayoifanya/matumizi ya nguvu dhidi ya kiasi cha chakula/nguvu/wanga unazoingiza mwilini.
Mwili unapopokea nguvu hizi/ kutoka kwenye wanga, kuna vitu viwili tu ambavyo huweza kufanyika:
1: nguvu kutumika/kwa kufanya kazi
2: nguvu kutunzwa kwa pale zinapokuwa ni za ziada.
Ili kutunza nguvu hizi ambazo hutunzwa kwenye mfumo wa mafuta, miili yetu ina receptors/ vipokea maagizo ya kutunza mafuta.
Kuna watu wana receptor ambazo zina njaa zaidi/uwezo zaidi/hazishibi haraka hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kila kiasi cha mafuta yanayipatikana. Hapa ndipo masuala ya urithi wa unene huanzia. Ukirithi hizi receptor zenye kiu/njaa sana ya kutunza mafuta, ujue ni rahisi sana wewe kunenepa maana kila jinachopatikana hutunzwa kwa kiasi kikubwa.
Hivyo, utunzaji wa mafuta huamriwa pia na amri iliyoko nyuma ya hizi receptors.